Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

Hivi ni kweli kileleni mwa mlima Kilimanjaro kuna shimo?

wa stendi

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
25,190
Reaction score
27,434
Poleni na mihangaiko ya hapa na pale pamoja na manung'uniko yanayoendelea kuhusu makenikia.

Husika na kichwa cha habari hapo juu tangu napata akili hadi sasa kumekuwa na maneno kuhusu mlima Kilimanjaro kuwa pale juu kileleni kuna shimo refu sana na inavyosemekana ndani ya shimo kuna maji na nguvu ya mvutano kiasi kwamba ukikaribia kufika hapo unavutwa na kunasa.

Wajuzi naomba kujuzwa je, Kuna ukweli wowote?

1637136088059.jpeg
 
Nnachokifaham, pale kileleni kwenye usawa wa juu kabisa wa mlima, hakuna shimo eneo hilo isipokua
unaweza kuona kwa mbali duara eneo lililopo hilo unaloliita shimo, ni njia ambayo ule ujiuji ulitokea hapo kutoka ardhini wakati wa volcano, ni kama kidonda kilichopona lakini hakikufunga, kuna uwazi. Nilitamani sana kwenda karibu na hilo eneo ila nilichoka mno hata kufika Uhuru peak ilikua bahati.


Hayo ya maji ya moto watakuja wataalam.
 
Kuna shimo kaka tena moja lipo kileleni na jingine kwa ubavuni kdg just 50 MTS. Toka shimo kuu. hakyna kuvutwa ila upepo in mkali hawashauri kufika pale unaweza kuteleza kuangukia ndani.nimeshawahi kufika km x5 hivi.
 
Shimo lipo pale panaitwa creter,,ukipita njia ya kialia machame ndio utapapita hapo creter vzr zaid kuliko mtu anaepitia njia ya marangu,,ila kuna barid sana kwa kwel,,sana sana sanaaaaaa..... Nadhan mto uzi ameuliza vzr tu ili kujua sasa ukimwambia akapande sidhan km ni jibu la uhakika sana alilolitegemea
 
Falcon Mombasa......swali lako linaniacha hoi saana.Najua uko Mombasa ...Tanga mara kwa mara kwa sababu ya kazi zako.kinachonipa shida ni kwa nini hilo swali lije leo na umeshafika Moshi mara nyingi.....???
 
Back
Top Bottom