Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Mimi mwanajeshi sichoki upesi
Yaani Ni wabishi Sana.
Ila huyu Marianah huwa hachoki[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1373][emoji1373][emoji1373][emoji1373][emoji1373]
 
@SAINTANNE I am fvcking sick and tired of your incessant biased diplomatic game. Hope you read this comment below .. You better stay on the sidelines from now.
Sawa.

Sicomment Tena hata Kama nnawashwa kiasi gani.
 
Yaani nashangaa mtu anajifananisha na Suleiman aliyekuwa na imani ya kuhamisha milima wakati yeye hana hata imani japo ya kusogeza kiti tu hawajui kwamba wale imani zao ziliwabeba na kumfanya Mungu asamehe maovu yao yote
Wanaume kujifananisha na suleiman wananichekeshaga kweli

Unakuta mtu anasema mfalme Suleiman wakati hata baiskeli hana, nguvu za kiume za kudunduliza, hekima hana wawe wanajitolea mifano wanayofanania lakini vinginevyo tutawacheka sana tu
 
Habari za usiku huu wana jukwaa, kabla ya yote naomba kwanza niwasihi sana wale wavivu wa kusoma nyuzi ndefu kwamba huu uzi tafadhali kabla hamjatoa comments zozote naombeni muusome wote kama ulivyo kuanzia mwanzo hadi mwisho halafu ndiyo mtoe comments maana kuna watu wana tabia ya kukurupuka kuchangia vitu ambavyo tayari vimeshafafanuliwa kwenye uzi.

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza, leo nataka niongee na wanaume wanaoongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwao kana kwamba wanaume hawakosei kwenye jamii wakati maovu yote yanayofanywa na wanawake ni sawa tu na maovu yote yanayofanywa na wanaume lakini kabla sijaendelea naomba niorodheshe kwanza maovu yanayofanywa na wanawake na jinsi yanavyoendana na maovu yanayofanywa na wanaume.

1. Wanawake wanaochepuka wanaendana na Wanaume wanaochepuka

2. Wanawake wanaozalishwa bila ndoa/nje ya ndoa wanaendana na Wanaume wanaozalisha bila ndoa/nje ya ndoa

3. Wanawake wanaojiuza wanaendana na Wanaume wanaowanunua

4. Wanawake wasagaji wanaendana na Wanaume mashoga

5. Wanawake wanaopenda kutembea na waume za watu wanaendana na Wanaume wanaopenda kutembea na wake za watu

6. Wanawake wanaopenda kutoka na mijibaba alias sugardaddies kwa ajili ya pesa wanaendana na Wanaume wanaopenda kutoka na mijimama alias sugarmummies kwa ajili ya pesa

7. Wanawake waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya pesa tu wanaendana na Wanaume waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya mbunye tu

8. Wanawake wanaopenda kuhudumiwa (kupewa pesa, kununuliwa vitu et al) na wapenzi wao wanaendana na Wanaume wanaopenda kulelewa (kupikiwa, kufuliwa et al) na wapenzi wao

9. Wanawake wasio na utii kwa waume zao wanaendana na Wanaume wasio na upendo kwa wake zao

10. Wanawake wanaowaacha wanaume waliowasomesha wanaendana na Wanaume wanaowaacha wanawake walioanza nao kwenye umasikini

Hayo ni machache mengine mnaweza kuongezea ila nimeona nijikite zaidi kwenye maovu yanayohusiana na ngono kwa sababu ndiyo janga kubwa kwenye jamii na nilitaka niwaoneshe ni namna gani jinsia zote zina maovu yake kwenye jamii, sasa hapa najua wapo watu watakaoleta habari za kutaka usawa sijui ushindani sikilizeni niwaambie, wanawake na wanaume tutatofautiana kote lakini siyo kwenye uovu yaani tutatofautiana kwenye jinsia, nafasi na majukumu lakini tofauti zote hizo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti kwa sababu tu wao ndiyo wako juu ya wanawake

Wapo wengine watasema eti wanaongelea sana maovu ya wanawake kwa sababu wanawake ndiyo wanaopata madhara kuliko wanaume kwamba wanaume wao linapokuja kwenye swala la mahusiano ya kimapenzi hawana cha kupoteza kabisa ila niwaambie tu kuwa bado hiyo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti ili tu kuwakomoa wanawake sasa mbona na magonjwa ya zinaa nayo hayaangalii jinsia na yanaua wote wanawake na wanaume kwa mtindo ule ule??

