Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Tatizo lako unajifanya umeshai hack mind yangu. Na pengine wakati unaandika huu uzi ulikuwa tayari una mawazo yako kichwani kuwa mimi nikija hapa mchango wangu utawa vipi.
Ndiyo kwa sababu you are always negative on issues concerning women!!
 
Sijakukariri ila ningekuwa na uwezo ningepekua comments zako zote tangu ulipoanza kucomment hapa JF hadi leo ili nipate walau japo mbili au tatu tu zinazoongelea mazuri ya wanawake halafu ndiyo tungejua kosa ni la nani mimi kukukariri au wewe kutaka tukuone hivyo
Unaoana sasa, punguza kunikariri
 
Mkuu hivi unadhani kwanini wanawake wanakaa uchi??
Sipati picha hicho kipindi ambacho kweli mtakuwa nyie ndo mna sauti ya mwisho duniani cha kwanza viwanda vya nguo vitafungwa maana hakuna kiumbe mwenye utashi anayependa kukaa uchi kama sio half naked kama mwanamke.
 
hapa upo sahihi
Na huu ukuu hutumiwa vibaya na wanaume karibia wote.
Wamebaki waking'ang'ania tu kuwa Ni vichwa lakini matendo yao hayasadifu wayasemayo...


hapa haupo sahihi, imani bila matendo ndio inaexist now, watu wanaamini ila hawatendi kulingana na imani zao.

imani inayoambatana na matendo ndio imekufa, mana watu wanaamini ila hawaiexpress hio imani kimatendo.

Mwanaume anaamini yeye ni kichwa cha familia ila huduma hatoi, mwanamke anaamini baba ndio kichwa cha familia lakini hampi heshma yake na anataka usawa, akilini akijua kabisa hakuna kampuni yenye CEO wawili, ila anataka kulazimisha.
Na imani bila matendo imekufa...

hapa umeongea ukweli kabisa Saint anne

kichwa Cha familia bila vitendo nilivyotaja hapo juu Ni sawa na kazi bure.
 
Haya maneno angeyasema mtu mwingine ningeshangaa ila kwa vile ni wewe sikushangai
Maandishi marefu hata hayaelweki Boss..... Yanaleta usingizi tu.
 
Sawa wanaume endeleeni kuongelea maovu ya wanawake ipo siku mtafanikiwa kuyarekebisha yote msijali
Hunijui vema, siko humu jukwaani kubishana. Natoa mchango. wangu tu, si lazima ukufurahishe na hiyo ndiyo democracy.. JF where we dare talk openly and I am doing just that!!
 
Cariha if you don't mind can I ask you this??

Are you a Kenyan??
 
Mbona mnalazimisha mada iwe utawala badala ya maovu?? Nilijua tu wengi hamtajisumbua kusoma huu uzi ila cha ajabu mnakuja comment na matokeo yake ndiyo haya kuandika ambavyo havipo kwenye mada!!
 
Namaanisha mwanga una outdo giza[emoji2][emoji2] japo vyote ni muhimu.
Sawa kwahiyo hapo mwanga ni nani na giza ni nani?? Na ukijibu uje na vigezo ulivyotumia kutoa jibu lako!!
 
Unafungua duka sehemu ukitegema wateja waje, wasipokuja unafunga. Unafungua kampuni sehemu kama biashara inakufa.....wanaume tunahitaji mbunye lakini kama hakuna wa kununua i think tutaoa
Oohh
 
Nature. Nikirefer Quran inasema wanaume ni viongozi wa wanawake. Sasa we na prefect wako mnataka muwe sawa? Au hukuona shuleni?
Ndiyo kwenye maovu wote sawa tu na hata maandiko ndivyo yanavyosema na hata huko mashuleni pia kuwa prefect siyo ticket ya kufanya makosa na kutarajia asikosolewe
 
Mkuu, kwa wakristo hakuna ndoa za wake wengi wala waume wengi bali kuna ndoa za mume mmoja na mke mmoja tu na hata maandiko yapo.

Halafu hapo mnapotolea mifano ya hao mitume na manabii ndipo ninapowashangaa sana hivi mnajua hao mwisho wao ulikuwaje na je mnajua kuwa hao baadhi yao waliua na kuua kabisa lakini bado Mungu aliendelea kuwabariki sasa utasema kwamba kuua siyo dhambi tena kwa sababu kuna mitume na manabii waliua na Mungu aliwabariki?? Au mnadhani mtu kuwa mtume au nabii basi ndiyo ameshakuwa malaika na siyo binadamu tena hivyo hawezi kutenda dhambi na kusamehewa??
 
Social constructionism is a theory of knowledge in sociology and communication theory that examines the development of jointly constructed understandings of the world that form the basis for shared assumptions about reality.

Mifano ya social constructs (mambo tuliyojijengea na kukubali kama social standards katika jamii)

1. mwanamke akiwa na wanaume wengi anaitwa malaya, mwanaume anaitwa kidume, na unakuta hata mamaake anafurahia moyoni. na sometimes unakuta mama mzazi anawaambia rafiki zake "huyu akikua atakuja kuwasumbua wadada, kisha wanacheka"

2. binti haruhusiwi kukaa nje hadi usiku, mtoto wa kiume anaweza kukaa hadi saa tano usiku, akarudi nyumbani bila kufanywa kitu chochote.

3. mtoto wa kiume anajengewa chumba chake cha nje, mtoto wa kike lazima akae kwenye main house

4. mtoto wa kike akipata mimba ataadhibiwa na anaweza akafukuzwa kabisa nyumbani, mtoto wa kiume akimtia binti mimba hawezi kufukuzwa nyumbani

hata wewe ukizaa mtoto wa kiume utaziendeleza hizi standards. amini usiamini. usipoziexpress wewe, ulimwengu utamfundisha how things run in the world.

kumbuka, sihalalishi uovu wowote, naelezea tu source ya haya yote.
Mbona mnalazimisha mada iwe utawala badala ya maovu?? Nilijua tu wengi hamtajisumbua kusoma huu uzi ila cha ajabu mnakuja comment na matokeo yake ndiyo haya kuandika ambavyo havipo kwenye mada!!
 
Wewe Lizarazu acha uongo miaka 15 iliyopita si ulikuwa mvulana tu tena ulikuwa hata bado haujabalehe wewe sasa huo mfumo wa sasa unaousemea umeuishi lini??

Ila nimegundua tatizo wanaume wengi wa kiafrika mnaona kuwakandamiza na kuwaonea wanawake ndiyo namna ya kujionesha kuwa mko juu yao tofauti na hapo mnasingizia kwamba wanawapanda vichwani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…