Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Hivi ni kweli kuna maisha baada ya kifo?

Mtu akifa roho yake kama imetenda mema itaenda kwa aliyeiumba na kama imetenda adhabu kubwa itaenda motoni.Na kama imetenda dhambi za kawaida katika ubinadamu wake itaenda kulipia dhambi hizo na ikimaliza itaungana na Muumba(Mungu ni Mtakatifu hivyo huwezi kwenda kwake ilhali bado unadhambi hata kama ni ndogo inapaswa uwe mwenye moyo safi)
una udhibitisho wa hili
 
Ndo unavyojiliwaza hivyo au siyo....Lakini unasahau kabla ya hapo wewe HUKUWEPO na HUKUJULIKANA KABISA KAMA UTAKUWEPO ghafla UKAWEPO BILA RIDHAA YAKO,hivi huyo aliyekufanya UWEPO akakutengenezea system ghali na kubwa kama hzo na tena kama ulivyosema zinafanya kazi kwa kushirikiana,yan kazi yote hiyo kubwa aliyoifanya kisha ufe tu upitee kizembe zembe asikurudishe tena? Umeishi muda flan kisha hizo SYSTEMS akazi SHOOT DOWN(kufa) bila wewe kupenda,Hivi huyo atashindwa kweli KUKUWASHA ILI UWAKE TENA KWA MFUMO MWINGINE bila ridhaa yako?
Kumbuka wewe ulikuwa HAUPO KABISA,umekuja Duniani kupitia STAREHE walioifanya watu wawili mwanmke na mwanaume amabo wewe ndo unawaita WAZAZI wangu,Starehe hiyo waliifanya lakin pia walikuwa hawajui ndo unakuja wewe...
Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni kwamba YUPO ALIYEKUANZISHA NA HUYO HUYO ATAKUFISHA NA ATAKURUDISHA TENA KTK UHAI WA AINA NYINGINE...kama anavyofanya kwenye mbegu ya mimea
Mia fil mia.
 
QURAN 22: 1- 2

"Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi. Hakika tetemeko la Saa (ya Kiyama) ni jambo kuu. Siku mtapo iona, kila mwenye kunyonyesha atamsahau amnyonyeshaye, na kila mwenye mimba ataharibu mimba yake. Na utaona watu wamelewa, na kumbe hawakulewa. Lakini adhabu ya Mwenyezi Mungu ni kali. "






 
Sio kweli kama ambavyo wewe unataka kuaminisha UMMA ionekane yeyote anayefata amri kumi za Mungu basi anampendeza Mungu na anaweza kuiona pepo

Ushoga upo kwenye makatazo ya amri kumi za Mungu?

Mtu akiwa anafata amri za Mungu zote kumi halafu akawa anajihusisha na ushoga, atakuwa anampendeza Mungu?
sodoma na gomora walipatiwa tiba
 
Ndio maisha baada ya kifo yapo.
Kama.
Kama uliweza kutoka kwenye shahaaa za baba yako.
Ukiwa sio kitu.
Basi hata maisha ya baada ya kifo yanawezekana.
Tena huko nu Raha kwa wacha mungu na Maisha kwa watu waovu.
Mungu atuepushe na hao watu waovu
 
lakini hapa nina sitofahamu pia kama kuna maisha baada ya kifo kwa nini Jesus alipaa na kuelekea huko mbinguni kwenye hayo maisha na mwili wake??
 
