Ni kweli kabisa maandiko yapo wazi katika hayo yote,kizuri ni kwamba unasoma vema biblia!
Umejibu baadhi tu ya hoja nikizokupa,nami nitakupa majibu machache lakini nitarejea hapo juu kukumbusha yale ambayo uliyasahau!
Mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa,ndiyo! Kama baba/kichwa cha familia anapaswa kuwa clear,kama anaweza kuoa mmoja,wawili, watatu ... Kwa nini ajifiche fiche? Anapaswa kufanya maamuzi ya kiume,ni either nabaki na mmoja au naingeza wengine ASIZINI!
Hapo utawatazama mababa wa imani,kuanzia IBRAHIM, na wengine wengi katika maandiko,waliweza kujitwalia wake kwa kadri walivyotaka,kikubwa uwezo wao wa kuwahudumia ujitosheleze
Lakini hakuna mahali mwanamke ameolewa na waume wawili au watatu katika marejeo ya kimaandiko,ukipata popote nitakulipa nusu ya pesa zote nilizo nazo!
Then mwanaume atamwacha baba yake na mama yake,naye ataambatana na mkewe,ni sawa kabisa,hapo mwanaume anapewa majukumu rasmi ya kumuongoza mke,(kwani ukienda mbele zaidi katika maandiko ulitlyoyanukuu,yanamtaja mwanaume kuwa kichwa cha familia) kwa maana hiyo,mke pamoja na kuwa anakuwa mwili mmoja na mumewe lakini mwenye kuongoza na kuendesha mambo ya huo mwili mmoja,amepewa mwanaume ambaye ndiye "kichwa"
Kwa hiyo dhana nzima ya kutenda dhambi haina justification,haijalishi anayeitenda ni mwanamke au mwanaume!