Hivi ni Demokrasia gani inayopiganiwa na vyama vya Upinzani? Sioni Chama cha kukipa Nchi

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
CCM ni Chama ambacho kina misingi na utaratibu wa namna kinavyojiendesha ndio maana utaona viongozi wanaachiana madaraka kwa taratibu hizo.

Utasikia mtu kapita kwa asilimia 100, bila kupingwa etc.. ni taaratibu zao na Wanachama wao wanazipenda.

Huku kwetu upinzani Mtu akishaanzisha Chama au Kuwa kiongozi basi yeye atakuwa kila kitu .hakuna maamuzi ya maana yatafanyika bila yeye kuwepo.

Kuna wenyeviti wana zaidi ya miaka Ishirini madarakani na bado wanaendelea kuongoza Chama ,Swali mtu kama huyu akipewa Nchi atakubali toka Madarakani?

Kuna Chama mtu kajitafutia cheo anaitwa Kiongozi Mkuu yote hiyo vyeo vingine vinavyobadilika yeye asiguswe ,swali je hawa watu ni wazalendo au anaangalia Maslahi yake tu?

Kuna vyama Nenda rudi mgombea nafasi ya Urais ni huyo kiongozi wa Chama kana kwamba hakuna mtu mwingine wa kuweza simama.

Hivi ni demokrasia ipi iko Upinzani ? Mbona miundo yao ya uongozi na mbadilishano wa madaraka haueleweki na hauwi wazi?

Mimi ni mpinzani ila naona ni bora CCM iendelee kuwepo Madarakani mbali na kwamba imetufanya Maskini wa kutupwa kwa kila siku kutujazia Mafisadi na Kukosa Maono kwa Taifa kuliko sisi Wapinzani tunao hubiri kitu ambacho hakipo kwenye vyama vyetu.
 

Hivi ni Demokrasia gani inayopiganiwa na vyama vya Upinzani? Sioni Chama cha kukipa Nchi​

Kwani wewe ndo unaamua umpe nani nafasi ya kuongoza nchi au ni umma wa Watanzania kupitia sanduku la kura?!

MATAGA mnateseka sana, na bado!

Subiri Tume Huru ya Uchaguzi iwepo ndo utajua hujui
 

Huoni chama Cha kukipa madaraka kutoka Upinzani, wakati serikali na ccm inakopa na kununua Viongozi kutoka Upinzani?. Leo Kuna wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi walichukuliwa kutoka Upinzani hasa chadema. Pia Kuna manaibu waziri walitoka Upinzani.

Unasema hivyo kisa Ni chama kimoja tu kimetawala nchi ndio maana.
 
ukomavu wa CCM ndiyo ule mnaoufanya NCCR Mageuzi siyo !!
 
Kwa akili matege yako matege unadhani ccm nao wanauwezo wa kuongoza Nchi au wanaibemenda Nchi[emoji849]
 
Mkuu kama kiongozi unanunulika basi Hufai kuwa kiongozi
 

Jifunze na usikariri. Wewe unadhani chama ndio kila kitu, watu wa kuongoza ndio wamuhimu.Hapo tu Kenya tangu Uhuru vimetawala vyama vinne tofauti na wapo mbali kiuchumi na kisiasa kutuzidi.

KANU, NARC, PNU na Sasa Jubillee Party. Na Kuna uwezekano mwaka huu ukaingia Mrengo mpya wa aidha Kenya kwanza ya UDA au Azimio ya ODM na Jubillee. Kenya walishaacha kuabudu chama kimoja Kama sisi Tanzania ambako tunadhani Bila CCM hatuwezi ishi, tunaibudu CCM hata inapoonesha imeshindwa kutawala.
 
Huna akili
 
Chama cha kukipa nchiโ€ฆ. nchi sio 'ndogo' yako unayoweza kupeana.
 
Umeshiba maharage ya wapi mleta mada?
 
Mjinga mkubwa kwani demokrasia maana yake chama cha upinzani kupewa nchi?
 
Ya ni kweli, si unaona hata watu ambao wangefika kwenye mikutano ya wapinzani walinunuliwa ili wasifike mikutanoni ktk uchaguzi mkuu. Kuwa chawa wa mwanaume mwenzio kwa kweli ni hasara kwa familia. Uzuri wa chawa, hautakiwi kuona aibu hata pale unapohitajika kuona aibu kwa uongo unaouandika.
 

Attachments

  • images (7).jpeg
    60 KB · Views: 9
  • images (19) (1).jpeg
    34.1 KB · Views: 11
  • IMG-20220407-WA0040.jpg
    52.5 KB · Views: 10
  • images (10).jpeg
    72.2 KB · Views: 9
  • images (9).jpeg
    45.7 KB · Views: 10
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Wewe au kilaza mwingine hatakiwi kuamua chama cha kukipa nchi, wananchi wengi kupitia tume huru ya uchaguzi ndio wanapaswa waamue chama gani kiongeze nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