Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

Siku hizi unakuta kijana kavaa Suruali chini ya Makalio,sasa hapa atapigana vipi? Si itaanguka! Watoto wa siku hizi ni ubishoo na vimatusi kwenye social media tu,Kijana kapaka poda,cream ya kulainisha ngozi na hereni sikioni,saa ngapi atawaza kupigana? Afya zenyewe siku hizi ni mchoko tu,unaweza kukuta mtu anatembea kumbe kisha jifia zamani! Ukigusa tu unakua umenunua kesi ya mauwaji!

Halafu zamani eti ukipigana lazima uvue shati ili lisije kuchanika na Mama akajua home kua umepigana,

Where are those gold days aiseee?!

 
Hatari sana....
 
Ha ha haaa umeanza mkwara wa keyboard?

Hahaha! Nilimsikia Mitemba anamwambia mzee Jongo kwenye mchezo wa radio. Jongo bwana alimwambia Mitemba kwamba kama sio uchovu wa safari aliokuwa nao wangeshikana mashati (Kosema kama sio kuchoka safari, nakwambia hapa ngumi zingewaka moto ndii). Mitemba akamwambia Jongo nakupa wiki moja kapumzike uchovu wa safari yako, ule na mayai kabisa, halafu njoo hapa nikuonyeshe kazi! Nilicheka sikuwa na mbavu!
 
 
The world is driven by brains. We piga pushup komaza ngumi, bonge mimi na Beretta mkononi can squash your brains 50 feet away. Without moving an inch.

Hata vita sikuhizi zinapigwa through presses of buttons.
 
kupigana zamani ilikuwa order of the day .....sasa hao machoko wangetoka wapi??? hata wale waliokuwa na nguvu waliunda UMOJA wa kusaidiana kama watoto wa mbwa mwitu ....ukimpiga mmoja wanakuja wote kuchangia ....hadi na viwembe
 
siku hz mbabe ni mwenye PESA ndo maana watu wapo bize kusaka PESA....
 
Watu wengi wamemrudia MUNGU aliyewaumba ndio maana kupigana kumefifia.
 
Enzi hizo mbabe wa kijiji/mtaa anajulikana kabisa, na watu walikuwa na maeneo ya kupogia matizi ya ngumi, ukipigwa sio rahisi kwenda kushitaki mambo yanaisha kibabe tu, ni mkono kwa kwenda mbele
 
Dah zama hizo nipo Dar, mgulani primary, kuna akina Wamensa (Shimo la udogo), Juma (Keko machungwa), Selemani (Keko mwanga) acha wale wa Temeke na Kurasini! hapo enzi za matumizi ya CHENI ile ya Bruce Lee!Zama hizi watu hawashibi, huko kupigana utaanzaje kufikiria?
 
Nilikua nikikupiga ngumi utahisi ni ndoo ya zege imekudondokea.........acha kabisa

Hahahaha. Kumbe wewe mtu hatari sana......hata Muhamad Ali hakuwa na ngumi nzito kiasi hicho!
Nilikuwa nakuona mpoleee, ila sasa nikikuona nabadili njia...!
 
Kumbuka ukiwa mdogo rika yako ni ya wale vijana wagomvi hata hivyo bado kupigana kupo ila wewe tu ndio umekuwa mkubwa na unapigana na maisha ambapo wadogo zako wanapigana bado
 
Hahahahaha umenifanya nicheke,
Ahsante.
 
Heeeeh!
Vituko, mtu kawa fimbo,
Hahahaha itakua unasema movies za bruce lee.
 
Dah umenikumbusha Mfike Mapugilo (Fike kwa sasa) alikuwa mtemi wa soko matola Mbeya, sijui yupo wapi huyu jamaa. Ilikuwa burudani tosha
 
Hahahaha. Kumbe wewe mtu hatari sana......hata Muhamad Ali hakuwa na ngumi nzito kiasi hicho!
Nilikuwa nakuona mpoleee, ila sasa nikikuona nabadili njia...!

Napiga jamani........shetani anaogopa.........
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…