QURAN 35: 36-37

"Na walio kufuru watakuwa na Moto wa Jahanamu, hawahukumiwi kufa, wala hawatapunguziwa adhabu yake. Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kuzidi ukafiri. Na humo watapiga makelele: Mola wetu Mlezi! Tutoe (uturudishe tena duniani) tufanye mema sio yale tuliyo kuwa tukiyafanya. (Wataambiwa) Kwani hatukukupeni umri wa kutosha akukumbuka mwenye kukumbuka? Na akakujieni Mwonyaji? Basi onjeni (adhabu)! Kwani walio dhulumu hawana wa kuwanusuru. "


 
Habari za humu wadau wa JF!!!! Ni ukweli usiopinga kuwa kuna maisha baada ya kifo(life after death) na kuna maisha upande wa pili wa kifo(The other side of death),wanasaikolojia||wanaphilosophia||na wanatheologia wamefanya tafiti za muda mrefu kwenye maeneo hayo!!! Ukweli ni kwamba sisi sio miili yetu na uhakika wa kifo ni asilia kabisa kwenye miili hii inayoharibika(physical bodies),na ndio maana wale wanaoishi kisawasawa ni wale wanaolewa na kujua vyema kuwa ipo siku WATAONDOKA KWENYE MIILI HIYO iliyo na mipaka ya muda[emoji848]!!!! Naomba kuwasilisha mawazo yangu kwenu...
Ahsanteni
 
QURAN 7 : 44-45

"Na watu wa Peponi watawaita watu wa Motoni (na kuwaambia): Sisi tumekuta aliyo tuahidi Mola wetu Mlezi kuwa ni kweli. Je, na nyinyi pia mumekuta aliyo kuahidini Mola wenu Mlezi kuwa ni kweli? Watasema: Ndiyo! Basi mtangazaji atawatangazia: Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu. Wale ambao walikuwa wakizuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wakataka kuipotosha, nao wanaikanusha siku ya mwisho. "
 
Habari wanazengo...
Leo ningependa kufahamu au kujua kile unachoamini wewe kama wewe tulivyoumbwa kila mmoja amepewa utashi ukiwa na lengo la kupambanua mambo, tuachane kwanza na hizi imani ambazo tunazoamini au kuaminishwa.

Hivi ulishawahi kujiuliza baada ya kufa nini kinaendelea, kuna maisha baada ya kufa au ndiyo ukifa umekufa mazima!
1Wakorintho 15

Ufufuo Wa Wafu

12Basi kama tumehubiri ya kwamba Kristo alifufuliwa kutoka kwa wafu, mbona baadhi yenu mnasema hakuna ufufuo wa wafu? 13Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo hakufufuliwa. 14Tena ikiwa Kristo hakufufuliwa kutoka kwa wafu, kuhubiri kwetu kumekuwa ni bure na imani yenu ni batili. 15Zaidi ya hayo, twaonekana kuwa mashahidi wa uongo kuhusu Mungu, kwa sababu tumeshuhudia kumhusu Mungu kwamba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu, lakini hilo haliwezi kuwa kweli kama wafu hawafufuliwi. 16Kwa kuwa kama wafu hawafufuliwi, basi hata Kristo hajafufuka. 17Tena kama Kristo hajafufuliwa, imani yenu ni batili; nanyi bado mko katika dhambi zenu. 18Hivyo basi, wote waliolala katika Kristo wamepotea. 19Ikiwa tumaini letu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wote.

20Lakini kweli Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, tunda la kwanza la wale wote waliolala. 21Kwa maana kama vile mauti ilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. 22Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai. 23Lakini kila mmoja kwa wakati wake: Kristo, tunda la kwanza kisha, wale walio wake, wakati atakapokuja. 24Ndipo mwisho utafika, wakati atakapomkabidhi Mungu Baba ufalme, akiisha angamiza kila utawala na kila mamlaka na nguvu. 25Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake. 26Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti. 27Kwa maana Mungu “ameweka vitu vyote chini ya miguu yake.” Lakini isemapo kwamba “vitu vyote” vimewekwa chini yake, ni wazi kwamba Mungu aliyetiisha vitu vyote chini ya Kristo hayumo miongoni mwa hivyo vilivyotiishwa. 28Atakapokuwa amekwisha kuyafanya haya, ndipo Mwana mwenyewe atatiishwa chini yake yeye aliyetiisha vitu vyote, ili Mungu awe yote katika yote.

