Hivi ni kweli kuna dawa ya mapenzi?

Hivi ni kweli kuna dawa ya mapenzi?

kwamba eti kuna mganga wa kienyeji mahali Fulani, anaweza kumrudisha mpenzi wako alie potea au kukutoroka au kukufanya upendwe sana na boss wako ofisini au akupe dawa ya kupandishwa cheo kazini?

Au akupe dawa ya mvuto wa kimapenzi?🐒

vipi ndugu, uliwahi kujaribu kupitia njia hii na vipi matokeo yalionekana? nini kilikuchochea 🐒
Sawa zipo na unatakiwa u renew Kila baada ya muda but ya nn ufanye YOTE hayo ??? acha mtu akupende yeye mwenyewe
 
Mkuu hao wote unao waona wanavuma kwenye tasnia nyingi wanatumia waganga na hizo dawa za mvuto,hata wanawake wa mjini wanaohongwa magari,nyumba,biashara kubwa wanatumia madawa kuwavutia watu.

kuna madalali waliwahi kumwambia jamaa mmoja alikuwa kaenda kununua nyumba maeneo flani dar,sasa akajifanya ni dalali wa maeneo mengine tofauti na hapo basi dalali mmoja wapo akawa anajisifu yaani yeye hata nyumba iwe mbovu vipi yeye akimuonesha mteja hachomoi kabla ya kuongea na mteja anajipaka hiyo dawa akiongea kitu wewe mteja hupindui utakuja kushtuka mlishafanya biashara.

Hizo dalala mnazopanda uliza madereva wtakuwambia mengi sana kuhusu madawa.
ubishi tu ila ukweli wanaujua

kwa uzoefu tumewahi toka sehemu tukapewa dawa flani ya ngekewa

ebwana mmoja wetu akajipaka ile tunaingia kwenye bus kakaa mzee mmoja stori mbili tatu konda anapita achukue fedha mzee kasema kijana acha kamlipia nauli zaidi ya elfu 30

hapo ndo utaamini dawa zipo
 
Kama ilivyo Good and Evil, Mwanga na giza, panapo nguvu za Mungu basi na za giza zipo......kikubwa ni kutoa sacrifice, kama kwa Mungu utatoa sadaka, kufunga, maombi n.k basi vice versa is true hata na upande wa pili utafanikiwa pale utapotimiza masharti, shida ni pale utapoacha kutekeleza masharti na kurecharge hizo nguvu za giza na maagano, kiufupi nguvu za giza huwa hazidumu. Mganga wa kweli ni Mungu na uchawi wetu ni sala/maombi.
Sio kweli mfano unyamwezini wanajua dawa sana hazina masharti mfano kuna dawa inaitwa Nshoma hii inatoa mauchawi mikosi mapepo mabaya hata wale wenye mambo ya magendo unaikoga na kuimwaga chini unachora + pande zote hakukamati asikari yoyote haina masharti Kuna dawa yaitwa Mwelekela maana yake kuelekea inatumika Kwa mapenzi na biashara unalonuia linaelekea haina masharti isipokuwa inakufa nguvu baada ya muda kuna mkirungu ulopigwa na radi hii dawa ya mapenzi hutumia sana wanawake kuchanjiwa wanaume wakimuona moto unafanya paaaa kama umepigwa radi hii mwanamke pia anatia kwenye lotion mafuta ajipaka Kuna kalilila pia yaani dawa ziko nyingi sanaa na hazina masharti yoyote Tabora Shinyanga wengi wajua miti dawa na sio waganga.
 
kwamba eti kuna mganga wa kienyeji mahali Fulani, anaweza kumrudisha mpenzi wako alie potea au kukutoroka au kukufanya upendwe sana na boss wako ofisini au akupe dawa ya kupandishwa cheo kazini?

Au akupe dawa ya mvuto wa kimapenzi?🐒

vipi ndugu, uliwahi kujaribu kupitia njia hii na vipi matokeo yalionekana? nini kilikuchochea 🐒
Kwan nn kimekukuta 😀🙄🙄
 
Achana na hayo mambo
Fanya kazi kwa bidii cheo kitapanda.

Ukiwa mwaminifu kwa mwenza wako na yeye atakupenda na kukuamini.

Ukitaka kuwa Boss fungua kampuni yako na wewe uajiri wafanyakazi uitwe Boss.

Kikubwa ni Kufanya kazi kwa bidii na Maarifa, Uaminifu, Subira na kujishusha
Tatizo kuna wakati bidii hazileti mafanikio, niamini mimi.
 
Kwan nn kimekukuta 😀🙄🙄
nimekutana na bango kubwa sana, la kisasa mno, linawaka taa kabisa, likielekeza kuna huduma ya kumrejesha mpenz aliepotea ndani ya siku3, na pembeni kuna ofisi ya maana sana.

vijana warembo na watanashati wamepanga foleni kusubiri zamu zao waingie kupata huduma ya mtaalamu nikastuka na mojakwamoja nikaandika uzi, halafu sasa ilikua usiku mkali 🐒
 
Nisiwe mnafki nasali napokuwa na shida ila mwezi wa Ramadhan Qiyam Layl nasimama kama ibada sio shida zangu.swala za faradh nasali.
upo vizuri kama swala tano ipo dada.
Wengi tupo hivyo mpaka upate matatizo ndio unasimama usiku,swala za usiku zina malipo makubwa na hutatua matatizo...sema tunakuwa wavivu kuswali kila siku.
 
Nimesikitika sana kuona hakuna tapeli yeyote aliyejitokeza upande wa comments kumvuruga mtoa mada 🤒😎
kwamba aweke namba nijae mzima mzima kichwa kichwa sio?🐒

napendwa sana na wanainchi wangu kwa dhati sana, bure bila gharama yoyote mpaka raha aise 🐒
 
ubishi tu ila ukweli wanaujua

kwa uzoefu tumewahi toka sehemu tukapewa dawa flani ya ngekewa

ebwana mmoja wetu akajipaka ile tunaingia kwenye bus kakaa mzee mmoja stori mbili tatu konda anapita achukue fedha mzee kasema kijana acha kamlipia nauli zaidi ya elfu 30

hapo ndo utaamini dawa zipo
Dawa zipo mkuu.
 
Back
Top Bottom