Halafu pia kinachonishangaza kama kweli wanaume hamna cha kupoteza kwenye mapenzi kwanini ninyi ndiyo mnaoongoza kwa kuyalalamikia na kuyaongelea maovu ya wanawake humu mitandaoni na mitaani kila siku?? Kuna mmoja alisema eti mnafanya hivyo kwa lengo la kutusaidia sasa kama kweli mngekuwa mna nia ya kuwasaidia hao wanawake wenye hayo maovu kwanini muishie kuongea kwa mdomo tu na siyo kufanya kwa vitendo??

Eti unakuta mwanaume anasema "kuna demu jana nilimtongoza akakubali muda ule ule na akanipa mzigo muda ule ule" halafu anamalizia kwa kusema "daah wanawake wa siku hizi mnajirahisisha sana acheni umalaya la sivyo wanaume tutaendelea kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha" sasa mwanaume kama huyu unamuona tu ni jinsi gani alivyo mnafiki yaani anajifanya kusikitishwa na wimbi la wadada kujirahisisha wakati huo huo yeye ndiye kinara wa kuwatongoza hao wadada ili wajirahisishe sasa kama kweli huyu mwanaume angekuwa hapendi wanawake wajirahisishe kwanini asiache kuwatongoza na kuwaomba mizigo kama hana nia nao??

Namaanisha kama wanaume mna nia ya kutusaidia wanawake na mmeona kwa maneno haisaidii kwanini msifanye kwa vitendo kwa kuacha hayo mambo yanayowafanya wanawake wajirahisishe kwenu?? Halafu wanaume wengi utasikia wanasema "kwanini mwanamke ukitongozwa ukubali" badala ya kuuliza "kwanini mwanaume anatongoza pasipo na nia ya dhati" yaani wanalazimisha ionekane kama mwanaume kutongoza siyo kosa ila mwanamke kukubali ndiyo kosa wakati actually kinachoanza ni kutongoza halafu kinachofuata ndiyo kukubali au kukataa hivyo lazima tukubali kuwa mwanaume anayetongoza na mwanamke anayekubali wote wana makosa na haya yote ni kutokana na tamaduni kandamizi zilizoanzishwa na mababu zetu enzi hizo bibi zetu wakiwa hawana sauti kwenye jamii hivyo walitupiwa mizigo yote na walilazimishwa kuikubali watake wasitake nasikitika kusema kuwa mamlaka ambayo wanaume walipewa na Mungu juu ya wanawake babu zetu waliyatumia vibaya kwa bibi zetu yaani waliyatumia kuwakandamiza badala ya kuwalinda

Kitendo cha kulazimisha kwamba mwanaume akitenda dhambi ni sawa ila mwanamke akitenda dhambi ni kosa ni kinyume hata na maandiko kwa sisi tunaoamini katika Mungu na Dini yaani jamii yetu imejenga mitazamo ya hovyo inayochagizwa na mfumo dume kwamba eti maovu ya mwanaume hayatakiwi kuhojiwa wala kurekebishwa bali maovu ya mwanamke ndiyo yanatakiwa kuhojiwa na kurekebishwa halafu wanalazimisha kwamba eti ni Mungu ndiyo ametaka hivyo ni mungu gani huyo aliyesema wanaume mtende dhambi mnavyojisikia eti ili tu mjitofautishe na wanawake na muonekane mko juu ya wanawake?? Ukweli ni kwamba tofauti kati ya mwanamke na mwanaume haipo kwenye dhambi hata siku moja yaani imefikia hatua wanaume wanajisifia umalaya na tena wanakataa kabisa eti mwanaume haitwi malaya bali kidume ukiuliza hiyo ni kwa mujibu wa nani hawana majibu wanakuja na mapovu!!

