Ndo unavyojiliwaza hivyo au siyo....Lakini unasahau kabisa kwamba kabla ya hapo wewe HUKUWEPO na HUKUJULIKANA KABISA KAMA UTAKUWEPO ghafla ulishtukia tu UPO na UKAWEPO BILA RIDHAA YAKO,hivi huyo aliyekufanya UWEPO akakutengenezea system za kustaajabisha na zinazoshangaza kama hzo na tena kama ulivyosema zinafanya kazi kwa kushirikiana bila kukosea,na baadhi huwa zinafanya kazi bila ridhaa yako ikiwemo MOYO,yan kazi yote hiyo kubwa aliyoifanya awe amekuleta tu duniani hapa kuja kucheza cheza huku muda unaenda kisha ufe tu na ipitee kizembe zembe iwe imeisha eti asikurudishe tena? Kirahisi rahisi tu....Umeishi muda flan hv kisha huyo Mtengenezaji hizo SYSTEMS akaamua kuzi SHOOT DOWN(kufa) bila wewe kupenda,Hivi HUYO kwa ujuzi mkubwa wa kushangaza kama hivyo ashindwe kweli KUKUWASHA (kuhuisha)ILI UWAKE TENA KWA MFUMO MWINGINE bila ridhaa yako?
Kumbuka wewe ulikuwa HAUPO KABISA na hakuna mtu alikuwa anakutaja,umekuja Duniani kupitia STAREHE walioifanya watu wawili kitandani kati ya mwanamke na mwanaume ambapo wewe ndo unawaita baba mwingine unamwita mama.
Starehe hiyo waliifanya lakin pia walikuwa hawajapanga kabisa na hawajui ndo unakuja wewe...NA HUENDA HATA SIKU ILE MIMBA YAKO INATUNGWA KUNA MMOJA KATI YAO HAKUZIPOKEA VIZURI TAARIFA YA MIMBA YA WEWE KUTUNGWA LKN PIA HUENDA WALILAUMIANA KWANINI WEWE UMETUNGWA ILA KWA VILE SIO RIDHAA YAO NAO WAKAAMUA TU KUPOTEZEA MAANA HAKUNA JINSI, MAMA AKAKUBALI KULEA IMBA YAKO KWA SHIDA AFU NDO UKAJA WEWE LEO AMBAYE SASA HV UPO hapa JF na simu yako UNASEMA HAKUNA KUFA NA HUYO MUNGU HAYUPOOO.umekuja huku ukiwa dhaifu wa mwili na akili unajinyea,unakojoa popote tu unatoka udenda muda wote,lakini BILA RIDHAA YAKO tena unakuwa mtu mzima unafanya mabalaa ya kuyafanya,unaiba,unazini, unatukana watu,unadhurumu KWA RIDHAA YAKO mwisho YULE YULE alikuekuleta Anakuzima tena BILA RIDHAA YAKO,anakupeleka kulee wasiporudi kisha akwambie yote uliyowahi kuyafanya kuanzia unabalekhe/vunja ungo mpk siku ile UNAZIMWA na kisha akutie motoni kwa mabaya au akutie peponi kwa mazuri uliyofanya.
Tuache kujitoa akili ndugu zangu,huyo aliyekuleta hajakuleta tu hivihivi amekuleta kwa mpango maalum na uje utii sheria zake na ufuate kile alichokuamuru ufanye kwa kutumia mfumo sahihi ambao ni dini SAHIHI,dini ya mitume wote walioletwa na Mungu muumbaji.Hujaletwa kuja kupoteza muda na hapa duniani sio mahali pa kuishi alipopanga Mungu,Dunia ni sehemu ya kufanya Utii ili atkaefanya vzr huo utii basi kuna mahali Mungu ndo ameandaa maisha yasiyoisha.
Hebu jiulize kitu kimoja,kama hii dunia ni sehemu ya kuishi kwanini watu wanakufa,kwanini watu wanakufa katika umri wa uchanga,utoto,ujana na utu uzima?
Kama dunia ni kutafuta maisha mbona ukiyapatia hayo maisha pia unakufa?Kwanini ufe?
Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni kwamba YUPO ALIYEKUANZISHA NA KUKULETA DUNIANI KWA MUDA bila ridhaa yako ILI UJE UFANYE MITIHANI (MAJARIBU)kwa ridhaa yako mwenyewe huku akiwa amekupa nyenzo za wewe kufaulu hiyo mitihani,amekupa Muongozo wa vitabu (Zaburi,Torati,Injili na QURAN),pia akakupa Akili,kusikia,kuona,kunusa,kuonja nk,anakupa muda flani,baada ya muda huo flan HUYO HUYO ATAKUFISHA bila ridhaa yako tena NA ATAKURUDISHA TENA KTK UHAI WA AINA NYINGINE bila ridhaa yako pia...kama anavyofanya kwenye mbegu ya mimea yote Duniani...kisha sasa ndo sote tutakutana huko kwenye SIKU YA HUKUMU,siku ambayo kila mtu atabeba alichokipanda kwenye uhai wa Duniani.
Wewe endelea kuuchezea tu muda lakini ipo siku na wewe utapangiwa ratiba na watu kwamba wakakuzike wapi na lini wakati huo wewe upo kwingine kabisa unapambana na hali yako huko.
Hzi pumzi zisituhadae ndg zangu,hakuna watu wanaoendelea kujilaumu hivi sasa kama wale marehemu wetu tuliowazika,Mtu mwema kwa mazuri anayoyaona huko saizi anajilaumu kwanini amefanya mema machache,na mtu mbaya ndo analia na kusaga meno kumuomba Mungu awarudishe kidoogo warudi Duniani kuja kusawazisha yale yote waliyokosea jambo ambalo abadani haliwezekani.