Hivi ni kweli kina Chikwende ni zaidi ya akina Ajibu!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Jana kulikuwa na mechi kubwa hapa kwetu Simba na Azam! Matokeo tuliyaona na mpira ulikuwa mzuri. Cha kushangaza na sio Afya kwa mpira wetu ni uwepo waa Lundo la wageni. Zaidi ya asilimia 50 waliocheza jana ni wageni! ni kweli Ligi yetu sio ya ridhaa na mpira ni biashara ...Ila hii biashara Ina Afya kwa ustawi wa soka letu!?

Hakuna dhambi yoyote kuletaBwachezaji wa nje! Ila Ni wachezaji wa aina gani tunawahitaji! Hivi ni kweli humu jdai Hakuna wachezaji wanaomziddi Chikwende, Chirwa, Fiston, Lokasa! Hivi AJIBU ni wa kukaa benchi huku tukiwafanyia majaribio kina Chikwendwe!

Angalia beki Tatu na Mbili wa Yanga si wametoka huku Uswazi kwetu, vipi kuhusu Ame na Mwamyeto! Kuna tatizo mahali!
Kama tunafikia mahali tunatamba na kufurahia wachezaji na makocha kutoka Burundi na tunajiona wajanja. Kuna kitu somewhere hakipo sawa!

Kama hatutaamka tutaendelea kupokea kina Sarpong na Yikpe wa kutosha!
 
Chikwende ni Ajibu anaejituma, wachezaji wa kitanzania brother wanakua na u-father sana na wanabweteka so ni vyema hao wageni wawepo ili kuwafanya hawa jamaa wapambane na wasibweteke.
 
Tatizo Watanzania tunalalamika tukiwa hatuna nafasi, tukishapewa tunalala, tunataka tulipwe bure na kazi hatufanyi tena, ninayo mifano mingi, watanzania ni watu wa kubweteka sana, binafsi mimi siridhishwi na wingi wa wageni kwenye ligi yetu lakini hamna namna.
 
Watu wenye uwezo zaidi ya Samatta kule uturuki wapo kibao na Msuva Morocco pia.

Ramadhani Singano,Eliud Ambokile tunajua hawana uwezo wa kuwa Mazembe lakini tunajua uwepo wao Kule watapata vitu.

Sisi tunataka wachezaji wa kitz wasombwe waende nje Ila wao tunawawekea vikwazo.
 
Badala ya kulalamikia wingi wa wachezaji wa kigeni nchini kwetu, ningeshauri tuongeze jitihada za kuwajenga na kuwaimarisha wachezaji wetu wa ndani, wajitambue, wajiheshimu na wapate washauri sahihi, sio washauri makanjanja wanawapotosha na kuwaharibia maisha yao.
 
Utopolo mtupu

Weee uwezo wa mchezaji mmoja mmoja, kwa hapa bongo ndan ya simba

Chikwende unamlinganisha nanan?

Morison nanan?

Luis nanan?

Chama nanan?

Kagere nanan?

Bwalya Nanan?

Muwe mnaacha ujinga, yaleyale ya Mabeberu hawawapendi Waafrika.

Kama unatumia mchezo wa jana kujenga hoja yako
 
Nchi yetu imeingia kwenye ubaguzi.
Watu wenye uwezo zaidi ya Samatta kule uturuki wapo kibao na Msuva Morocco pia. Tukisema kila MTU arudi kwao itakuwaje?
 
Huna hoja takataka tupu umeandika! Kama hao watanzania wenzako wengekua wanakua sana mpira timu yao ya Taifa ingefika mbali
 
Uzuri mpira ni mchezo wa uwazi...Ajibu na wenzie kila wanapopewa nafasi....kiwango Chao kinakuwa chini Sana....Sio rahisi kocha kuendelea kumpa nafasi mchezaji ambaye haleti matokeo chanya...hata hao wageni wasipoleta matokeo watakaa benchi.
 
Mtu Kama ajibu usimtete kabisa .

Huyo jamaa Ni fala Sana alizichanga karata zake vibaya .

Aliondoka Yanga kwa dharau

TP mazembe walimuhitaji akawadengulia.

So acha apambanae na Hali yake

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Hata Simba aliondoka kwa dharau kwenda yanga ila kitendo cha kutoka yanga kurudi Simba kinawauma sana lakini kiukweli hao wazawa unaowatetea kiwango chao kidogo muangalie Mzamiru alipoingia alileta impact gani wazawa wa sasa hawajitambui wangekuwa wanajitambua kama wachezaji wa zamani na pesa wanazolipwa timu yetu ya taifa ingejaa wachezaji wa kulipwa
 
Mtu Kama ajibu usimtete kabisa .

Huyo jamaa Ni fala Sana alizichanga karata zake vibaya .

Aliondoka Yanga kwa dharau

TP mazembe walimuhitaji akawadengulia.

So acha apambanae na Hali yake

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
Mtoa mada amenishangaza anapo mtetea mchezaji kama Ibrahim Ajibu!! Mwenzake ndiyo anafurahia kukaa benchi huku mzigo ukiingia mwisho wa mwezi kama kawaida.

Dogo ana kipaji ila ni mvivu!! Baada ya kuona anahenyeshwa na Mwinyi Zahera na kupewa unahodha, akaona isiwe soo. Yeye na mwenzake Gadiel Michael wakaona ni bora kupokea mshahara, ila siyo kucheza!

Tofauti kabisa na maproo wa Ulaya.
 
Yule sio wa kumuonea huruma usikute ndio anawaona mafala

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Wabongo misifa inawalewesha,acha wawekwe benchi,kwanza itasaidi waanze rasmi kufungua mipaka watoke kama wana uo uwezo.
 
Wewe nini kinakuuma?Hawa wachezaji wa ndani si waoneshe uwezo wao kwenye timu nyingine,mbona ziko nyingi tu?

Pia waoneshe kiwango kwenye national team.Huwezi kuja na utetezi wa hisia za ukabila na ujinga zikiwa zimejificha ndani ya koti la uzalendo.

Wachezaji wetu wengi hawajielewi.Mchezaji akiwa mpenzi wa yanga siku timu yake ikicheza against yanga anajilainisha,vivyo hivyo kwa Simba.
Wachezaji wakishapata pesa ya pombe na mademu wanakosa nidhamu kabisa.
Tuanze na elimu ya kijitambua kwanza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…