Hahah wanawake hamjawahi kutulia, ni swala la mda tu before hujajishtukia tena. Utaomba ID mpya.Hamna mwaya kila id ninayoitumia naona haifai sababu nilikuwa sijapata id muafaka ila nadhani hii ndiyo nitakaa nayo kwa muda mrefu zaidi halafu hauwezi amini id zote kanibadilishia Melo mwenyewe maana yeye ndiye yuko active muda wote
Mods wengine hawako active sana unampm leo anakupm back baada ya wiki mbili ila Melo anakupm back siku hiyo hiyo au akichelewa sana ni siku mbili kwahiyo nahisi kuanzia leo nikimpm tena Melo kumuomba anibadilishie id atanipotezea
Mi nimesema usemacho uko sawa kabisa 100%...Naomba hunielewe nimekwambia tatizo ni mfumo dume Ova!!..we naona unaniletea mada ambazo mi sijazizungumzia mara hujakua mara maandiko yameruhusu wanaume kutenda dhambi....hayo sijataja apa labda wewe ndio naona una mihemkoNikuwe mara ngapi?? I might even be older than you!!
Kwahiyo muumba aliposema mwanaume atamtawala mwanamke ndiyo alimaanisha mwanaume atende dhambi anavyojisikia huku mwanamke awe mtakatifu?? Uje na andiko kutoka kwenye biblia la sivyo acha mihemko!!
Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote dada.Hizo sifa nimeziona na ninaamini ni za kweli kabisa (sijasema ni halali alivyomjibu yule dada hell no!!! ) ila kwa sifa alizotupa ni kweli kila alichoandika and as for me huwa ananisifia sana japo tunalumbanaga ila alishaniambia mimi ni miongoni mwa watu smart Jf.. Lizarazu popote ulipo najua haukuni flatter[emoji23][emoji23][emoji23].
So Karma hata kama Lizarazu anabishana na wewe na anakubishia kila kitu au kila unachoandika anaona ni mfumo dume haina maana wewe ni kilaza wewe bado ni smart na ndio maana anaendelea ku argue na wewe ni vile tuu mjadala wowote ili uende lazima pawe na wanaopinga na wanao support.
Kuamini kitu ambacho mwenzako hakiamini haimaanisha yeye ni mjinga. Cha msingi ni kuweza kusimamia unachokiamini na kujikita kwenye mjadala.
Mfano Kiranga haamini uwepo wa Mungu na mimi nina amini Mungu yupo sasa hiyo hainipi uhalali wa kumuona yeye ni mjinga, au yeye anione mimi ni mjinga kwa sababu anasema Mungu hayupo na anasimamia anachokiamini na ana point zinazoeleweka hata kama hauta kubaliana nazo. Na mimi nikiingia kwenye mjadala kama nimesimamia ninachokiamini na nimejikita kwenye mjadala hata kama haamini point zangu.
Hivyo sifa za Lizarazu na amini ni za kweli kabisa kwa mtu yoyote mwenye akili sema sasa hiyo ya kusifia kwa mtu mwingine hiyo sasa.........
Unajipa moyo eeh.Hahahaha inawezekana wanawake hatujatulia ila hatujawazidi wanaume aise
😀😀😀 sawa mamilooMoyo ninao tayari hivyo siwezi kujipa mwingine mkuu!!
Kupiga punyeto na matumizi ya ndomu?Hakuna Mwanaume anaweza kuwa na roho kama ya wanawake wanaofanya Abortion. Yaani wanaoua vichanga au kuwatupa chooni au mtaroni na kusepa.
Eeeh mkuuu list ungeitaja tu maana hayuko pekee ana tag hilo chaf pozi;Karma unapenda battle haijapata kutokea. Inabidi uingie kwenye Guinness World Records. Ingawa ninatumaini kwamba huu ubishi unaishia jamii forum, ukiwa kwako ni mke msikivu na mtiifu.
Kwani haya ninayoyaandika humu ni uongo??
Eeeh mkuuu list ungeitaja tu maana hayuko pekee ana tag hilo chaf pozi;
1)Karma
2)cookie smokey
3)cariha.
Hzo ni chaf poz hatari zinapenda battle hadi zinasahau kula.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kama nyie mlovyomshikia Lizarazu.Mmoja akitoka kwenda kula anamuaga mwenzake amshikie ubishi
Eeeh mkuuu list ungeitaja tu maana hayuko pekee ana tag hilo chaf pozi;
1)Karma
2)cookie smokey
3)cariha.
