Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikifanya hivyo nakuwa naudanganya moyo wangu tu mkuuUngemsamehe 2
Mwanaume anaweza kuuchukua huu ushauri?Rafiki HakiKwanza_2015 nikujuze tu swala la kuridhisha/kuridhishwa sio tatizo bali ni mtazamo.
Ukiwa na mtazamo chanya na huyo mtu wako hakika utaibua hisia njema za mapenzi nae. Na hata ukilala nae haihitaji upigwe jerk kwa muda mrefu ili uridhike.
Kuwepo nyumbani tu kusifanye uchepuke. Hapana ni kweli ukila ukashiba na huna kazi za kufanya basi wazo la mapenzi Huwa linachukua sehemu kubwa. Hivyo basi...
Jikiweke katika Hali ya kujishughulisha na kazi ndogo ndogo ikiwemo kutunza mazingira ya mji wako au hata kutumia muda kufundisha wanao au kufanya nao homeworks.
Karibu sana.
Jibu swaliWewe ni Ke Au Me?
Waje waje. Nimefurahi kuona baadhi ya watu wamejaribu kuandika japo ni katika comments. Hii ni safi.Sema nao wanawake wakija na uzi za kutoka wa Waume za watu.....Naamini pasipo na shaka lolote Server za JF zitajaa maana katika wanawake 10 hawa Gen z 8 wanatoka na waume za watu.
HakiKwanza_2015 nimekuuliza ili nijibu swali lako. Karibu.Jibu swali
Ahsante sana Barakoa. Hakika nilikua bwege wa mapenzi. Ilikua darasa zuri kwangu lakini. Ni gharama niliolipa kufika maturity level niliopo sasa. Ile Link ya vijana ktk Bonus Episode Ina jambo letu kaka. Karibu sana.Mtiririko mzuri, unadishi makini na mafundisho yaliyobebwa, yamefanya simulizi hii kuwa isiyochosha, yenye mafunzo na kuburudisha. Japo wivu wako dhidi ya mali ya wizi kuna wakati ulikuzidi msimuliaji. Tunashukuru hasa kwa Bonus Episode.
BalaaaTuendelee EP 06
Kweli nikaweka mambo yangu sawa kisha nikaitikia wito. " Babaa nina mimba...ila sijui ina muda gani". Akaendelea " nimetoka kupima muda nakupigia simu ". Mimi "kipimo kipo wapi naomba nione". Recho " kwani hata nimeipata nguvu ya kukitunza...nilivoona majibu nikakiflash chooni kabisaa!!. Mungu wangu!?!!".
Nilipatwa na hisia mbili kwa mpigo. Moja, sasa huyu ni mke wa mtu tutafanyaje, huzini. Pili, ilikua ni hisia za furaha kwamba kumbe uwezo upo. Mpaka naweza kutia mwanamke mimba, ewaa safii.
Mimi " naomba Ile dawa tulionunua juzi". Akaieleta na nikaanza kusoma maelezo kwa mtumiaji. Kweli bhana haitakiwi kutumiwa na mjamzito. Hapo nikajiridhisha ni kweli huyu ana mimba ndio maana baada ya kutumia tu hali yake ilikua mbaya. Wakati napitia yale maelezo ya Ile dawa, Recho alisoma uso wangu na kungundua kuna kitu nilikua nawaza.
Recho " unawaza nini my love...please niambie!". Mimi " nipo sawa ila nimeona hapa ni kweli hii dawa haifai kwa mjamzito". Recho " Em nione... na kwelii maana badala ya kupata haueni kidogo nife".
Hii dawa sitaitaja jina. Ila nafikiri kwa mjamzito inaweza toa mimba na hata kusababisha kifo ingawa sina uhakika sana kuhusu kusababisha kifo.
Baada ya kujiridhisha kweli Recho kashika mimba mjadala uliofata hapo ni tutafanyaje. Ipo wazi kwamba Mimi ni jobless na yeye ni mke wa mtu. Je atoe au alee mimba?. Kwa namna yoyote' hakukua na option ya ziada zaidi ya kutoa mimba kwa maslahi yetu wote wawili , lakini yeye zaidi kulinda ndoa yake.
