Hivi ndivyo wanaofurahia uzinzi, ulevi na dhambi nyingine watakavyoteseka milele

Ingawaje sijasoma nikamaliza naomba kuuliza swali

Mi nikiamua kula bata la maana kabisa hadi nizeeke labda miaka 60 ndio niokoke...... Je nikifanikiwa kutoboa hadi 60yrs halafu ndio nikaokoka nikifa nakwenda Peponi?
😁Naona unataka uingie heaven kwa kuangushia
 
Loo, wanacheka, wanarukaruka, wanacheza wakifurahia uzinzi, ulevi, ulaghai, wizi, na anasa za dunia. Wanadhani maisha hayo hayana tatizo. Lakini Biblia iko wazi kabisa: maisha ya dhambi yana mwisho mbaya mno. Ni mateso ya milele na milele. Tafadhali, fuatana nami leo tuitafakari habari ya tajiri na Lazaro iliyoandikwa katika Luka 16:19–31, pamoja na maandiko mengine, tuone kwa undani mateso yanayowasubiri wanaoendelea kufurahia dhambi na kukataa kuokoka:

1. Watu hao wakifa tu, wanaingia moja kwa moja mahali penye mateso. Biblia inasema tajiri aliyekuwa akifurahia maisha ya anasa alikufa na mara moja akaingia katika mateso:
ā€œYule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso...akaliaā€ (Luka 16:22–23)

Hii ni tahadhari kwa wale wanaoishi katika dhambi: kifo sio mwisho wa maisha, ni mwanzo wa mateso ya milele kwa wasiotubu.

2. Wanateseka katika moto mkali usiozimika. Tajiri aliyezoea starehe, alijikuta akililia tone la maji kwa sababu ya mateso:
ā€œAkalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.ā€ (Luka 16:24)

Wale wanaoishi maisha ya ulevi, uasherati na dhambi nyingine hawatapata tena faraja wala kicheko, bali mateso makali yasiyo na mwisho:
ā€œNao watatupwa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.ā€ (Mathayo 13:42)

3. Wanajuta sana, lakini majuto ya marehemu hayana faida. Tajiri alitamani ndugu zake waambiwe ili wasiende mahali alipo kwenye mateso, lakini alikuwa amechelewa:
ā€œBasi, nakuomba, baba, umtume Lazaro... awashuhudie.ā€ (Luka 16:27–28)

Majuto hayo yatawapata wote wanaodharau habari njema za Yesu Kristo. Ni heri ujute sasa na kuacha dhambi zako kuliko kujuta milele bila msaada.

4. Watahukumiwa na kisha kutupwa katika ziwa la moto. Kuzimu ni hatua ya kwanza tu. Baada ya hukumu kuu ya mwisho, watenda dhambi wote watatupwa kwenye ziwa la moto la milele:
ā€œNa iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.ā€ (Ufunuo 20:15)

Hii ndiyo hatima ya mwisho ya wale wanaoendelea kufurahia dhambi bila kutubu. Jehanam ni mahali penye maumivu, upweke, huzuni, hofu, na mateso ndani ya moto usiozimika, milele na milele.

Ndugu yangu usipoteze bure fursa ya kuingia mbinguni. Kama tulivyoona, wenye dhambi wanapokufa bila kutubu, hawana tena nafasi ya kubadilisha hatima yao. Tajiri alimwona Lazaro akiwa kifuani mwa Ibrahimu, lakini hakuweza kufika huko (Luka 16:26).

Furaha ya dhambi ni ya muda mfupi, lakini athari yake ni ya milele. Mtu akiikataa neema sasa, ataukosa uzima wa milele baadaye.

Bado nafasi ipo. Leo ni siku yako mwafaka ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu, na kumpokea Yesu awe Bwana wa maisha yako. Usingoje hadi uwe mfu ndio ujue uzinzi na ulevi vilikuwa mtego wa ibilisi.

Naamini umenielewa na utafanya uamuzi wa kuokoka sasa hivi. Kumbuka, hakuna aijuaye siku ya kuondoka duniani. Kwa sababu hiyo, usiupuuze ujumbe huu, vinginevyo ukifa kabla hujatubu na kuokoka, utaingia kwenye mateso hayo ya milele.
ā€œTazama, sasa ni wakati uliokubalika; tazama, sasa ni siku ya wokovu.ā€
(2 Wakorintho 6:2)

cc: Binti wa zamani Mallerina Lamomy I feel good leo dada
Asante kutujuza
 
Na wavaao mavazi yasiyostahili.... Wakike kuvaa kikahaba... Wakiume kuvaa kihuni na kunyoa kiajabuajabu/hovyo
Mkuu ina maana wanyoa viduku wote watachomwa moto. Vipi kwa wazee wa kobazi wenye wake wanne huo sio uzinzi kweli nao watachomwa moto?

Vipi kwa wa Asia wengi wasio amini kwenye ukristo/uislam nao moto unawahusu? Au kutakua na exceptions
 
What a sadist! Wewe ndiyo unateseka kuandika nyuzi ndefu kusambaza hofu yako uliyoketewa na wazungu kwa waafrika wenzio.
Wote tutakufa na hakuna cha ziada kitafanyika zaidi ya decomposition tu.
Huo moto, labda uwe cremated!
 
