Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivo utasoma story kupoteza muda tu. Hamna kitu humo. Hiyo utasoma kama adventureNi mwendo wa kuwasoma wauza madawa ya kulevya jinsi walivyo na ujasiri halafu nitumie ujasiri huo kwenye mishe za halali
Power of the Dog
The Cartel
The Border
Savages
Gentlemen's hour
Mkuu me nadhani kinachombadilisha mtu kupitia vitabu vya imani ni Imani anayoijenga wakati anasoma vile vitabu, na mafundisho ya kuamua. Yaani anasoma kitu huku anakihisi.Ndiyo ni kweli, mfano biblia na quran zimebadiri wasomaji wengi wamekuwa vilaza na mazombi yasiyotaka kutumia akili zaidi ya hisia zinazotokana na vitisho vya hivyo vitabu.
Kitu unachokiona,unachokisoma, kukitazama ndicho unachoulisha ubongo wako, usitegemee akili yako itabaki kuwa empty kwa vitu unavyovisoma, lazima kuna baadhi ya vitu vitaingia akilini mwako na baadae vitakuwa sehemu ya maisha yako.
Ndiomaana mnasisitizwa kusoma sana vitabu vyenye mambo chanya ili kujenga akili zenu ktk mambo chanya yenye maendeleo kwenu na taifa kwa ujumla.
Maandiko yana siri kubwa, ndiomaana wakoloni walitumia elimu bandia kupitia maandiko ya vitabu kututawala na stori za uongo za vitabu vya kidini kutukalilisha ili akili zetu zisifikiri tena mambo ya msingi zaidi zaidi tubaki ktk vifungo vya hayo maandiko yao ya uongo(dini&elimu).
Mfano mzuri tizama wasomi wengi wa kidini akili zao ni hovyo hawana tena ile hali ya uelewa na tafakari ya mambo sensetive zaidi zaidi wamejawa na hofu&fikra chafu zitokanayo na hizo stori za maandiko yao, bila kuwasahau hawa maprofesa wetu vilaza hawa tunaowaona kuwa wamesoma sana hiyo elimu tuliyoletewa, matatizo makubwa na shida kubwa hapa nchini chanzo ni wao.
Rushwa wao, wizi wa mali za umma wao, ubinafsi wao, kusariti nchi yao wenyewe kupitia saini za mikataba ya kishenzi ni wao wenyewe, yaani hata ubunifu wa vitu vidogo walivyosomea darasani hawana kabisa zaidi ya kuwa mzigo kwa taifa kulipa mishahara watu wasio na tija.
Hivyo basi maandiko yana nguvu kubwa ya kumbadirisha mtu mindset yake na utu wake jinsi ya kuenenda kivipi na kuact vipi ktk jamii.
Tusome maandiko yaliyo bora ili tujikinge na shambulio la ukilaza na ukichaa wa masomo bandia.
Namna ya kuwa tajiri chap kwa haraka am sure hujaiona hii kopi ya kiswahiliWakuu habari,
Kwanini watu waliowahi kufanya makubwa hawakufanikisha hayo kupitia kusoma vitabu.
Unakuta mtu anasoma kitabu cha How to influence people lakini hadi anakimaliza hana influence yoyote.
Mtu anaandika kitabu cha how to get rich fast afu pesa ya kuchapisha hicho kitabu amekopa.
Kiufupi nawaza hivi , huenda watu wengi wanaopenda kusoma vitabu huwa ni kwa lengo la kujifariji tu.
Ila mwalimu mzuri wa maisha yako ni uzoefu wako mwenyewe.
Kusoma vitabu ni sawa na kujaribu kujifunza kupitia maisha ya watu wengine huku ukijua maisha ya mwanadamu hayajirudii.
Kitabu kimewahi kubadilisha maisha yako kwa kiasi gani.