29Basi kama hakuna ufufuo, watafanyaje wale wabatizwao kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kamwe, mbona watu wanabatizwa kwa ajili yao? 30Nasi kwa upande wetu kwa nini tunajihatarisha kila saa? 31Kama majivuno yangu kwa ajili yenu katika Kristo Yesu Bwana wetu ni kweli, ndugu zangu, ninakufa kila siku. 32Kama kwa sababu za kibinadamu tu nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, ningekuwa nimepata faida gani? Kama wafu hawafufuliwi,

“Tuleni na kunywa,

kwa kuwa kesho tutakufa.”

33Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.” 34Zindukeni mwe na akili kama iwapasavyo, wala msitende dhambi tena; kwa maana watu wengine hawamjui Mungu. Nasema mambo haya ili mwone aibu.

Mwili Wa Ufufuo

35Lakini mtu anaweza kuuliza, “Wafu wafufuliwaje? Watakuwa na mwili wa namna gani?” 36Ninyi wapumbavu kiasi gani? Mpandacho hakiwi hai kama hakikufa. 37Mpandapo, hampandi mwili ule utakao kuwa, bali mwapanda mbegu tu, pengine ya ngano au ya kitu kingine. 38Lakini Mungu huipa mbegu umbo kama alivyokusudia mwenyewe na kila aina ya mbegu huipa umbo lake. 39Kwa maana nyama zote si za aina moja. Binadamu wana nyama ya aina moja, wanyama wana aina nyingine, kadhalika ndege na samaki wana nyama tofauti. 40Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani, lakini fahari wa ile miili ya mbinguni ni wa aina moja na fahari wa ile miili ya duniani ni wa aina nyingine. 41Jua lina fahari ya aina moja, mwezi nao una fahari yake na nyota pia, nazo nyota hutofautiana katika fahari.

42Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati wa ufufuo wa wafu. Ule mwili wa kuharibika uliopandwa, utafufuliwa usioharibika, 43unapandwa katika aibu, unafufuliwa katika utukufu, unapandwa katika udhaifu, unafufuliwa katika nguvu, 44unapandwa mwili wa asili, unafufuliwa mwili wa kiroho.

Kama kuna mwili wa asili, basi kuna mwili wa kiroho pia. 45Kwa hiyo imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika kiumbe hai”; Adamu wa mwisho, yeye ni roho iletayo uzima. 46Lakini si ule wa kiroho uliotangulia, bali ni ule wa asili, kisha ule wa kiroho. 47Mtu wa kwanza aliumbwa kwa mavumbi ya ardhini, mtu wa pili alitoka mbinguni. 48Kama vile alivyokuwa yule wa ardhini, ndivyo walivyo wale walio wa ardhini; na kwa vile alivyo mtu yule aliyetoka mbinguni, ndivyo walivyo wale walio wa mbinguni. 49Kama vile tulivyochukua mfano wa mtu wa ardhini, ndivyo tutakavyochukua mfano wa yule mtu aliyetoka mbinguni.

50Ndugu zangu nisemalo ni hili: nyama na damu haviwezi kuurithi ufalme wa Mungu, wala kuharibika kurithi kutokuharibika. 51Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa 52ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa. 53Kwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa. 54Kwa hiyo, mwili huu wa kuharibika utakapovaa kutokuharibika, nao huu mwili wa kufa utakapovaa kutokufa, ndipo lile neno lililoandikwa litakapotimia: “Mauti imemezwa kwa kushinda.”

55“Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako?

Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?”

56Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. 57Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.

58Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure.
 

