ward41
JF-Expert Member
- Apr 3, 2022
- 749
- 2,533
Nimesikia watu wakisema bara la Africa Lina utajiri mkubwa wa rasilimali. Cha kushangaza ktk somasoma yangu naona kama hatumo kivile.
Kwenye mafuta middle east, Canada, Russia, USA, Venezuela wanatamba. Kwenye gas ni haohao.
Madini ya chuma naona china, Iran, Chile, USA wanatamba. Kwenye rare earth naona china, north Korea.
DHAHABU naona china, Australia, Canada, Chile, Brazil wanatamba.
Kumbukeni wajomba hayo madini ndiyo yanayotamba Kwenye uchumi wa Sasa.
Kidogo naona DRC katutoa kimasomaso Kwenye cobalt na coltan.
Sasa hizo resources ziko wapi? Wese la Angola, Nigeria,Libya ni kidogo sana. They are not giants.
Je, ni Kweli tuna resources nyingi?