20250802_065339.jpg

Uko sahihi madam.
 
Wewe mama mchungaji taratibu kwanza, kwani kuna kiumbe hakizini hapa duniani?
Au nyie mlio kwenye ndoa ndo mnataka peke yenu mlombwe? 😹😹😹

*Kuzini ni kuzini, hata mama yake Yesu alipatikana kwa midinyano. āœ…

*Kulewa ntalewa sana Yesu mwenyewe aliwalewesha watu kwenye harusi kwa mvinyo uliochachuka. āœ…

Hiyo mbingu haipo usitutishe, wewe uliiona? Ulifika ukaikuta?
Eti hataki tulombane babe😁
 
Mkuu ina maana wanyoa viduku wote watachomwa moto. Vipi kwa wazee wa kobazi wenye wake wanne huo sio uzinzi kweli nao watachomwa moto?

Vipi kwa wa Asia wengi wasio amini kwenye ukristo/uislam nao moto unawahusu? Au kutakua na exceptions
ukijua yakupasayo kutenda ili kuikamilisha haki na usitende, hukumu inakuhusu...
 
Loo, wanacheka, wanarukaruka, wanacheza wakifurahia uzinzi, ulevi, ulaghai, wizi, na anasa za dunia. Wanadhani maisha hayo hayana tatizo. Lakini Biblia iko wazi kabisa: maisha ya dhambi yana mwisho mbaya mno. Ni mateso ya milele na milele. Tafadhali, fuatana nami leo tuitafakari habari ya tajiri na Lazaro iliyoandikwa katika Luka 16:19–31, pamoja na maandiko mengine, tuone kwa undani mateso yanayowasubiri wanaoendelea kufurahia dhambi na kukataa kuokoka:

1. Watu hao wakifa tu, wanaingia moja kwa moja mahali penye mateso. Biblia inasema tajiri aliyekuwa akifurahia maisha ya anasa alikufa na mara moja akaingia katika mateso:
ā€œYule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso...akaliaā€ (Luka 16:22–23)

Hii ni tahadhari kwa wale wanaoishi katika dhambi: kifo sio mwisho wa maisha, ni mwanzo wa mateso ya milele kwa wasiotubu.

2. Wanateseka katika moto mkali usiozimika. Tajiri aliyezoea starehe, alijikuta akililia tone la maji kwa sababu ya mateso:
ā€œAkalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.ā€ (Luka 16:24)

Wale wanaoishi maisha ya ulevi, uasherati na dhambi nyingine hawatapata tena faraja wala kicheko, bali mateso makali yasiyo na mwisho:
ā€œNao watatupwa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.ā€ (Mathayo 13:42)

3. Wanajuta sana, lakini majuto ya marehemu hayana faida. Tajiri alitamani ndugu zake waambiwe ili wasiende mahali alipo kwenye mateso, lakini alikuwa amechelewa:
ā€œBasi, nakuomba, baba, umtume Lazaro... awashuhudie.ā€ (Luka 16:27–28)

Majuto hayo yatawapata wote wanaodharau habari njema za Yesu Kristo. Ni heri ujute sasa na kuacha dhambi zako kuliko kujuta milele bila msaada.

4. Watahukumiwa na kisha kutupwa katika ziwa la moto. Kuzimu ni hatua ya kwanza tu. Baada ya hukumu kuu ya mwisho, watenda dhambi wote watatupwa kwenye ziwa la moto la milele:
ā€œNa iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.ā€ (Ufunuo 20:15)

Hii ndiyo hatima ya mwisho ya wale wanaoendelea kufurahia dhambi bila kutubu. Jehanam ni mahali penye maumivu, upweke, huzuni, hofu, na mateso ndani ya moto usiozimika, milele na milele.

Ndugu yangu usipoteze bure fursa ya kuingia mbinguni. Kama tulivyoona, wenye dhambi wanapokufa bila kutubu, hawana tena nafasi ya kubadilisha hatima yao. Tajiri alimwona Lazaro akiwa kifuani mwa Ibrahimu, lakini hakuweza kufika huko (Luka 16:26).

Furaha ya dhambi ni ya muda mfupi, lakini athari yake ni ya milele. Mtu akiikataa neema sasa, ataukosa uzima wa milele baadaye.

Bado nafasi ipo. Leo ni siku yako mwafaka ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu, na kumpokea Yesu awe Bwana wa maisha yako. Usingoje hadi uwe mfu ndio ujue uzinzi na ulevi vilikuwa mtego wa ibilisi.

Naamini umenielewa na utafanya uamuzi wa kuokoka sasa hivi. Kumbuka, hakuna aijuaye siku ya kuondoka duniani. Kwa sababu hiyo, usiupuuze ujumbe huu, vinginevyo ukifa kabla hujatubu na kuokoka, utaingia kwenye mateso hayo ya milele.
ā€œTazama, sasa ni wakati uliokubalika; tazama, sasa ni siku ya wokovu.ā€
(2 Wakorintho 6:2)

cc: Binti wa zamani Mallerina Lamomy I feel good leo dada
Hicho ni kivuri Cha mambo yajayo na moto hakuna
 
Back
Top Bottom