Haihitaji kujua hesabu, tumia fomula niliyoweka hapo kwenye link. Halafu kuna vingi vya kujifunza hapa zaidi ya hiyo hesabu moja.
Kama unasema haiwezekani endelea kulalamikia maisha halafu baadae utatuambia kulalamika kwako kumekusaidia nini.
Miaka 20 au 30 nimetumia tu kuonesha ukuaji, target kubwa ni miaka mitano au kumi ambapo mabadiliko ya fedha yanakuwa sio makubwa sana na unaweza kuendelea kujifunza kuhusiana na biashara husika.
Milioni kumi ya mwaka 2009 na milioni kumi ya leo ina tofauti gani kwenye kuanzisha biashara? Ipo lakini sio kubwa sana kiasi cha kukufanya ushindwe kuanza biashara.
Tatizo kubwa la watanzania ni kutokujifunza na kuishi kwa mazoea tu na mwisowe kusema kitu hakiwezekani kwa sababu wewe hujawahi kufanya au hujawahi kumuona mtu anafanya.
Kwa miaka mitatu iliyopita nimesoma vitabu karibu mia tatu, sasa unasema kwa kujiamini kabisa kwamba miatano haviwezekani?
Nakuambia uweke elfu moja pembeni, elfu moja ambayo ungekunywa soda isiyo na maana kwenye maisha yako au kutumia hovyo tu na baada ya muda itakua na kufikia kiwango kikubwa kidogo, unasema pia haiwezekani?
Naweza kukuambia neno moja tu, KAFE MASIKINI.
Nduhu uliyeanzisha hii tread umeongea vitu vya kweli kabisa na nina kuunga mkono asilimia 100.
Tatizo la watanzania ni la muda mrefu sana, tangia utoto hatijapata elimu za muhimu kwa mfano kuhusu mambo ya pesa au kujisomea.
Mimi binafsi nimejifunza mambo mengi yaliyonibadilisha kutokana na kusoma, Bill Gates mwenyewe anasoma kitabu kimoja kila wiki, jiulize mpaka leo amesoma vitabu vingapi?
Naamini kabisa kuwa kipato chako kinaweza kulingana na mambo uliyojifunza kwenye maisha. Yaani kichwani una nini? Ndio maana yake hiyo. Wanaojua vitu vingi wanapata hela nyingi. Period.
Watanzania wengi wameshakubaliana na hali walizonazo, wana taka slope tu. Kujitaabisha wala!
Mkuu unaweza kuisoma vizuri hii makala na kuielewa ndio uweke post? Maana hakuna sehemu niliyosema uweke buku akiba nimekuambia uiwekeze hiyo buku sehemu inayokua.
Halafu hebu niambie unawezaje kuizungusha buku ukapata faida?
This is very unrealistic.. My Arguments are;
1. Kusoma vitabu 100 ndani ya mwaka mmoja ni jambo lisilo na faida yeyote.. Ideas gani unazitafuta kenye vitabu 8 kila mwezi?? Je, ikifika December utakikumbuka ulichokisoma the first week of January?? Kwangu ni bora uchague vitabu 6 vizuri usome 1 taratibu kwa miezi miwili, hapo utapata muda zaidi wa kukichambua kitabu vizuri..
2. Kusikiliza audio books kwenye daladala zetu za kibongo hapohapo ukapata point ya kinachoongelewa ni kujidanganya.. Audio books zinahitaji concentration ya hali ya juu, ni sawa na mtu anayeenda na madaftari club akitegemea atasoma akaelewa..
3. Kusoma vitabu 500 na kuweka 1000 kila siku kwa miaka mitano is another unrealistic thing.. Let's say kila kitabu kina mawazo matatu mazuri, which means ubebe mawazo 1500 ili baada ya miaka mitano uanze kuyafanyia utekelezaji ni kujidanganya na kuchosha akili bure..
4. Hiyo hoja yako haina tofauti na kitu kinaitwa "pig bank", its obvious that ni ngumu kwa mtu mzima anayetegemewa kuweza kuyatekeleza hayo, kuna mambo ya muda (kuhusu vitabu 500) na matatizo mbalimbali, hivyo hii idea ni nzuri kuwafundisha watoto wetu, mfano kwa mwaka wa kwanza unakua unamwekea mia 5 kwenye kibubu then unampa task ya yeye kufanya hivyo kwa miaka kumi, ikiwa kila ikifika birthday yake mnakivunja na kuhesabu then unaenda kumwekea kwenye account yake. Hii itamjenga ajue saving na pia akiendelea hivyo mpaka anamaliza university atakua na mtaji mzuri tu (sasa hapo he/she can decide kujiajiri ama kuajiriwa).. Kwetu sie watu wazima ni ngumu
Pia, naona una malengo yako binafsi kwenye hii elimu unayoitoa, kwanini watu wakikataa hoja yao unaleta maneno ya kejeli na unajibu kwa ghadhabu?? Kwa maisha ya watanzania hiyo njia yako ni ngumu mno, na ambao wanaweza ndio kama huyo mkuu hapo juu aliyesema mtakua exceptional.. Kuna njia nyingi za kupata mitaji na kutajirika... Si Bahressa, Mengi wala Patrick Ngowi ametumia hizo njia zako lakini they are known all over (Forbes). So, MTU kukataa hoja yako haina maana atakufa maskini, futa hiyo kauli yako, si ya kistaarabu kutolewa na mtu kama wewe
Bil gates huwezi kumlimganisha na mtanzania.
