Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Hivi ni kwanini wanaume mnaongelea sana maovu ya wanawake na kuyaacha ya kwenu?

Ndio nime majadiliano ya hoja nyie mumeshindwa kutetea hoja mnamsingizia Mungu wakati binadamu mumepewa utashi tofauti na viumbe wengine
Mkuu labda hukunielewa vizuri. Mimi binafsi siyo mfuasi wa hivyo vinavyoitwa vitabu vitakatifu. Kwa lugha nyingine nipo pamoja na suala la usawa wa kijinsia hususani katika mlengo wa utu . kitu nilichopingana na wewe ni katika suala la ufanisi katika mambo mbalimbali kati ya mwanaume na mwanamke. Ni dhahiri mwanaume ni bora kiufaninisi katika nyanja nyingi za maisha lakini hiyo haimpi haki kumnyanyasa mwanamke na hapo nakuwa nimeungana na wewe...
 
Wanasingizia eti maumbile yanawafavour sasa mbona na magonjwa ya zinaa nayo hayawafavour wote yanawaua kama yanavyowaua wanawake tu??
Suala la dhambi hili ni baya kwetu sote,haliangalii nani wala nani.

Tatizo linakuja pale mnapotaka kujitutuma na kulingana na sisi.

Tujikite kwenye mada.
 
Ngoja nitaanzisha Uzi kabisa maana watu wanachaganya mambo ya gender na Feminism kuwa ni movement za kupotosha wanaume kumbe si kweli.
Natamani haya unayoyaandika kwenye comments uyaanzishie thread kabisa ili kila mtu ayaone maana hapa najua kuna watu hawayaoni hivyo watakosa kuujua huu ukweli
 
Kuna biashara yoyote inayofanikiwa bila kuwa na wanunuzi?
Mnavyoonekana kukerwa na wanawake wanaojiuza nilitegemea kwa pamoja muungane mpinge kununua lakini sio mnanunua baadae mnakuja kuhubiri dhambi zetu.
Hivi ilikuwaje mpaka wanawake wakaanza kujiuza ?

Nakuja kuendelea hapa nilipoishia.
 
Wanaume wengi wenye wanawake wengi wana upungufu wa nguvu za kiume ingawa mnahangaika ka bisi kikaangoni. Na ndio maana wanawake huwa tunawafanyia matukio kimya kimya hamjui tu
ha ha ha utakuwa ni mtazamo wako tu mkuu
 
Hapo kwenye Eva kumpindua Adam ili awe kama Mungu,, ushahidi wako nausubiri hapa
[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]hakika wanawake ni jeshi kubwa nilitaka nimkazanie hapo ila nikaona nimuache maana comment yangu ingekuwa ndefu lakini asante umenisaidia na hata mimi nasubiri jibu lake hapo
 
Hujakosa.

Nani amekwambia hao walio olewa mitala/matala wamekosa wanaume ?
Walikosa pia kukimbilia ndoa nikutokujiamini kabisa pia uoga wa maisha huo. Yani mke wa nne kah si bora kuwa single. Niwaachie wenyewe na imani zao
 
Kwahiyo wewe unasemaje mkuu?? Yaani wanaume na wanawake wanatakiwa kubehave vipi kwenye jamii kutokana na maandiko??
Ndo mana nakwambiaje, ni mfumo uliwekwa kupitia vitabu vya Mungu jinsi ya mwanamke na mwanaume wanavyotakiwa kubehave kwenye jamii.

Huo mfumo unaotaka wewe uwepo inabidi uwekewe utaratibu wake ili usije ukakinzana na mafunzo ya kwenye dini.

kwa sababu mtoto wako wa kiume akipelekwa mafundisho atafundishwa misimamo ya kibiblia kuhusu wanawake na wanaume katika jamii.

akirudi mtaani na akienda shuleni anakutana na misingi mipya ya iliyowekwa na utandawazi.

akikaribia kuoa, mama mzazi anampa lisala kuhusu wanawake. yani mama mzazi anaogopa mtoto wake wa kiume asipelekeshwe na mke wake na anataka ahakikishe mtoto wake wa kiume ana uwezo wa kumtawala mke wake.

mwanamke huyo huyo anaelilia usawa, ndo huyohuyo anaemnong'oneza mtoto wake wa kiume asipelekeshwe na mke wake. Na akijua mtoto wake anatawaliwa, atavuruga tu hio ndoa.

Cariha rafki angu haya mambo yanakinzana sana.
 
You could have been a very good company to her.

Mtuvumilie tu, maisha yamebadilika katika kiasi ambacho hatukuwa tumejipanga nacho, we relaxed thinking kwamba we will always be on top.

Shule, utandawazi umeleta mabadiliko ambayo hatukuyategemea, so linapokuja swala la kukutana na wanawake ambao ni argumentative, cash self independent, brain na reasoning tunajikuta Thrones zinakuwa hatarini.

Kinachobaki kinafanyika, tunafanya personal attack, character assassination na abuses kuraise esteem yetu. Na hii ni kwa sababu tumeshindwa kupambana katika level hitajika.

Mtusamehe bure.
Usamehewe wewe,acha kujipendekeza kwa huyo binti
 
Walikosa pia kukimbilia ndoa nikutokujiamini kabisa pia uoga wa maisha huo. Yani mke wa nne kah si bora kuwa single. Niwaachie wenyewe na imani zao
Kwanza hujapinga swali langu.

Ushawahi kuiona kesho yako ?

Uoga wa maisha wa kutafuta hela au uoga wa maisha kulingana na mila na desturi ?

Pili,unajuaje huyu amekimbilia ndoa na huyu ameolewa wakati muafaka ? Hapa hutakiwi kubahatisha.
 
Back
Top Bottom