Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Wanadamu wote wa Dini zote wanabebwa na Amri kumi za Mungu hivyo haijalishi watabadili Dini mara ngapi kitakacho safisha roho zao ni Amri kumi za Mungu peke yake yoyote hata asiye na Dini akifata hizo sheria za Amri kumi za Mungu anampendeza Mungu.
 
Ulivyokuja hapa Duniani ulianza au uliendelea na umri ulipotoka nao huko ulipotoka?
Suala la kufa na kuzaliwa vinatofautiana! Wengine wanakufa na umri mdogo na wengine wanakufa wakiwa wazee kabisa tena wanakuwa wameshamaliza nguvu zote! Hawa hawawezi kuwa sawa na wanaokufa na umri wa ujana au watoto!
 
Suala la kufa na kuzaliwa vinatofautiana! Wengine wanakufa na umri mdogo na wengine wanakufa wakiwa wazee kabisa tena wanakuwa wameshamaliza nguvu zote! Hawa hawawezi kuwa sawa na wanaokufa na umri wa ujana au watoto!



Wapo Sawa hao😀😀😀

Labda kimwili lakini kiroho hawana tofauti

Roho haina umri😀😀😀
 
Nadharia ni moja tu mkuu kwamba KUFA KUPO NA TUTAFUFULIWA ILI MFUFUAJI ATUONYESHE YOTE TULIYOYAFANYA NA ATUINGIZE PEPONI AU MOTONI kulingana na matendo yetu.
Hao wenye nadhalia ya kisayansi wanashindwa nini sasa kuzuia huko KUFA?

Ila hukunisoma vyema mkuu.

Nimekazia kuwa ni vyote sayansi na dini zinagongelea pale pale kwenye uwepo wa maisha baada ya kifo.
 
Naona wengi wetu humu tunahoji haya mambo kimasihara zaidi,lakini niseme tu kwa sababu organs zetu ziko normal tunatembea na tunapumua afya iko vzr tunafurahi Lakini kwa hakika ni kwamba KUZUNGUMZIA KIFO NI JAMBO MOJA NA KUKIKARIBIA KIFO NI JAMBO JINGINE NA KUFA KWENYEWE NI JAMBO JINGINE KABISA..nikupe idea moja hv kama unataka kuyaamini haya mambo ya baada ya kufa.

Mfano 1:
Kumbuka siku ambayo ulilala na mwenzio kitandani kisha usiku ukaanza KUOTA unakimbizwa na simba,wakati wewe unajitahidi kupambana unakimbia huku na huko,unaruka mdimbwi unaruka visiki unakimbia maporini ili simba asikukamate,wakati ndoto inaendela wewe presha ipo juu unaona kabisa hapa nitakamatwa nitaliwa na simba,Wakati Simba anakukmbiza huku upande wa pili wa mwenzio ANAKUONA WEWE UMELALA NA UMEJIFUNIKA SHUKA UNAKOROMA hajui chochote unachopitia kwa muda huo,lakini wewe kiuhalisia upp kwenye MAPAMBANO MAZITO ili ujinasue kuliwa na Simba na wala huna habari kabisa kwamba UPO NYUMBANI KWAKO NA UMELALA KITANDANI NA MWENZIO.
huu ndiyo mfano wa mteso anayoyapata ROHO ya mtenda maovu akiwa amekufa.

Mfano 2:
Kwa wanaume mtanielewa zaidi,
Hebu vuta picha siku ile ulipolala kitandani pekeako afu usiku ukaanza kuota upo bar umemtongoza demu kisha mkaenda sehemu hivi kustarehe sana tu mkala na kunywa sana tu na mwisho mkaenda sehemu hv kufanya ngono,umefanya ngono na msichana huyo mpaka ukafika kileleni kisha baadae unashtuka unaamka na boxer pia imeshaloa.....Hivi kwenye hzo starehe zote ulizofanya unadhani ni kweli KIMWILI ulikuwepo hayo maeneo na huyo binti?
Huu ndiyo mfano wa mtu mwema anavyopata starehe akiwa upande wa pili wa uhai huu wa Dunia(akifa)
 
Hyo law of nature inasababishwa na nn au Nani? Kwan wanaotenda maovu wote wameadhibiwa hapahapa kabla ya kufa?
 