Nikurudishe nyumba kidogo. Nilisema hali ya kumpenda kwa dhati Recho ilianza kuibuka siku hadi siku sio kwasababu ya sex pekee. Sasa ilikua hivi.
Kama wiki moja kupita toka tuanze wizi, Recho alianza kuniulizia habari za kutafuta kazi na hata palipo hitajika support ya pesa ili kufanikisha harakati za kutembeza bahasha yule dada alijitoa kwa dhati.
Maneno kama " hujachoka kula ugali wa shikamo".." tafuta kazi babaa sikumoja uje uwasaidie wazee wako hasa mama", ni kauli ambazo zilikua zikijirudia kwenye akili yangu na kusababisha nione huyu mwanamke ana kitu".
Recho hakuishia hapo tu, alifika hatua ananiamba " kama hujatuma maombi/application yeyote leo hunikuliii". Na hapo atakomaa mpaka nimpe ushahidi, kama sio email nilizotuma basi copy za barua nilizopeleka kwa mkono. It was really funny but potential somehow. Hakika ilikua kama masihara lakini yenye faida.
Hapa vijana tuongee jambo, ni kweli unapenda mashuga mamy ya kulee ni sawa. Au wake za watu kwasababu hawana gharama kuwatunza ni sawa pia lakini amini mwisho wa mahusiano utabaini umepoteza zaidi kuliko kupata. Why?
Sugar mamy atahitaji umtimizie haja za mwili na si vinginevyo. Pesa atakupa ndio, kitu ambacho kitakulemaza au kukufanya kuwa tegemezi pasipo kuchangamka/kupambana wewe kama wewe kupata chako kitakacho dumu.
Hio ni moja lakini pili, Hilo li jimama lina watoto au familia tayari yani maanake hadaiwi kuzaa zaidi ya kula maisha. Je kwako wewe ambaye unamwaga maji ya ujanani yenye uwezo mkubwa wa kukupa watoto kila wiki una uhakika utabaki rijali hivo mpaka utakapo oa ?
Jibu rahisi ni Hapana. Uwezo lazima utashuka kwasababu ya kutumika sana. Hapo magonjwa ya zinaa nimeyaweka kando. Fikiria Hilo kisha chukua hatua.
Ok tulitoka nje ya kisa kidogo lakini ni kwa manufaa ya Adam. Turejee, kutokana na Hali ya Recho kuonesha langu lake lake langu nilijipata nampenda sana. Na ndio maana sasa baada ya Nailah kuleta shida Ile siku nikamplease kwa udhaifu mkubwa. Hivyo suala la yeye kushuka mimba yangu lilinipa furaha zaidi kuliko mawazo kitu ambacho Recho hakujua. Kweli mapenzi ni upofu.
Tukakubaliana atoe ila nimtafutie elfu hamsini tupate dawa ya kutolea. Kwa wakati ule ni kweli kuna kimchongo part time nilikipata kutokana na Ile pushing efforts zake kuhusu kazi kwahio nilimudu kupata hio pesa. Mimi " Sawa hio pesa unahitaji muda gani?". Recho " ikipatikana mapema ni sawa zaidi ili nimuagizie mtu then nitameza usiku".
Nilimpatia hio pesa majira ya mchana na nilipofika kwake nikakutana na habari nyingine mpya. Sasa hii habari ikaniondolea furaha na kuleta hisia mbaya.
Recho " me sielewi hii siku ina nini". Mimi "Kuna Nini tena mamaa, mbona sikuelewi?". Mume wangu kasema anakuja mwezi huu au ujao sijui itakuaje!?!". Hapo ndio nikaamini huyu ni mke wa mtu. Na nilishindwa kuhimili Ile taarifa nikanyongonyea mpaka dada wa watu akaogopa.
