Ni haki yangu maana linanihusu na Uhuru wakujiamulia kufanya jambo linalonipa furaha sio kubanwa na MTU yoyote yule kunipangia na mindset zake.
Hili sasa ndio tatizo ndio maana mnalia lia,inaonekana hujui hata haki yako ni ipi na lipi si haki yako.
Nakufundisha sasa sio kila jambo linalokupa wewe furaha ni haki yako au linakuhusu,huu sio uhuru bali ni utumwa wa matamanio ya nafsi,inatakiwa muwe mnajifunza mjue lipi lenu na lipi si lenu na kwanini.
Nimekupima kwa swali rahisi sana lakini umeshindwa kujibu,nimekuuliza unajuaje kama lipi lako na lipi sio lako. Furaha sio kipimo cha wewe kujua hilo linalo kufurahisha ni lako,nakupa mfano wapo ambao wanafurahia na kufurahishwa na uzinzi,ufisadi,dhulma,wizi,unyang'anyi,kusema uongo,umbea,unafiki,uzandiki,kusengenya na mfano wa hayo,je ni kweli hayo mambo anatakiwa mtu kuyafanya hata kama yanamfurahisha ? Sasa bibie unatakiwa utoke katika utumwa ulio nao,utumwa ambao unakufanya ufikirie mambo kitoto na kwa upande mmoja,na uhuru bila mipaka ni utumwa na kutumia akili vibaya.
Nchi lazima ifate haki za raia za wananchi wake Kwa kutoa usawa Kwa kila jambo Kwa watu wake
Mimi nimeamua kukufundisha sasa,baada ya kuona hujui kitu juu ya hicho unacho kidai,hakuna haki isiyo zingatia maumbile na silika.
Nakuuliza swali,je huanza haki au huanza nchi ? Kama huanza haki kisha haki zinasimamiwa ni wazi kabisa nchi imezikuta haki na nchi haina uwezo wa kuijua haki mpaka haki iwepo,unakubaliana na hilo ?
Lakini,kauli yako bado inaonyesha ya kuwa haki ndio ilianza na serikali inasimamia haki,sasa swali la msingi liko pale pale,je unajuaje kwamba hii ni haki yako na hii si haki kisha ndio serikali ije kuisimamia ?
Dini ambayo ni muongozo wa wanadamu imemkandamiza mwanamke hasa dini flani siitaji.
Najua unaashiria dini gani,naweza kukupa hata miaka elfu uonyeshe wapi imemkandamiza mwanamke kisha ujibu kila swali nitakalo kuuliza,najua hutaweza kujibu hata swali moja,sababu hata misingi ya haki na haki yenyewe huijui.
Unaiweza kuniambia hiyo dini imemkandamiza wapi mwanamke na wewe umejuaje hilo na marejeo yako ni yapi na kwanini hayo marejeo yako tuyafate ?
Ndio mana nili prefer mada huru bila kuingiza hizi dini maana hazi encourage watu kufikiria nje ya chupa
Naendelea kukufundisha bibie,hakuna mtu ambae anafikiria kwa uhalisia kuliko mtu mwenye dini,sababu mtu wa dini anakuwa na yote ya dunia na akhera,na anafikiria pale ambapo akili ilipokomea.
Nilikuuliza juu a kufikiria nje ya box,na ulitoa maana nzuri sana,ambayo kwa maelezo yako inaakisi ya kuwa kwanza uko kinyume na maana ile bali hujaielewa na huifanyii kazi pia. Katika maana yako ulizungumzia kuhusu faida na hasara au kama ulivyoandika,lakini ajabu kiutendaji na maandishi yako hayaonyeshi kama unazingatia faida na hasara katika kulitaka jambo.
Nipo ...