Wadau nimeusoma huu uzi kuanzia mwanzo hadi mwisho lkn hakuna aliyetoa jibu la kweli humu ndani. Swali linasema kwa nini meli ikitembea inatoa maji nje? Jibu! Kwanza sio tu meli ikiwa inatembea ndio inamwaga au inatoa maji nje no hata ikiwa haitembei bado itakuwa inatoa maji nje.kwa nini kwa sababu chini ya meli kuna propela zipo kama feni vile, ikiwashwa engine ndio zile propela zinazunguka meli au boti inatembea sasa pale kwenye zile propela kunakuwa na uwazi unaopitisha maji kuingia ndani na maji yale yakiingia ndani lazima yatolewe kwa sababu yakijaa bila kutolewa yatasababisha meli kuzama ndio maaana kuna mashine maalumu za kuyatolea nje yale maji ndio hapo unapoyaona yanatoka nje.na zile mashine zinajitegemea zenyewe hazitegemei lufanya kazi hadi engine ya meli iwe on na ndio maana hata meli ikiwa imesimama bado zile mashine zinatumika kutoa maji nje na ikitokea siku mashine ya kutolea maji nje zimezima linaweza tokea balaa ila wanakuwa nazo nyingi inategemea na ukubwa wa chombo.hata ukiwaangalia wale wavuvi wanaotumia mitumbwi coz hata mtumbwi pia unaingiza maji ndani yanapitia pale kwebye viungio bc wale utawakuta na makopo ya kutolea maji nje ili chombo kisizame.na hata wale wanaopanda vimtumbwi vya kubebea abiria bc utawaona manahodha na makopo yao wanatoa maji nje na kama unepewa lifti basi utapewa kazi ya kutoa maji nje.Hilo ndio jibu sahihi kabisa sio hayo yaliopita huko juu.
Mkuu majibu yameshatolewa na hili lakwako naona ni kama unatuingiza chaka, fuatilia page za mwanzo kuna majibu yenye mashiko yametolewa.