Hzo ni chaf poz hatari zinapenda battle hadi zinasahau kula.
Ila mashine mtaendelea kupigwa kama kawaWewe ulishawahi kumuona huyo mungu au vile viliandikwa na wanaume Kwa hisia mkajipendelea, acheni kujificha kwenye maandiko ili kukandamiza wanawake, eti mlaumu Mungu mxiiiiiew, ndio maana ili udumu na mwanamke lazima umuonee mwanamke, mabadiliko ya sasa ya wanawake kuwa huru mnabaki kulia lia umagharibi, I'm happy wanawake sasa tuna raise against all forms of discrimination na years to come tuta rule the world na nyie muanze kulia lia tu.
We tema mate chini, punyeto na arbotion ni vitu viwili tofauti kabisaaaaa. Ni sawa na kufanisha aliemwaga maji ya ugali na aliemwaga ugali wenyewe watakuaje sawa hao.Na Mwanamke anayefanya Abortion ni sawa na Mwanaume anayepiga punyeto. Wote wauaji.
Vyote sawaHabari za usiku huu wana jukwaa, kabla ya yote naomba kwanza niwasihi sana wale wavivu wa kusoma nyuzi ndefu kwamba huu uzi tafadhali kabla hamjatoa comments zozote naombeni muusome wote kama ulivyo kuanzia mwanzo hadi mwisho halafu ndiyo mtoe comments maana kuna watu wana tabia ya kukurupuka kuchangia vitu ambavyo tayari vimeshafafanuliwa kwenye uzi.
Kama kichwa cha mada kinavyojieleza, leo nataka niongee na wanaume wanaoongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwao kana kwamba wanaume hawakosei kwenye jamii wakati maovu yote yanayofanywa na wanawake ni sawa tu na maovu yote yanayofanywa na wanaume lakini kabla sijaendelea naomba niorodheshe kwanza maovu yanayofanywa na wanawake na jinsi yanavyoendana na maovu yanayofanywa na wanaume.
1. Wanawake wanaochepuka wanaendana na Wanaume wanaochepuka
2. Wanawake wanaozalishwa bila ndoa/nje ya ndoa wanaendana na Wanaume wanaozalisha bila ndoa/nje ya ndoa
3. Wanawake wanaojiuza wanaendana na Wanaume wanaowanunua
4. Wanawake wasagaji wanaendana na Wanaume mashoga
5. Wanawake wanaopenda kutembea na waume za watu wanaendana na Wanaume wanaopenda kutembea na wake za watu
6. Wanawake wanaopenda kutoka na mijibaba alias sugardaddies kwa ajili ya pesa wanaendana na Wanaume wanaopenda kutoka na mijimama alias sugarmummies kwa ajili ya pesa
7. Wanawake waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya pesa tu wanaendana na Wanaume waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya mbunye tu
8. Wanawake wanaopenda kuhudumiwa (kupewa pesa, kununuliwa vitu et al) na wapenzi wao wanaendana na Wanaume wanaopenda kulelewa (kupikiwa, kufuliwa et al) na wapenzi wao
9. Wanawake wasio na utii kwa waume zao wanaendana na Wanaume wasio na upendo kwa wake zao
10. Wanawake wanaowaacha wanaume waliowasomesha wanaendana na Wanaume wanaowaacha wanawake walioanza nao kwenye umasikini
Hayo ni machache mengine mnaweza kuongezea ila nimeona nijikite zaidi kwenye maovu yanayohusiana na ngono kwa sababu ndiyo janga kubwa kwenye jamii na nilitaka niwaoneshe ni namna gani jinsia zote zina maovu yake kwenye jamii, sasa hapa najua wapo watu watakaoleta habari za kutaka usawa sijui ushindani sikilizeni niwaambie, wanawake na wanaume tutatofautiana kote lakini siyo kwenye uovu yaani tutatofautiana kwenye jinsia, nafasi na majukumu lakini tofauti zote hizo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti kwa sababu tu wao ndiyo wako juu ya wanawake
Wapo wengine watasema eti wanaongelea sana maovu ya wanawake kwa sababu wanawake ndiyo wanaopata madhara kuliko wanaume kwamba wanaume wao linapokuja kwenye swala la mahusiano ya kimapenzi hawana cha kupoteza kabisa ila niwaambie tu kuwa bado hiyo siyo sababu ya wanaume kufanya maovu vile wanavyojisikia eti ili tu kuwakomoa wanawake sasa mbona na magonjwa ya zinaa nayo hayaangalii jinsia na yanaua wote wanawake na wanaume kwa mtindo ule ule??
