Hivi ni kwanini meli ikitembea maji yanamwagika?

Hivi ni kwanini meli ikitembea maji yanamwagika?

radika

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2014
Posts
20,440
Reaction score
32,260
Wataalam wa Meli nisaidieni kujua meli ikitembea huwa inamwaga maji na yanapitia wapi?

Kwa juujuu unawezasema nii kweli maji ya bahari hutumika kupoza engine ya meli. Lakini kiundani ni hapana, ila maji ya bahari hutumika kupooza 'coolant' ambayo ndiyo hutumika kupoza engine ya meli. Maji ya bahari ni corrosive sana. Yakitumika kuzunguka kwenye parts za engine ili kupooza, engine itachoka baada ya muda mfupi sana. Hata kwenye engine zetu za kawaida (majenerator, magari, nk) maji yanayopoza engine hupozwa na feni kupitia rejeta. Kwenye meli hutumia 'heat exchanger'. Kifaa ambacho kina mirija ya kupitisha maji ya kupooza engine, na pia mirija mingine ya kupitisha maji ya bahari. Kitendo hicho hufanya maji ya kupooza engine yabadilishane jotoridi na maji ya bahari. Hivyo maji ya kupooza engine yakitoka kwenye 'heat exchanger' yanakuwa yamepoa na yanarudi tena kwenye mzunguko wa kupooza engine. Na maji ya bahari nayo yanakuwa yamepata joto yanarudi baharini na mzunguko unaendelea. Hivyo ndiyokusema....maji ya bahari hayapoozi engine bali hupoza 'coolant' inayotumika kupooza engine. Hebu jaribu kuangalia mchoro huo hapo chini kama unaweza pata picha zaidi.
View attachment 277544

  • 1. Valve
  • 2. Pump ya kunyonya maji ya bahari
  • 3. Filter
  • 4. Heat exchanger yenyewe (kuna HE za aina nyingi sana)
  • 5. Engine IC
  • 6. Clutch
  • 7. Outlet pipe ya kumwaga maji baharini

Pia jaribu kuangalia mchoro huo hapo chini. Ni mchoro tata kidogo, lakini unaweza ukakupa picha zaidi.
View attachment 277545


Hehehehee! Nimefurahishwa na michango ya wengi wenu hapo juu. Ni kweli meli nyingi saana huwa zinatoa maji hasa the moment zinapong'oa nanga na kuanza safari. Nitaanzia mbali kidogo. Niliwahi kujiuliza inakuaje zile meli ya kivita, Nyambizi (submarine) zinaweza kuzama baharini na kurudi kwenye surface water. Ndio katika kuchimbua nikakutana na kitu kinaitwa "ballast tanks". Nyambizi ina matangi makubwa saana ya maji ambayo yana mechanism ya kujaa maji pale inapohitaji kuzama baharini, na pale inapohitaji kurudi kwenye surface water, yale matangi yanatoa maji na kuingiza hewa. Wengi wenu mkikumbuka kwenye physics tulifundishwa kuwa hewa ina density dongo kuliko maji, ndio maana air bubbles hazikai ndani ya maji, zinakuja kwenye surface, so nyumbizi ikifungulia maji, inarudi kwenye surface kwa same mechanism as air bubbles.

Now lets get back to our topic. Meli pia zina hayo matangi makubwa, either upande wa pembeni, au upande wa chini. Lengo kubwa la hayo matangi ni kuongeza uzito wa meli ili ku improve stability inapokua majini. Kumbuka chombo kinachoelea huwa kinakua chepesi saana kiasi kwamba hata upepo tu unaweza kukipeperusha. Hivyo kuna level ya ujazo au uzito unaokuwa recommended kuwa maintained na kila meli ili kuimprove stability. Kwa madereva mtanielewa vizuri, ukiendesha gari nzito kama Mercedes S class na Carina Ti kuna tofauti kubwa saana katika stability, gari nzito iko stable saana as uzito unasaidia kuimprove the center of gravity, hivyo gari inakua chini na inabalance vizuri. (Wengine huwa tunajaza mizigo au kubeba watu ili gari iwe na balance, wengine tunaweka spoilers)

Meli pia zinahitaji that same mechanism kuimprove stability. Vile mara nyingi meli huwa zinabeba mzigo mzito, mara nyingi inakuwa nzito saana, lakini utakumbuka kuwa hiyo mizigo huwa inapungua au kuongezeka pindi meli inapofika kituo fulani, so density ya meli inapungua na kuongezeka pia. Vile vile sehemu kama unavyofahamu, sehemu mbali mbali za bahari zina concentration tofauti ya chumvi, hivyo hata density ya maji inapishana pia. So ili kuhakikisha meli iko stable kwenye kila condition kunakua na constant trade off kati ya mizigo, maji na hewa ili kuendelea ku maintain uzito unaohitajika kupata stability. Meli ikiwa haina mzigo, inajaza maji mengi kwenye matangi yake ili iwe nzito na iwe stable baharini, lakini pindi mzigo unapoongezeka, inabidi yale maji yaondolewe kwenye matangi, ili uzito usidi kipimo cha ujazo as indicated by the Plimsoll line ndio maana ukiwa bandarini au meli ikianza kuondoka utaona maji mengi yakiondolewa maana inakua imepakia mzigo. Lakini ikishusha huo mzigo, maji yanaongezwa tena kwenye meli. So it is a constant process, either kuongeza maji au kupunguza as long as uzito fulani unakua maintained.

I hope umepata mwangaza kidogo kwenye hilo swali lako.

View attachment 277663View attachment 277664
View attachment 277665
 
Nadhani anaongelea yale matundu ya pembeni but si kila meli huwa in hayo matundu..
 
ages.jpgimes.jpg
index.jpg

Jamani!!....bado tu hamjamuelewa!!!. Au hamtaki kumjibiu??
 
Ni maji yanayopoza mashine huwa yanavutwa kutoka baharini na kurudi humo
 
Engine ya meli kubwa inapoozwa kwa water fins surrounding the Engine na hivyo maji ya Chumvi ya baharini yanatumika kupooza kwa kuvuta...kuyazungusha kwenye water guides including oil coolers na yakipata moto yanarudishwa baharini.

Engine za meli hazijatengenezwa na cooling system (radiator kama magari au earth moving machines au generators nope!)
 
Back
Top Bottom