Mtanzania anasomea vitabu vya udaku.
Bill gates anasomea vitabu vya kimaarifa zaidi.
Hapo ndio usipopajua kabisa.
Hata ukienda kariakoo 89% ya vitabu utakavyovikuta havina tija za kimaisha.
Bill gates anaenda kukodi kitabu maktaba ambacho ni sawa na masomo yetu ya chuo kikuu ya mwaka mzima.
Binaadamu kamwe hawezi kubakia nyuma ikiwa maarifa yake ni makubwa.
Mkuu unaposema unrealistic ni kwa upande wako, yaani sema wewe huwezi kwa sababu hizo ulizozitaja hapo juu, which is very right.
Sijamjibu mtu kwa kejeli kwa sababu yoyote mbaya ila ni kwa kauli hizi mnazotumia kwamba HAIWEZEKANI itakuwaje haiwezekani nawakati mimi binafsi nafanya? Hapa ndio nashindwa kuwaelewa, kama wewe hujawahi kufanya kitu au hujawahi kumwona mtu akifanya haimaanishi kwamba haiwezekani. Ila wewe mwenyewe ndio huwezi.
Kufa masikini kunaanza hivi, badala ya kusoma hoja kama hii halafu ukaangalia ni jinsi gani unaweza kuifanyia marekebisho na ikawa na faida kwako(i agree nothing work to everybody) mtu anakimbilia kusema tu haiwezekani na haiwezi kutokea. At the same time itamkuta mtu huyo analalamika maisha magumu au ajira inamsumbua, sasa what left for this fellow? Ni kufa masikini kwa sababu tayari ana negative mentality, hayuko tayari kujifunza kitu kipya.
Kwa mfano sio lazima uweke buku kama nilivyosuggest, sio lazima uweke miaka mitano, kumi, thelathini au hata sitini ijayo. Swali ni je una utamaduni wa kuwekeza kipato chako sehemu ambayo kinaweza kukua taratibu wakati wewe unaendelea na mambo mengine? It turns out kwamba watanzania wengi hawana itaratibu huo. Mtu anapokea mshahara ndani ya soku kumi umeisha anaanza kiukopa, akipokea mshahara mwingine analipa madeni halafu anaanza tena kukopa? Sasa hayo ndio maisha?
Kuhusu kusoma vitabu 500 inawezekana, sema wewe huwezi. Sasa basi kwa sababu huwezi kusoma 500 hebu tuambie wewe bimafsi kwanzia mwaka huu umeanza umeshasoma vitabu vingapi both for your professional na personal development? Kama hujasoma hata kimoja nafikiri nisingekuwa na haja ya kiukuambia haya yote maana ukisoma na kumaliza utajuabkwa nini nakwambia 500 inawezekana.
Umesema kuna njia nyingi za watu kupata mitaji, hebu tusaidie njia tatu ambazo ni realistic kama ulivyosema kwa mtanzania mwenye kipato cha chini anazoweza kitumia kupata mtaji wa kuanzia biashara.
Halafu unaposema mengi ja bakhresa hawakuanza hivyo sifikiri uko sahihi, wote tunajua these guys walianza chini sana doing very odd jobs na waliweka servings kwa kiwango kikubwa sana ndio maana wakaweza kuingia kwenye biashara.
Asante.
Kiddo, if you think the mar in your computations doesn't affect and nullify your advice then you are a long way from home. Hiyo computation ndio foundation ya argument yako na advice yako, na ina makosa. Go find something to do. Sio unapoteza muda hapa trying to give people advice ya vitu ambavyo hata wewe mwenyewe huelewi.
hu ndo upumbavu.....yani nitunze pesa ili nije nipate mtaji nikiwa nina miaka 60 sa kama nkifa au kama idea yangu ya biashara ambayo nnayo sa hv ndo itahit market so itabidi nisubirie mpaka hiyo miaka 10 au 20......kingine ni suala la inflation hiyo million 26 inaweza kuwa na thaman kubwa sasa hivi lakini ifikapo miaka 20 ijayo itakua na thamn gan......i hink me na unfa mkono kwa wale waliosema hili jambo ni unrealistic......kingine huu mfuko sio kwa ajili ya kusaidia middle class or the poor.....hii ni kwa ajili ya kuwapa mtaji the rich clas ambao wanamiliki huo mfuko
Umasikini sifi nao lakini njia yako situmii samahani kwa hilo![/QUOTE
mimi nimeweka vipande huko kwa kweli watu hawajui tu kuna faida na nikauliza dse stock of exchange wanasema watanzsnia wengi hawanufaiki na soko ls hisA ila wageni ndio zaid.kuna mtanzania aliweka kdogo kdgo akafikisha mil kumi baada ya miaka mitatu akapata mil120 anaitwa emiliani busara na kaandika vitabu vizur sana vya uwekezaji tafuta kwenye maduka pale mliman site na eagt city centre kwa pastor katunzi sabasaba utavikuta bei kuanzia elf tano ni vizur sana.
Mkuu, tofautisha kati ya UTT na DSE. DSE kunaweza kulipa zaidi ukicheza karata vizuri. Na ukicheza vibaya unaptoeza chote. UTT kuna usalama zaidi ila faida kidogo.