Recho " sasa mbona unakua hivo my love... kwani nimesema tutaachana?!.. hapana nimekwambia tu ili ujue". Mimi "Ooh! Sawa!" Huku nikishusha mpumzi kubwa. Nakaaga nikaondoka lakini Recho alinotice sikua sawa.
Swala la mimba likakosa mashiko badala yake huzuni yangu niliyonesha baada ya kutaarifiwa ujio wa mkuu wa kaya ukachukua nafasi zaidi kichwani kwa Recho. Tuliwasiliana mpaka saa 4 usiku na tukaagana vizuri. Sasa ni saa sita usiku Recho ananipigia tena , napatwa na hofu, je anataka kuniambia Nini....
Shem imebidi nisome, story tam unahisi upo ndani yake.🤣🤣
😅😅😅😅Shem imebidi nisome, story tam unahisi upo ndani yake.🤣🤣
Usiku nilipitia ile ya Patrick, nayo nzuri balaa, hawa jamaa wanajua kusimulia.
Mbona naona wenzetu wana bahati sana kupendwa, sisi wengine tuna nini???
Ukipata mda pitia hapo, kuna kina Mary, Recho na Grace🤣🤣😅😅😅😅
Hii story nzuri sana Shem...
Hiyo ya Patrick sijaiona..
Huu ushauri wa kuwafundisha Imani zao na ili wawe na hofu ya mungu kweli kbsaa. Mwanamke akiwa na hofu ya mungu hawezi kuchepuka hata awe mpweke kiasi gani.BONUS EPISODE
HIVI NDIVYO TUNAVOCHEAT, PALIPO NA VIATU VYA MUMEWE KUNA NDALA ZANGU story ya kweli kati yangu Hovering na Recho ambaye ni mke halali wa mtu. Nimeileta kwenu kama sehemu ya kuonesha nini kinatokea linapokuja suala la kutoka nje ya Ndoa iwe kwa maksudi au bahati mbaya.
Kama ilivyo kwa wengi ambao tukisoma habari za uchawi tunahisi ni uongo au kuchanganyikiwa kwa mtu mpaka likukute, ndivo ilivo katika mapenzi ya aina hii. Wengi hushindwa kuamini habari za fulani ana chepuka na fulani mpaka tukio la kufumaniwa/kufumania likukute.
Andiko langu halichochei wala kuchagiza ukosefu wa uadilifu kwenye mahusiano halali hapana. Nimetoa picha kwa uchache namna mambo yanavyokua walau kwa kusoma tu upate ABC, Mimi nikiwa kama muhusika mkuu.
Kupitia 'comments' nimeona watu wakitoa hisia zao na mawazo yao kila mtu kulinga na alivyoitafsiri stori na hii inatoa picha halisi jinsi gani haya mambo ni kweli yanatokea katika jamii na yanatugusa.
Bwana mmoja nimuhifadhi ID yake naona nilimgusa kiasi cha kunitishia nisiendee na kisa. Wapo waliofurahi na kutamani stori iendelee. Haya yote nimeyapokea.
Na hii sasa ndio imenishawishi kuongeza kipande hiki walau nizungumze na makundi makubwa matatu. Mosi ni sisi vijana. Pili, wanawake waliopo ndani ya mahusiano hususa ni ndoa, uchumba nk na mwisho nimalize na sisi wa baba/watu wazima tulioa au lah.
Karibu sana tuzungumze kupitia kundi lako.
Vijana
Imekuwa ni kawaida kabisa kukuta vijana wa umri kati ya miaka 23 hadi 35 wanatambiana kulelewa na wanawake wanaojiweza kiuchumi na umri mkubwa, huku wengine wakibaki wanajiuliza hizo 'bahati' wenzao wanazipata vipi.
Kwa kifupi kweli ni 'bahati' lakini ni 'bahati mbaya'. Kwanini ni bahati mbaya nimekuweka link ya Uzi wangu pendwa. Hapo naamini utajiona upo salama au lah!.
Nisingeamua, ningeacha kimemo kama Katibu
Wanawake ndani ya Mahusiano.