Halafu pia kinachonishangaza kama kweli wanaume hamna cha kupoteza kwenye mapenzi kwanini ninyi ndiyo mnaoongoza kwa kuyalalamikia na kuyaongelea maovu ya wanawake humu mitandaoni na mitaani kila siku?? Kuna mmoja alisema eti mnafanya hivyo kwa lengo la kutusaidia sasa kama kweli mngekuwa mna nia ya kuwasaidia hao wanawake wenye hayo maovu kwanini muishie kuongea kwa mdomo tu na siyo kufanya kwa vitendo??
Eti unakuta mwanaume anasema "kuna demu jana nilimtongoza akakubali muda ule ule na akanipa mzigo muda ule ule" halafu anamalizia kwa kusema "daah wanawake wa siku hizi mnajirahisisha sana acheni umalaya la sivyo wanaume tutaendelea kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha" sasa mwanaume kama huyu unamuona tu ni jinsi gani alivyo mnafiki yaani anajifanya kusikitishwa na wimbi la wadada kujirahisisha wakati huo huo yeye ndiye kinara wa kuwatongoza hao wadada ili wajirahisishe sasa kama kweli huyu mwanaume angekuwa hapendi wanawake wajirahisishe kwanini asiache kuwatongoza na kuwaomba mizigo kama hana nia nao??
Namaanisha kama wanaume mna nia ya kutusaidia wanawake na mmeona kwa maneno haisaidii kwanini msifanye kwa vitendo kwa kuacha hayo mambo yanayowafanya wanawake wajirahisishe kwenu?? Halafu wanaume wengi utasikia wanasema "kwanini mwanamke ukitongozwa ukubali" badala ya kuuliza "kwanini mwanaume anatongoza pasipo na nia ya dhati" yaani wanalazimisha ionekane kama mwanaume kutongoza siyo kosa ila mwanamke kukubali ndiyo kosa wakati actually kinachoanza ni kutongoza halafu kinachofuata ndiyo kukubali au kukataa hivyo lazima tukubali kuwa mwanaume anayetongoza na mwanamke anayekubali wote wana makosa na haya yote ni kutokana na tamaduni kandamizi zilizoanzishwa na mababu zetu enzi hizo bibi zetu wakiwa hawana sauti kwenye jamii hivyo walitupiwa mizigo yote na walilazimishwa kuikubali watake wasitake nasikitika kusema kuwa mamlaka ambayo wanaume walipewa na Mungu juu ya wanawake babu zetu waliyatumia vibaya kwa bibi zetu yaani waliyatumia kuwakandamiza badala ya kuwalinda
Kitendo cha kulazimisha kwamba mwanaume akitenda dhambi ni sawa ila mwanamke akitenda dhambi ni kosa ni kinyume hata na maandiko kwa sisi tunaoamini katika Mungu na Dini yaani jamii yetu imejenga mitazamo ya hovyo inayochagizwa na mfumo dume kwamba eti maovu ya mwanaume hayatakiwi kuhojiwa wala kurekebishwa bali maovu ya mwanamke ndiyo yanatakiwa kuhojiwa na kurekebishwa halafu wanalazimisha kwamba eti ni Mungu ndiyo ametaka hivyo ni mungu gani huyo aliyesema wanaume mtende dhambi mnavyojisikia eti ili tu mjitofautishe na wanawake na muonekane mko juu ya wanawake?? Ukweli ni kwamba tofauti kati ya mwanamke na mwanaume haipo kwenye dhambi hata siku moja yaani imefikia hatua wanaume wanajisifia umalaya na tena wanakataa kabisa eti mwanaume haitwi malaya bali kidume ukiuliza hiyo ni kwa mujibu wa nani hawana majibu wanakuja na mapovu!!
Kama kila jinsia imeshindwa kubadilika kwa nafasi yake na kusubiria eti jinsia nyingine ndiyo ianze kubadilika halafu nayo ndiyo itafuata basi niwasihi tu tuache kusubiri meli kwenye uwanja wa ndege au embe chini ya mkorosho mimi naona ifike pahala jamii iache uongo na unafiki kama tumeamua kukemea maovu tukemee kwa jinsia zote na kama tumeamua kuacha yaendelee tuache kwa jinsia zote after all wanaume si hamna cha kupoteza bwana so why mjihangaishe?? Ninyi endeleeni kupiga na kusepa au kuzalisha na kuacha halafu tutaona mwisho wake maana hata hivyo pamoja na malalamiko yote haya ya wanaume kwa wanawake naona ni kama vile mnajaribu kudeki bahari au kufagia jangwa tu!!