Hyo law of nature inasababishwa na nn au Nani? Kwan wanaotenda maovu wote wameadhibiwa hapahapa kabla ya kufa?
Sijui anaesababisha ni nani,nature haina adhabu zote kusema kuwe na haki ya asilimia mia na inategemea maouvu hayo kuna maovu ya kutendeana sisi kwa sisi hayo tutaamua kwa utashi wetu.

Unahitaji kuwa na upana wa fikra kunielewa nachoandika.
 
Mimi nimeuliza swali kulingana na hoja yako ambayo katika history ilishawahi kutolea na mwana philosopher Pascal wager
"Ni heri kuamini Mungu yupo ili ata kama ukifa na usipate nafasi ya kukutana nae fresh tu inakua imeisha iyo.
Kuliko usiamini Mungu yupo then ukafa ukaenda kumkuta yupo."


Logic ya pascal wager iko hapa

1. Kama hakuna Mungu, basi kuamini Mungu yupo hakutakuwa na madhara kwako
2. Kama Mungu yupo, basi kuamini Mungu yupo kutakupa faida ya wewe kuweza kuingia peponi

Nikirejea hoja yako

Kwamba wewe unaona sahihi kuamini Mungu hata kama ikitokea ukafa na usimkute haitakupunguzia chochote kuliko ukafanya kiburi na mwisho wa siku ukamkuta

Lakini vipi kama ukiambiwa na mtu mwingine tofauti na dini yako kwamba Mungu wa dini yake ndio wa ukweli na hivyo unapaswa kumuamini na kumuacha huyo Mungu wa uongo unayemuabudu maana hautapungukiwa kitu kuliko ukampuuza na ukaendelea kuamimi Mungu wako ambaye ni potofu na mwisho wa siku ukaja ukakutana na Mungu wa kweli ambaye ulimpuuza?

Swali langu liko hapa

Je utakubali kuhama dini yako na kuanza kumuabudu huyo Mungu wa dini hiyo nyingine ulitambulishwa na mtu huyo ili usalimike siku ya mwisho?

David Mitchell alishawahi kui flip hiyo hoja ya pascal wager akauliza vipi kama peponi ni sehemu ambayo wanaruhusiwa kuingia atheist peke yao

Hivi ndivyo itakavyokua

1. Kama hakuna Mungu, basi kutomuamini hakutaweza kukudhuru
2. Kama Mungu yupo, kutokumuamini kutakupa faida wewe kama atheist uweze kuingia peponi

Kwa hiyo ukitumia logic hiyo hiyo utajua tena kumbe haupaswi kuamini Mungu
 
Wanadamu wote wa Dini zote wanabebwa na Amri kumi za Mungu hivyo haijalishi watabadili Dini mara ngapi kitakacho safisha roho zao ni Amri kumi za Mungu peke yake yoyote hata asiye na Dini akifata hizo sheria za Amri kumi za Mungu anampendeza Mungu.
Sio kweli kama ambavyo wewe unataka kuaminisha UMMA ionekane yeyote anayefata amri kumi za Mungu basi anampendeza Mungu na anaweza kuiona pepo

Ushoga upo kwenye makatazo ya amri kumi za Mungu?

Mtu akiwa anafata amri za Mungu zote kumi halafu akawa anajihusisha na ushoga, atakuwa anampendeza Mungu?
 
Ufunuo wa Yohana 21:1 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena.
 
Tenda mema ili kama Mungu yupo uwe na uzima wa milele kama hayupo pia hauna cha kupoteza.
 
Ukipekua pekua sana inasemekana nasema inasemekana kwa sababu sijawahi shuhudia kuna watu wana uwezo wa kutoka kwenye miili yao na kurudi tena kwa maana hiyo huu mwili ndiyo utaoza na kuwa udongo tena ila roho itaishi sasa inaishi vipi na wapi

Ongezea na ubongo
Yap,ubongo ukikosa oxygen ndo neurons zinakufa na hakuna ufahamu tena. Mifumo ya fahamu yote inacease.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…