"Does man think that We cannot assemble his bones? Nay, We are able to put together in perfect order, the very tip of his fingers." (Surah Qiyamah)​


Mwanadamu usipumbazwe na maisha mafupi ya dunuani yakupita tu

Mche M/mungu. Adhabu zake zinatisha

Over

Screenshot_20211228-152314.png
 
QURAN 39 : 68-70

"Na litapulizwa barugumu, wazimie waliomo mbinguni na waliomo katika ardhi, isipo kuwa aliye mtaka Mwenyezi Mungu. Kisha litapulizwa mara nyengine. Hapo watainuka wawe wanangojea. Na ardhi itang'ara kwa Nuru ya Mola wake Mlezi, na Kitabu kitawekwa, na wataletwa Manabii na mashahidi, na patahukumiwa kati yao kwa haki, wala hawatadhulumiwa. Na kila nafsi italipwa kwa yale iliyo yafanya, na Yeye anayajua sana wanayo yatenda."


QURAN 39: 71: 72

" Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahanamu makundi kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: La! (walikuja, lakini sisi tuliwakataa) Na limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri.(waliowakataa mitume) Itasemwa: Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Basi ni ubaya ulioje wa makaazi ya wanao jivuna! "
 
Habari wanazengo...
Leo ningependa kufahamu au kujua kile unachoamini wewe kama wewe tulivyoumbwa kila mmoja amepewa utashi ukiwa na lengo la kupambanua mambo, tuachane kwanza na hizi imani ambazo tunazoamini au kuaminishwa.

Hivi ulishawahi kujiuliza baada ya kufa nini kinaendelea, kuna maisha baada ya kufa au ndiyo ukifa umekufa mazima!
Jaribu kufa utatupa mrejesho

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Habari za humu wadau wa JF!!!! Ni ukweli usiopinga kuwa kuna maisha baada ya kifo(life after death) na kuna maisha upande wa pili wa kifo(The other side of death),wanasaikolojia||wanaphilosophia||na wanatheologia wamefanya tafiti za muda mrefu kwenye maeneo hayo!!! Ukweli ni kwamba sisi sio miili yetu na uhakika wa kifo ni asilia kabisa kwenye miili hii inayoharibika(physical bodies),na ndio maana wale wanaoishi kisawasawa ni wale wanaolewa na kujua vyema kuwa ipo siku WATAONDOKA KWENYE MIILI HIYO iliyo na mipaka ya muda[emoji848]!!!! Naomba kuwasilisha mawazo yangu kwenu...
Ahsanteni
sasa hii after death inakuwaje ukifika huko unaanza upya ama kwa mfano huku si mtu unafamilia so mkikutana huko munaliendeleza ama kila mtu na kona yake
 
Ndo unavyojiliwaza hivyo au siyo....Lakini unasahau kabla ya hapo wewe HUKUWEPO na HUKUJULIKANA KABISA KAMA UTAKUWEPO ghafla UKAWEPO BILA RIDHAA YAKO,hivi huyo aliyekufanya UWEPO akakutengenezea system ghali na kubwa kama hzo na tena kama ulivyosema zinafanya kazi kwa kushirikiana,yan kazi yote hiyo kubwa aliyoifanya kisha ufe tu upitee kizembe zembe asikurudishe tena? Umeishi muda flan kisha hizo SYSTEMS akazi SHOOT DOWN(kufa) bila wewe kupenda,Hivi huyo atashindwa kweli KUKUWASHA ILI UWAKE TENA KWA MFUMO MWINGINE bila ridhaa yako?
Kumbuka wewe ulikuwa HAUPO KABISA,umekuja Duniani kupitia STAREHE walioifanya watu wawili mwanmke na mwanaume amabo wewe ndo unawaita WAZAZI wangu,Starehe hiyo waliifanya lakin pia walikuwa hawajui ndo unakuja wewe...
Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni kwamba YUPO ALIYEKUANZISHA NA HUYO HUYO ATAKUFISHA NA ATAKURUDISHA TENA KTK UHAI WA AINA NYINGINE...kama anavyofanya kwenye mbegu ya mimea
Hizi ndio hoja za kujadili sasa.

Ajabu sana ukifuatilia historia ya binadamu tokea manii inakimbilia yai la mama utaona kuwa ni process iso na mwisho..
 
Back
Top Bottom