Kwa kuhitimisha naomba niseme tu kuwa hiki nilichokiandika ni robo tu ya nilichonacho ila kwa sasa naomba niishie hapa lakini bado nina mengi ya kuandika hapa sitayamaliza ila nitajaribu kuyajibu kwenye comments kutegemeana na maoni ya wadau japo najua nitaoga mapovu ya kutosha hasa kutoka kwa jinsia ya kiume lakini sitajali nayakaribisha ila wale wazee wa kukisia maisha ya watu wale wa "wewe utakuwa na stress za wanaume siyo bure" au wale wa "wewe unapenda kujilinganisha na wanaume" maana wenzetu mkiguswa kidogo tu mnakimbilia kusema wanawake tunataka usawa au ushindani na wanaume utafikiri labda wanaume mna kitu cha ziada mmependelewa nacho yaani labda wenzetu hamfi mnapaa mbinguni moja kwa moja kama mlivyo na ingekuwa hivyo mbona ningebadili jinsia kabisa niwe mwanaume ili nisife ila tofauti na hapo sijaona cha kunifanya nitake kujilinganisha na mwanaume maana hapa duniani kinaogopwa kifo tu kwa sababu hakikwepeki ila mengine yote yanakwepeka tu na tunayoweza kupambana nayo tunapambana nayo kikubwa uhai sasa leo naomba mje na hoja tafadhali hizo kauli zenu za ushindani sijui usawa siyo hoja bali ni mihemko tu
Nipo....
Hii sio sawa kabisa, mwanaume atachepuka na atahudumia familia kama kawaida, ni nadra sana kwa mwanamke kuchepuka na kuendelea na mumewe. Kama wewe ni mwana MMU basi utakua umeona shuhuda nyingi za wadau wakivunja mahusiano na wanawake waliohamisha mapenzi yao kwa michepuko.1. Wanawake wanaochepuka wanaendana na Wanaume wanaochepuka
Kuendana kivipi hapo. Muuzaji ndie kaanza ndipo kaja mnunuzi na hapo utaona kua anaefanya ujuha ni anaeuza. Hebu fikiria mtu analala na zaidi ya watu 2 kwa siku utamfananisha na anaepita kwa mala moja tu. Tena huyo ni ajira yake kabisa jama jama unamfananishaje na mteja wa mala moja moja.3. Wanawake wanaojiuza wanaendana na Wanaume wanaowanunua
Hapa sijui kwasababu mashoga wanaonekana lakini wasagaji kuwagundua ni kazi wote mnaitana mpenzi na majina ka hayo.4. Wanawake wasagaji wanaendana na Wanaume mashoga
Idadi haifanani mkuu wewe pia unaweza kua shahidi wa hili.6. Wanawake wanaopenda kutoka na mijibaba alias sugardaddies kwa ajili ya pesa wanaendana na Wanaume wanaopenda kutoka na mijimama alias sugarmummies kwa ajili ya pesa
Hawaendabi hata kidogo, mwanamke atataka pesa na penzi, ndivyo mlivyoumwa. Na sisi tunataka mbunye coz huna cha kutoa ukiacha mbunye utatoa nini sasa, labda uwe mke lakini kama ni mpenzi tu nasikitika kusema kua girls wengi hamna cha kuoffer zaidi ya mbunye.7. Wanawake waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya pesa tu wanaendana na Wanaume waliopo kwenye mahusiano kwa sababu ya mbunye tu
Ni nature hiyo mkuu, mwanaume kumhudumia mwanamke na mwanamke kufanya izo kazi hapo ulizotaja. Ndio maana kwenye jamii zetu wanawake wanajua mambo ya mapishi kuliko wanaume, wanajua mambo ya usafi kuliko wanaume, ndivyo walivyoumbwa na izo hulka wala sio jambo la kustaabisha hilo.8. Wanawake wanaopenda kuhudumiwa (kupewa pesa, kununuliwa vitu et al) na wapenzi wao wanaendana na Wanaume wanaopenda kulelewa (kupikiwa, kufuliwa et al) na wapenzi wao
Daah yaani hata hii umeona iko sawa kabisa.10. Wanawake wanaowaacha wanaume waliowasomesha wanaendana na Wanaume wanaowaacha wanawake walioanza nao kwenye umasikini