Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hunijui vema, siko humu jukwaani kubishana. Natoa mchango. wangu tu, si lazima ukufurahishe na hiyo ndiyo democracy.. JF where we dare talk openly and I am doing just that!!
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] Mkuu umetisha
 
Ni haki yangu maana linanihusu na Uhuru wakujiamulia kufanya jambo linalonipa furaha sio kubanwa na MTU yoyote yule kunipangia na mindset zake.
Hili sasa ndio tatizo ndio maana mnalia lia,inaonekana hujui hata haki yako ni ipi na lipi si haki yako.

Nakufundisha sasa sio kila jambo linalokupa wewe furaha ni haki yako au linakuhusu,huu sio uhuru bali ni utumwa wa matamanio ya nafsi,inatakiwa muwe mnajifunza mjue lipi lenu na lipi si lenu na kwanini.

Nimekupima kwa swali rahisi sana lakini umeshindwa kujibu,nimekuuliza unajuaje kama lipi lako na lipi sio lako. Furaha sio kipimo cha wewe kujua hilo linalo kufurahisha ni lako,nakupa mfano wapo ambao wanafurahia na kufurahishwa na uzinzi,ufisadi,dhulma,wizi,unyang'anyi,kusema uongo,umbea,unafiki,uzandiki,kusengenya na mfano wa hayo,je ni kweli hayo mambo anatakiwa mtu kuyafanya hata kama yanamfurahisha ? Sasa bibie unatakiwa utoke katika utumwa ulio nao,utumwa ambao unakufanya ufikirie mambo kitoto na kwa upande mmoja,na uhuru bila mipaka ni utumwa na kutumia akili vibaya.
Nchi lazima ifate haki za raia za wananchi wake Kwa kutoa usawa Kwa kila jambo Kwa watu wake
Mimi nimeamua kukufundisha sasa,baada ya kuona hujui kitu juu ya hicho unacho kidai,hakuna haki isiyo zingatia maumbile na silika.

Nakuuliza swali,je huanza haki au huanza nchi ? Kama huanza haki kisha haki zinasimamiwa ni wazi kabisa nchi imezikuta haki na nchi haina uwezo wa kuijua haki mpaka haki iwepo,unakubaliana na hilo ?

Lakini,kauli yako bado inaonyesha ya kuwa haki ndio ilianza na serikali inasimamia haki,sasa swali la msingi liko pale pale,je unajuaje kwamba hii ni haki yako na hii si haki kisha ndio serikali ije kuisimamia ?
Dini ambayo ni muongozo wa wanadamu imemkandamiza mwanamke hasa dini flani siitaji.

Najua unaashiria dini gani,naweza kukupa hata miaka elfu uonyeshe wapi imemkandamiza mwanamke kisha ujibu kila swali nitakalo kuuliza,najua hutaweza kujibu hata swali moja,sababu hata misingi ya haki na haki yenyewe huijui.

Unaiweza kuniambia hiyo dini imemkandamiza wapi mwanamke na wewe umejuaje hilo na marejeo yako ni yapi na kwanini hayo marejeo yako tuyafate ?
Ndio mana nili prefer mada huru bila kuingiza hizi dini maana hazi encourage watu kufikiria nje ya chupa
Naendelea kukufundisha bibie,hakuna mtu ambae anafikiria kwa uhalisia kuliko mtu mwenye dini,sababu mtu wa dini anakuwa na yote ya dunia na akhera,na anafikiria pale ambapo akili ilipokomea.

Nilikuuliza juu a kufikiria nje ya box,na ulitoa maana nzuri sana,ambayo kwa maelezo yako inaakisi ya kuwa kwanza uko kinyume na maana ile bali hujaielewa na huifanyii kazi pia. Katika maana yako ulizungumzia kuhusu faida na hasara au kama ulivyoandika,lakini ajabu kiutendaji na maandishi yako hayaonyeshi kama unazingatia faida na hasara katika kulitaka jambo.

Nipo ...
 
Mkuu umemaliza ...
 
Hamtaki kutuletea, huoni wenzio wakileta matangazo ya kutafuta wake utasikia "awe na kipato" au awe na kazi ya kumuingizia pesa, means hawataki kutuletea.... Kuna mmoja jana humu amesema wanawake tutafute pesa zetu
Bibie,weka akilini hili,kwenye Wanaume kuna Wanaume.

Mwanaume kamili huyu wa pili,hawezi kumwambia Mwanamke alete hela nyumbani,kwanza anatoka katika maumbile na ni aibu kwetu sisi na hivyo ndivyo nilivyo mimi.
 
Sasa hutakiwi uandike unacho kiamini,uantakiwa uandike ukweli,kwenye kuanimi kuna imani potofu ambayo ya uongo pia.

Embu kaa utulie kisha uandike ukweli.
Ninandika chenye ukweli na uhalisia wa mambo Kwa mazingira ninayoishi. Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko kabisa aisee, why kuoneana wengine why why???
 
Endelea kujifariji
 
Ninandika chenye ukweli na uhalisia wa mambo Kwa mazingira ninayoishi. Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko kabisa aisee, why kuoneana wengine why why???
Bibie naona umetoka kwenye imani umehamia kwenye ukweli,ukweli hakika hauko nao bali hamko nao katika hili.

Hapa naweza kukuuliza nini maana ya UKWELI ukashindwa kunijibu,ajabu unadai kuwa una andika ukweli.

Niko pale pale,nakupa kazi sio lazima unipe jibu leo wala kesho,nenda kawaulize wakubwa zako katika hizo fikra za kivivu,kwamba huwa wanajuaje kwamba hii ni haki ya mtu na hii si haki yake ?

Wakikujibu nistue.
 
Sasa ujasiriamali wa kuuza juice, kupost viatu mitandaoni, kwa hela za kudanga ndo mnajiita wajasiriamali... Mnapoteza muda
 
Haya madini uliyoyatema bure bila ata ya ku charge pesa hayaitwi POINT bali yanaitwa "PURE FACT and FREE EDUCATION".
 
Mbona Mimi nakujua sana Zurri...
Umenijulia wapi mrembo ? Ila jf kubwa sana,yaani kama jiji fulani hivi ambalo lina mitaa kibao na watu wanaishi maisha yao kimpango wao na wanajuana na kutokujuana pia.
 
Kwangu Mimi furaha yangu ni muhimu kuliko jambo lolote na sipangiwi kufanya jambo na mtu ili nimfuraishe never, never, na hamna wa Ku ni force ili iweje, furaha yangu na kila kitu I live own my own world na reality na sio ya watu wachache au wanaume walojipangia.

I'm a woman of principle so hzo definition za furaha ulizo zimention ni according to you not me, Kwa jamii ya yoyote aliyestaarabika hawezi shabikia uzinzi, ufisadi na ukandamizaji au lolote huyo ni uncivilized pia barbaric,so my friend toka kwenye huo mtazamo wakupangia wengine furaha au kikandamiza wanawake vile umemezeshwa since utoto you have to change kabisa, nakuwa huru while dunia inapambana kuondoa ukandamizaji wewe umekumbatia yani ni mhafidhina you don't want change.

So na Mimi nasema kuna dini zina ukandamizaji mkubwa though na zenyewe zimeanza kubadili perception towards women's discrimination maana mengi yaliyofanyika ilikuwa zama za mawe sasa hivi ni zama mpya kabisa.

Acheni bias zenu za uonevu Mara sijui nini blah blah zimepanda na kushuka Mara nchi what I want ni equal treatment mambo ya ukandamizaji tupa kule kwenye dustbin ya dark ages.
#SayNoToWomenDisriminationandChildren.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…