Hivi ni kweli kuna dawa ya mapenzi?

aiseee 😳

si mchezo, mambo ni mazito hivi kumbe?πŸ’
 
Ni abrakadabra tu kwa wanaotamani mambo hayo. Waganga wanaangalia watu wanatamani nini na huanzisha matangazo kuwa wanatoa suluhisho hilo. Hata wezi hurubuniwa wakipewa dawa hawatakamatwa wakiiba
 
Ni abrakadabra tu kwa wanaotamani mambo hayo. Waganga wanaangalia watu wanatamani nini na huanzisha matangazo kuwa wanatoa suluhisho hilo. Hata wezi hurubuniwa wakipewa dawa hawatakamatwa wakiiba
huku kwenye maombi na maombezi vip, wanaeweza kua wamepenya wao pia nini.

maana kuwaombea watu mali na vitu wanavyotamani kua navyo naona ikitumika sana siku izi katika eneo hili. Je, huo utaalamu unaweza kua unatumia pia katika eneo hili au ni tofauti?πŸ’
 
πŸ˜€ Aanh sawa
 
umeeleza ukweli vizur sana, kwa uchungu sana, ndugu mwana familia..

bilashaka umeeleweka vizuri sana na Mungu akubariki sana, kwa sadaka yako ya huruma kwa familia hii ya JF.

hata hivyo, binafsi sihusiki kwa namna yoyote ile. Ni kwa Neema na Baraka za Mungu nimeleta hoja na ujumbe huu kwenu wadau, walau kukumbushana, kupeana uelewa na ufahamu wa mambo haya ili hatimae kila moja achague pa kufuata kati ya Nuru na Giza πŸ’
 
Quran ingekusaidia nini sasa bora tu ulivyokuwa unaiepuka kuisoma
 
unaweza kujikuta umekaribia kufika ofisini ndio unakumbuka umesahau hirizi muhimu maalumu nyumbani, ambayo mganga alikupa sharti la kutoisahau hata siku moja unapokwenda ofisini ili upandishwe cheo 🀣

Lakini Mungu, huwezi msahau, Daima yupo na wewe na wewe uko nae. Mtafute na kumuita maadamu anapatikana, na muite wakati yupo tayari...

na Mungu akubariki sana πŸ’
 
 
🀣🀣🀣! Wanajua binadamu wote wanapenda vitu vizuri! Be careful na hawa watumishi/nabii.
Ulimwengu wa roho ni zaidi ya tuujuavyo.
 
Miaka mitatu nyuma nimewahi kuwa kwenye mahusiano na binti wa kindali kutokea Mbozi ndanindani uko ila alikua anafanya biashara zake za salon na M-pesa maeneo ya mjini jirani na nilipokua naishi.
kuna siku kaja kulala kwangu nikamuagiza chips mtaani kwa kisingizio kuwa naumwa nikaamua kukagua mkoba wake [ni kawaida yangu kukagua mikoba au simu za madem zangu] nikakutana na tudawa twingi tumefungwa kwenye nyloni ndogondgo zaidi ya sita alivorudi nikamkazia ni dawa zanini akanambia kuwa huwa anapewa na mganga wake ili apate mvuto wa mapenzi ahongwe vitu vya thamani na biashara yake ya salon ishamiri.

nikaamua kuwauliza marafiki zake wawili ninao waamini ili nihakiki nikaambiwa kuwa ni kawaida yake kwenda kwa mganga kila anapoachika ili apate Bwana mwenye hela zaidi kuliko yule alomuacha.

to cut the long story short mahusiano yetu yaliisha, mwaka jana nmewasiliana nae akanambia biashara yake ya salon ilishakufa pia sababu mganga wake alifariki currently anakutana na matapeli tu. saiv kaolewa ni mama wa nyumbani.

Duniani kuna mambo 🀣
 
🀣🀣🀣! Wanajua binadamu wote wanapenda vitu vizuri! Be careful na hawa watumishi/nabii.
Ulimwengu wa roho ni zaidi ya tuujuavyo.
kila upande joto la mafanikio ni kali sana, na mchanganyo wa mambo ya Mungu na Giza umefikia kiwango cha juu sana cha hatari ya kuamsha hasira za Mungu πŸ’
 
umeona sasa hapo umeibua hatari nyingine πŸ’

Mganga wake alishakufa 🀣

hivi kumbe ndio chimbuko ka kale ka msemo kwamba wewe umerogwa na mganga wako ameshakufa? kwamba dhiki, mikosi na maisha magumu unayopitia ni kwasabb mganga wako amekufa, dah.....

Tumuamini Mungu Tu asiyebadilika wala Kufa ndugu zangu πŸ’
 
Hizo dawa zipo ila ni hatari sana kumfanyia mtu . Atateseka maisha yake yote kwa kukutumikia wewe tu. Kuna rafiki yangu alifanyiwa madawa sana na mke wake ambaye ni msukuma. Alifika hatua anaumwa sana na asijue anaumwa nini. Akachukuliwa na mjomba wale ni Padri akapelekwa kwa ajili ya maombi. Alitapika vitu vya ajabu sana, mpaka leo mzima na mke wameachana
Kaka yangu alifariki mwaka jana kwa maujinga kama hayo. Mke wake alikufa baada ya kuugua kwa mwezi mmoja. Baada ya kufa , kaka akaanza kuweweseka, anasema kila siku mke wake anakuja usiku anataka waende wote. Akawa kama kachanganyikiwa. Akafanyiwa maombi na akatakiwa afanye jambo la kimila ila akapuuzia. Siku ya 40 ya mkewe akazidiwa, akapelekwa hospital wakamuambia labda ana mawazo. Baada ya siku mbili akaanza kutapika madude meusi meengi mpaka tukashangaa yabatoka wapi. Ndio akakata roho. Kumbe mke wake alishasema nakufa lakini kaka yenu naye atafuata. Na yule mke wake alikuwa na mambo ya ajabu sana lakini kaka alikuwa zezeta kwa mkewe hata aje amelewa chakari. Imagine mtu wa swala tano unaishi na mlevi kupindukia miaka yote hiyo bila hata kuchukua hatua.

Hata madawa sio kabisa jamani. Acha mtu akupende naturally , akiondoka sio wako huyo.
 
dah,
aiseee ni hatari juu ya khatari πŸ’
 
Amen brother amen.
 
Zikiisha sasa...tabu inabaki pale pale
kuna vitu viko wazi kabisa na mtu anaweza akawa na ufahamu na uelewa wa kutosha kwamba faida za jambo hili zinaambatana na utumwa wa masharti magumu na ya fedheha sana, yasiyo kupa amani, Lakini pia manufaa yake ni ya muda tu πŸ’

si afadhali umtegemee Mungu na ufaidike na kufurahia atakachokujaali kwa amani maisha yako yote mpaka siki ya mwishoπŸ’
 
Mimi nina dawa ya kurudisha line zilizopotea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…