Kama kila jinsia imeshindwa kubadilika kwa nafasi yake na kusubiria eti jinsia nyingine ndiyo ianze kubadilika halafu nayo ndiyo itafuata basi niwasihi tu tuache kusubiri meli kwenye uwanja wa ndege au embe chini ya mkorosho mimi naona ifike pahala jamii iache uongo na unafiki kama tumeamua kukemea maovu tukemee kwa jinsia zote na kama tumeamua kuacha yaendelee tuache kwa jinsia zote after all wanaume si hamna cha kupoteza bwana so why mjihangaishe?? Ninyi endeleeni kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha halafu tutaona mwisho wake maana hata hivyo pamoja na malalamiko yote haya ya wanaume kwa wanawake naona ni kama vile mnajaribu kudeki bahari au kufagia jangwa tu!!

Kwa kuhitimisha naomba niseme tu kuwa hiki nilichokiandika ni robo tu ya nilichonacho ila kwa sasa naomba niishie hapa lakini bado nina mengi ya kuandika hapa sitayamaliza ila nitajaribu kuyajibu kwenye comments kutegemeana na maoni ya wadau japo najua nitaoga mapovu ya kutosha hasa kutoka kwa jinsia ya kiume lakini sitajali nayakaribisha ila wale wazee wa kukisia maisha ya watu wale wa "wewe utakuwa na stress za wanaume siyo bure" au wale wa "wewe unapenda kujilinganisha na wanaume" maana wenzetu mkiguswa kidogo tu mnakimbilia kusema wanawake tunataka usawa au ushindani na wanaume utafikiri labda wanaume mna kitu cha ziada mmependelewa nacho yaani labda wenzetu hamfi mnapaa mbinguni moja kwa moja kama mlivyo na ingekuwa hivyo mbona ningebadili jinsia kabisa niwe mwanaume ili nisife ila tofauti na hapo sijaona cha kunifanya nitake kujilinganisha na mwanaume maana hapa duniani kinaogopwa kifo tu kwa sababu hakikwepeki ila mengine yote yanakwepeka tu na tunayoweza kupambana nayo tunapambana nayo kikubwa uhai sasa leo naomba mje na hoja tafadhali hizo kauli zenu za ushindani sijui usawa siyo hoja bali ni mihemko tu

Nipo....
Ukitaka kufananisha mwanamke na mwanaume tuko sawa, unajipotezea muda..haswa hapa Africa
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ila huyu Lizarazu Ni jeshi la mtu mmoja[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Kumbe Hadi Nyenyere hamfikii..
 
Cariha anajinasibu kuwa amestaharabika wakati hana ustaharabu wowote, amejawa na mihemko tu na mdomo mchafu
Nilimuona tangu mwanzo. Sijui kwanini inakuwa ngumu kwao kufanya majadiliano bila kuingiza hisia. Anatakiwa ajifunze kwa marianah jinsi ya kufanya majadiliano bila ya kuingiza ad hominem attacks...
 
Vitabu vya Mungu vimemfeva sana mwanaume kuliko mwanamke.
Tumekua programmed tangu utotoni kwamba men are more superior and more deserving than women.

Unknowingly, we feel entitled to do wrongs and be tolerated, but a woman is supposed to behave properly at all times. We have been programmed like that.

Laumu vitabu vya Mungu, sio wanaume. kama vitabu vya Mungu vingeandikwa katika maudhui ya usawa basi maisha, na jinsi tunawavyowachukulia wanawake ingekua tofauti.

Kwa vile hatuwezi kubadili maandiko, hata mtoto wa kiume utakaemzaa kesho atakuzwa na mafundisho haya haya tuliyokuzwa nayo sisi na atabehave kama tunavyobehave sisi watu wazima, na hii endless cycle haitaweza kuwa broken.
Hakuna program men are physically, biological and emotional superior to women... Kwenye intelligence sina uhakika but historically tu naonekana we are by far superior
 
Hahahaha unakwepa hoja mkuu
]


Hakuna mfalme ambaye hajawahi kuua.