Kuwekwa ndani ya nyumba, kuaminiwa na mwanaume umzalie watoto, kuhudumiwa kwa kadri ya uwezo wa mwanaume wako ni dhamana kubwa ya mwanaume dhidi yako.
Ni kweli inawezekana umeolewa kwasababu kadha wa kadha ikiwemo unafuu wa maisha, kulazimishwa ndoa na sio hisia nzito za mapenzi juu ya mmeo lakini heshimu hio dhamana alioibeba kwajili yako.
Unaheshimu vipi. Ni kwa funga milango au mianya yote inayoweza kukuonesha mapungufu ya mtu wako. Kuna kina Z wengi sana katika jamii ambao malengo ya hua ni kupiga na kuondoka na hakika show zao ni kuntu lakini je mwisho wa siku Z wako ataleta ugali mezani!?
Jibu ni Hapana, basi jaribu kadri ya uwezo wako kumuheshimu anaeleta huo ugali mezani.
Toka naanza simulizi mpaka namaliza nimekuonesha jinsi mchango wa kuwa na kitu cha ziada mbali na sex kwa mtu wako kunavyoweza kugeuza akili yake na kuteka hisia zake za kimapenzi. Basi ichukue hio. Nayo ni silaha makini.
Kwa Wababa, wakuu wa kaya.
Nadhani kupitia stori tumeona namna Recho mke wa mwanaume mwenzetu alivoshawishika kutoka nje ya ndoa yake. Upweke!!
Wapo wanaume ambao kutokana na stori wameanza kuhisi wake zao bia shaka wanatoka nje. Hapana wapo wanawake wenye upendo wa dhati na hofu ya Mungu, hao wanaweza kutetea heshima yako na ukabaki mshindi daima.
Lakini pamoja na geti lako kubwa na uzio uliozungushia kwako hio bado haitoshi mke wako anaweza kuliwa ndani hapo hapo kwako.
Mtu mmoja katika 'comments' aliuliza "hivi na huyu wangu( akimaanisha mke wake) analiwa...mbona haioneshi hata dalili".
Jibu la swali lake ni 'uwezekano upo'. Hata huyo mlinzi uliyemuweka getini akulindie mji anaweza kuwa wa kwanza kuwa mwizi wa mkeo. Hapa namaanisha, mwanamke kuchepuka anaamua muda wowote mahali popote.
Basi nini tufanye.
Nashauri tuhimize familia zetu (watoto pamoja na mama yako) kuhudhuria ibada pamoja na mafundisho ya kidini kwa Imani zetu.
Hii Inasaidia kujenga hofu ya Mungu ndani mtu, Hali itakayomfanya kuhisi hatia dhidi ya mola wale pale anapotaka au kwisha kuteleleza dhambi .
Pili, hizi ni zama za ukweli na uwazi.
Ongea na mwanamke wako kuhusu athari za kutoka nje ya Ndoa na msimamo wako ni upi likijitokeza hilo. Kuwa muwazi kwa kumuelimisha mtu wako.
Nilisema ndani ya kisa mwanamke kaumbwa kama msaidizi kwa mwanaume yaani mfuwasi hivyo zungumza kiume pale unapokuwa una address swala nyeti na zito kama hio. Utaeleweka vizuri sana.
Mwisho, Acha kuchunguza simu ya mkeo mara kwa mara na badala yake focus zaidi kwenye kumstaajabisha kwa zawadi na show safii na kufurahia penzi. Isipokuwa ichunguze mara chache na kwa ambush.
Vilevile weka utaratibu wa kucheck afya mara kwa mara hasa unapokua umetoka safari. Nakukumbusha Recho alitoa mimba kipindi mkuu wa kaya yupo nje masomoni.
Lakini hakikisha kipindi cha joto cha mkeo ndani ya mwezi unakuwa karibu. Hii itapunguza zile sababu za kimazingira zinazoweza kuwawezesha kina Z wakapita na gap.
Kwa maoni na ushauri, PM wakati wowote.
Bonus Episode marks the End.