Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,491
Kwa juujuu unawezasema nii kweli maji ya bahari hutumika kupoza engine ya meli. Lakini kiundani ni hapana, ila maji ya bahari hutumika kupooza 'coolant' ambayo ndiyo hutumika kupoza engine ya meli. Maji ya bahari ni corrosive sana. Yakitumika kuzunguka kwenye parts za engine ili kupooza, engine itachoka baada ya muda mfupi sana. Hata kwenye engine zetu za kawaida (majenerator, magari, nk) maji yanayopoza engine hupozwa na feni kupitia rejeta. Kwenye meli hutumia 'heat exchanger'. Kifaa ambacho kina mirija ya kupitisha maji ya kupooza engine, na pia mirija mingine ya kupitisha maji ya bahari. Kitendo hicho hufanya maji ya kupooza engine yabadilishane jotoridi na maji ya bahari. Hivyo maji ya kupooza engine yakitoka kwenye 'heat exchanger' yanakuwa yamepoa na yanarudi tena kwenye mzunguko wa kupooza engine. Na maji ya bahari nayo yanakuwa yamepata joto yanarudi baharini na mzunguko unaendelea. Hivyo ndiyokusema....maji ya bahari hayapoozi engine bali hupoza 'coolant' inayotumika kupooza engine. Hebu jaribu kuangalia mchoro huo hapo chini kama unaweza pata picha zaidi.Engine ya meli kubwa inapoozwa kwa water fins surrounding the Engine na hivyo maji ya Chumvi ya baharini yanatumika kupooza kwa kuvuta...kuyazungusha kwenye water guides including oil coolers na yakipata moto yanarudishwa baharini.
Engine za meli hazijatengenezwa na cooling system (radiator kama magari au earth moving machines au generators nope!)

- 1. Valve
- 2. Pump ya kunyonya maji ya bahari
- 3. Filter
- 4. Heat exchanger yenyewe (kuna HE za aina nyingi sana)
- 5. Engine IC
- 6. Clutch
- 7. Outlet pipe ya kumwaga maji baharini
Pia jaribu kuangalia mchoro huo hapo chini. Ni mchoro tata kidogo, lakini unaweza ukakupa picha zaidi.