Waanzishie Uzi wasiojua Habari za Huyo Suleiman na wasiojua dunia inatoka wapi, Ilipo na inapokwenda.


Kwa habari ya Historia huna utakachoniambia maana huko ndipo nilipobobea.

Kwa habari ya lugha ndio kabisa. Sheria ndio usije ukagusa.

Habari ya falsafa usithubutu kabisa.

Binafsi najua hujui unachokipigania. Hujui matokeo ya wale waliokuwa wakisimamia kitu unachokisimamia leo hii.

Hapa utahangaika tuu Mkuu lakini mwisho wa siku hakuna utakalobadilisha kwenye huu ulimwengu.

Mwanamke hata asaidiwe vipi atabaki kuwa hivyo hivyo alivyo. Haijalishi yupo Ulaya au Asia. Ni yule yule siku zote.
 
Sisi hatupigia makelele kama unavyojinasibu humu.

Hizo ni propaganda tuu za Watawala.

Unaonekana hujui mambo mengi kuhusu huu ulimwengu.

Hata Wazungu wanawaandama kila siku Waafrika kwa maneno ya kejeli na dhihaka. Wanasema waafrika ni wajinga, wakatili, masikini n.k Lakini hizo ni propaganda za Watawala wa kizungu.

Hata Wachungaji na Mashekhe wanamuandama Shetani na mawakala wake yaani waganga wa kienyeji na wachawi. Hilo ni tabaka tawala linashambulia tabaka tawaliwa ambalo ni la shetani.

Kama hujui sifa ya tabaka tawala huwezi elewa wanachokifanya wanaume.

Kama nilivyokuambia endelea kupigana ba upepo lakini najua mambo haya yanaishia humu. Ukitoka hapa kaoshe vyombo, kafue na kumpikia mumeo.

Ni hayo tuu
Hahahaha mbona umekazania hayo ya kumfulia na kumpikia mume wangu utafikiri kufanya hayo ni adhabu?? Au ndiyo unajaribu kupotezea mada?? Hayo mbona nayafanya vizuri tu sababu hata yeye ananihudumia na anatimiza majukumu yake yote kama mwanaume!! Jaribu kingine!!
 
Wewe ni dhaifu ulipata miteremko dawa ya moto ni moto tu loh, na kwangu sio lazima unielewe Mimi ni negative ungrkuwa positive tunge attract each other.
Hao wawili niliowataja wanakuzidi mbali sana kiupeo.

Hata jinsi wanavyo shiriki mijadala tu hawako kama wewe. Akili zao zimetulia sana

Hawako too sensitive and emotional kama wewe.

Hawana argumentation chains mbovu mbovu kama ulivyo wewe ambaye karibia kila hoja unarudia maneno yale yale tu na huku ukijibu kwa mkato mkato hata pale unapotakiwa kutoa ufafanuzi wa kina.

Hawana kawaida ya kutoa majibu yaliyo njee ya mantiki, tofauti na wewe ambaye karibia kila jibu unalotoa linakuwa out of context ya kile ulichoulizwa.

Wanajua kujenga hoja na kuitetea tofauti na wewe ambaye haujui hata kuitetea hoja yako mwenyewe, unatoa hoja kisha baadae unakuja una ji contradict mwenyewe.

Hawana midomo michafu na kuandika andika matusi ovyoo mitandaoni mithili ya chokoraa kama ulivyo wewe.

Angalau wanajua hata wanachosimamia na kukitetea tofauti na wewe ambaye hata haujui unasimamia wapi halafu unajikuta mjuaji.

Kiufupi hao wawili wako smart kwenye majadaliano, hoja zao wanazojenga zina nguvu na zinafikirisha na wala sio nyepesi mithili ya karatasi ambazo nimeziona wewe ukiziandika hapa.

Mwisho kabisa jitahidi ukue bado una utoto mwingi sana wa kupayuka payuka tu na panick za ajabu ajabu.
 
Back
Top Bottom