Hivi ni kwanini Baraza Kuu la CCM liliwaita na kutaka kuwahoji akina Membe na kumwacha Musiba?

ukweli unabaki kuwa kila mtu ni ccm .. mnaijua mnaipenda na mnataka itende haki ama ifuate utaratibu fulani.

Get out of closet..[emoji1][emoji1][emoji1]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natumia Uhuru wa kutoa maoni yangu kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) inavyosema, nikiiinukuu " Kila mtu yuko huru kutoa nje maoni yake na kutafuta na kupokea habari zozote kupitia chochote cha habari bila kujali mipaka ya nchi na pia Uhuru huo wa mawasiliano kutotakiwa kuingiliwa kati na chombo chochote kile" mwisho wa kunukuu
 
unatumia katiba ya serikali kuongelea chama ccm? Haviingiliani boss.. Uhuru hauingilii taasisi zisizokuhusu..

umechanganya ama umechanganyikiwa?
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
unatumia katiba ya serikali kuongelea chama ccm? Haviingiliani boss.. Uhuru hauingilii taasisi zisizokuhusu..

umechanganya ama umechanganyikiwa?
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
Kutumia Katiba ya nchi kuhoji mambo ya yanavyoenda kwenye tahsisi binafsi ni sahihi kabisa

Kwa kuwa Katiba ya nchi ndiyo iko juu ya kila kitu hapa nchini
 
Hakuna chama hapo.

Yaani hii ni bunch la ma mazfrakars..

Musiba anatumwa na Magu.
Na wale CCM wameshajua kwa hio wanacheza ngoma ya Magu ili kumfurahisha kulinda vyeo vyao
 
Mkuu hutapata majibu sahihi ya maswali yako. Ukweli uko wazi kuwa anaeshikilia chama ndiye anaeamua ni nani ahojiwe ni nani ashitakiwe na kwa makosa yepi na amekwenda mbali zaidi hata kuwa Hakimu ktk maamuzi mbalimbali Mahakamani na hata ndani ya ule Mhimili unaotunga na kusimamia Sheria. Musiba ni speaker tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM haiogopi watu kama chadema ,huku ukizingua unasurubiwa kama yeyete

State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona kila kwenye matatizo yenu lazima muitaje Chadema? Wewe hata mumeo akishindwa kukupachika mimba utasingizia Chadema, nani kawaroga nyie? Au moja wapo ya masharti ya kulipwa buku7 ni kuitaja Chadema na Mbowe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi ni lazima iongozwe kwa kufuata sheria

Hatuwezi kama nchi kuongozwa kwa kufuata utashi wa mtu binafsi
 
Hivi wakiwa huko ndani, wanawahoji au ni mazungumzo ya maridhiano?
 
Hakuna chama hapo.

Yaani hii ni bunch la ma mazfrakars..

Musiba anatumwa na Magu.
Na wale CCM wameshajua kwa hio wanacheza ngoma ya Magu ili kumfurahisha kulinda vyeo vyao
Ni hatari mno nchi kuendeshwa kihuni kiasi hiki
 
Naomba nijibiwe kwa hoja, wala si kwa kutoa povu
Kosa kuu la akina kinana ni kumdhihaki na kumdhalilisha mwenyekiti,hakuna sehemu ambayo Musiba amemdhihaki mwenyekiti
Kwa mujibu wa katiba yetu ya ccm,makosa hayo yanajadiliwa na kamati ya madili na nidhamu,na ili haki ionekane imetendeka,ndio maana wameitwa
Nikukumbushe hata kwenu chadema mliwaita kubenea na komu na mkawahukumu kwa kumdhalilisha mwenyekiti wenu na hukufungua thread
 
Wamemdhihaki kivipi Rais??

Hivi hamjasikia namna Rais anavyowadhihaki na kuwadhalilisha hata kuwatukana, wapinzani kwenye hotuba zake za kisiasa??

Kwanini sheria ikate upande mmoja, wakati tunaambiwa kuwa sheria ni kama msumeno unakata huku na kule??

Je hujawahi pia sikia kuwa sheria haina macho, kwa hiyo haiangalii ni nani anahusika, awe mkubwa au mdogo yenyewe inabidi itoe hukumu
 
Kwani Musiba amekuwa kigogo wa CCM?na je aitwe na CCM kwa kosa gani na akiwa kama nani?
 
4. Hivi kwa kitendo kilichofanywa na baraza la CCM, siyo kinazidi kuthibitisha shutuma za wananchi walio wengi kuwa huyo Musiba anakingiwa kifua na anatumwa na mtu mzito sana ndani ya nchi hii kutoa hizo shutuma zake zisizokuwa na ushahidi?

Naomba nijibiwe kwa hoja, wala si kwa kutoa povu
[/QUOTE]
Bold = Huu ndio ukweli, ila tunaamini Uovu utashindwa dhidi ya ukweli. Best wishes Membe.
 
Hivi hamjasikia namna Rais anavyowadhihaki na kuwadhalilisha hata kuwatukana, wapinzani kwenye hotuba zake za kisiasa??
We una matatizo
Rais kuwadhihaki wapinzani hakuhalalishi wanachama wa ccm wamdhihaki mwenyekiti wetu
Kwan hata nyie si mnamwita jiwe,dikteta,
 
Musiba na wenzie ndiyo hit squad ya CCM wanatumwa kama majini. Ngoja tukutane na Jasusi mbobezi Bernard tusikie bombani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…