Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

yani kiufupi ukisumamrize utaona kwamba mungu anatutafutia tu sababu ili akatuchome moto yani anatuwekea mitego ya kila aina ili watu wamkosee ndio akapate watu wa kuwatesa milele, na kwa kosa gani kubwa ambalo tunaweza fanya wanadamu hadi mungu akasirike kiasi kwamba akatuchome moto milele?
Pia sisi aliyetuumba si ni yeye mwenyewe mana yake kila kitu tunachofanya yeye ndio alivyotuumba tuwe hivyo sasa kwanin atulaumu sisi wakat ni kazi yake yeye mwenyewe, who is responsible hapo?
 
Umenena vyema.
 
Hapa ni blah blah blah blahs tu kila mtu anaandika kile anajua na kwa sababu pumzi anayo ila huwezi kutana na jibu la maana hapa na hilo jibu duniani halijakuwepo na halitokuwepo jibu lipo kwa wale waliokwisha lala mauti so as long as bado unapumua muhimu amini kile unaamin subiri siku na wewe ufe u-taste maisha nje ya hayo uliyopo.

Halafu ni ajabu sana,unaichosha akili yako kwa vitu kama hivi ambavyo obviously huwezi kupata jibu hata kutoka kwa mtu wa aina gani huo muda wa kuwaza haya ungefanya mambo mengine ingekuwa rafiki sana kwa akili yako.
 
asili ya binadamu ni kudadisi na kutaka kujua
 
kama alishindwa kumsamehe Adam na Hawa atashindwaje hili
 
kama alishindwa kumsamehe Adam na Hawa atashindwaje hili
Mbona sisi anataka tusamehe wakat yeye kusamehe hawezi? Eti mtu tu kala tunda kwenye mti ndio imekua ishu kubwa yani kakasirika hatari
 
asili ya binadamu ni kudadisi na kutaka kujua
So tangu umetaka kujua baada ya kifo utaenda wapi ni kwa percent ngapi umejua ukweli wa hilo?

Au umepata wapi taarifa kuna siku atarudi mtu maiti aseme huko kuna moja mbili tatu?unapoteza muda wako kwa mambo kama haya nimekwambia hata babu yako mzaa babu wa babu yako wakati anakufa hakuwa akijua na hatatokea wa kujua hili ktk dunia hii focus kwenye mambo yenye maana acha kuichosha akili yako.
 
Mbona sisi anataka tusamehe wakat yeye kusamehe hawezi? Eti mtu tu kala tunda kwenye mti ndio imekua ishu kubwa yani kakasirika hatari
Tena imeandikwa saheme 7 mara 7
 
sawa usemavyo lakini kwa maana hiyo wewe hujali wala nini na hujawahi jiuliza kuhusu hii kitu itavyokuwa kwako poa tu
 
sawa usemavyo lakini kwa maana hiyo wewe hujali wala nini na hujawahi jiuliza kuhusu hii kitu itavyokuwa kwako poa tu
Kujali najali ila kujiuliza hapana maana asili ya swali mwenzake ni jibu,mf;leo nikiwa na swali la kwamba kwanini kuna wakati network ktk simu zetu inakata au inakuwa legevu?nitaenda kwa wataalam wa IT watanipa jibu niache kuteseka na swali hilo but leo mimi nijiulize kuna nini baada ya kifo jibu lake nitalitolea wapi na umri huu 30+ kweli si nitachakaa?

Mimi ni mtu wa Imani na nazingatia nilichofundishwa kuhusu maisha haya ya duniani na ya baada ya hapa but siyafikirii sana ya ng'ambo kutokana na hata yasipokuwepo sitakuwa na cha kupoteza.
 
nimekupata ila ndiyo asili yetu ilivyo tukiona kitu hakina majibu na hatuwezi pata majibu basi hutafuta namna ya kutojishughulisha nacho utasikia achana nacho hicho kitakupasua kichwa bure
 
Maisha baada ya kifo yapo na huwezi kuyaepuka ni kmaa kifo kilivyo hata usipo amini kama kifo kipo bado tu utakufa na hakuna wa kumzuia malaika wa mauti kuchukua roho ya mwanadamu na hapitishi hata sekunde moja pindi pale mda wa mwanadamu unapoisha.! Kifo kipo na maisha baada ya kifo yapo hapo kaburin .kama ni mtu mwema bustani yako ya peponi inaanzia hapo kaburini na kama ni muovu pia kisanga kinakukuta hapo hapo kaburini.! Sio kama ni vitisho vya masheikh bali ndio uhalisia ulivyo.no doubts kwa hili.! Na mtu kabla roho yake haijatoka anaonyeshwa sehemu anayofikia kama ni moton au peponi.! Kuna watu watakuja kupinga hii comment il kupinga kwao hakuondoi ukweli uliopo

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Asikudanganye mtu, maisha baada kifo yatakuwa sawa kabisa na maisha yalivyokuwa kabla ya kuzaliwa.
 
Mbona sisi anataka tusamehe wakat yeye kusamehe hawezi? Eti mtu tu kala tunda kwenye mti ndio imekua ishu kubwa yani kakasirika hatari
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Hatari Mkuu, japo mi ni muumini Wa Mungu. Ila reason yake haikuwa na justification. Yaani Siku hiyo (kama itakuwepo) akituacha tu argue na kujitetea sijui kama Kuna atakaechomwa.
 
Asikudanganye mtu, maisha baada kifo yatakuwa sawa kabisa na maisha yalivyokuwa kabla ya kuzaliwa.
kwa maana nyingine hamna maisha hapo maana kabla ya kuzaliwa sikuwepo[emoji848][emoji848]
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Hatari Mkuu, japo mi ni muumini Wa Mungu. Ila reason yake haikuwa na justification. Yaani Siku hiyo (kama itakuwepo) akituacha tu argue na kujitetea sijui kama Kuna atakaechomwa.
[emoji23][emoji23]hautopewa hiyo nafasi
 
Mimi ni mwanasayansi ila ni mkristo. Ninapokuwa kwenye sayansi ninareason kisayansi.Ninapokuwa kikristo ninareason kiimani ila sina evidences.
Sasa utakua upande upi endapo dini itakinzana na sayansi, kwa mfano ishu ya flat earth na jua kuzunguka dunia
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1] Hatari Mkuu, japo mi ni muumini Wa Mungu. Ila reason yake haikuwa na justification. Yaani Siku hiyo (kama itakuwepo) akituacha tu argue na kujitetea sijui kama Kuna atakaechomwa.
Na tusipopewa hiyo nafasi itakuwa ni udikteta wa hali ya juu.
 
na jee hiki tunachoamini leo ndicho walichokuwa wana amini wazee wetu mababu zetu asili yetu kabla ya kuja wakoloni barani Africa??
Futa huu ujinga kwenye kichwa chako.
Hata kuabudu mizimu ni kitu tuliletewa, huna historia yoyote unayojua, tulia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…