Mzee wa ukinipa ngumi ya jicho ukiniuliza Naonaje nami nakupiga ngumi ya sikio Nakuuliza unajisikiaje hahah,, hapana sio mimi chiefWewe sio fiq q kweli 😂
Nimeipenda hiiUnapokishika kitabu kimoja mkononi, haijalishi kina kurasa ngapi, tambua kwamba umeshika kazi iliyofanyiwa utafiti wa muda mrefu. Hakuna mtu anaandika kitabu bila utafiti, hivyo unaposoma kitabu kimoja ni sawa utasoma utafiti wa mtaalam fulani mwenye fani fulani. Ni sawa uko darasani unamsikiliza mhadhiri wa chuo kikuu akikupa madini kuhusu mada au somo fulani. Maana yake ni kwamba ukiweza kumudu kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi ni vitabu 12 kwa mwaka, ni sawasawa na kukaa darasani na kuwasikiliza wataalam 12 wakikupa nondo mmoja baada ya mwingine. Ukijenga hiyo tabia ya kusoma kila mwezi kwa miaka mitano, maana yake utakuwa umekutana na kuwasikiliza wataalamu sitini (60) ndani ya miaka mitano. Ukiamua kwamba hii ndio iwe tabia yako maisha yako yote, ina maana katika maisha yako umezungukwa na wataalam wa fani zote, utakuwa ni mtu mwenye maudhui na maarifa mengi. Mtu yeyote ambaye hana tabia ya kusoma vitabu ni sawa sawa na mtu 'aliyeacha kuishi', ni sawa na mtu aliyekufa - lakini anatembea.
Baadhi ya faida azipatazo mtu mwenye tabia ya usomaji wa vitabu;
Watanzania walio wengi, hata baadhi ya viongozi hawana tabia ya usomaji wa vitabu na matokeo yake wengi wanatia huruma, hawana maudhui, hawana hoja, hawana uwezo wa kuunga ama kupinga hoja fulani, wanatumia nguvu nyingi, makelele, mashambulizi binafsi, ubabe badala ya kujenga hoja. Yote haya ni matokeo ya ukosefu wa tabia ya kusoma vitabu.
- Kujenga uwezo wa kufikiri kwa kina (Critical thinking), hivyo hufanya maamuzi bila kukurupuka, maamuzi yaliyofanyiwa tafakuri jadidi.
- Kujenga maudhui (Content) ya kutosha, hata kwenye mazungumzo au mabishano, mtu mwenye tabia ya kusoma vitabu huzungumza kwa staha, kwa hoja, kwa sauti yenye utulivu, bila kupayuka. Kukwepa hoja ya msingi iliyopo mezani, kumshambulia mtoa hoja badala ya kutoa hoja, kupiga makelele ni dalili za watu wasio na tabia ya usomaji vitabu. Ukikaa kwenye mazungumzo au mabishano unaweza kuona kwa uwazi kabisa nani ni msomaji wa vitabu na nani si msomaji.
- Huboresha afya ya akili, kuimarisha kumbukumbu, ubunifu na ufanisi katika shughuli za kila siku. Hata viongozi wengi wazuri ni wasomaji wazuri wa vitabu.
- Ni namna nzuri ya kutumia muda wako vizuri, kujiliwaza, kujifariji, kujitia moyo, kuepuka msongo wa mawazo, na kukuepusha kutumia muda vibaya na kujihusisha na tabia mbaya kama vile ulevi, uvivu, uzinzi, sigara ina maana utaweza kutumia muda wako vizuri na hivyo kuboresha maisha yako.
EWE NDUGU ANZA TABIA YA USOMAJI WA VITABU SASA
Hapa ndipo tatizo huanzia..Ukishasoma yafanyie kazi uliyosoma...
Mkuu,Ni kweli kwamba Kitabu ni kitabu na maisha ni maisha.Ila Kusoma kunakusaidia kupanua upeo wako.Sasa ule upeo wako jinsi unavyoutumia inaweza kuwa tofauti.Kwa mfano kunaweza kuwa na kitabu cha muongozo wa kilimo Bora.Wakapewa Wakulima Watatu.Wa kwanza akaamua kwamba Hasomi kitabu atalima na kujifunza humo humo mpaka kieleweke.Wa pili akasoma lakini akaamua kutokufuata yaliyomo humo na wa tatu akaamua kusoma na kufanyia kazi yale anayofundishwa.Unafikiri yupi hapo anayo nafasi ya kufanikiwa?Wakuu habari,
Kwanini watu waliowahi kufanya makubwa hawakufanikisha hayo kupitia kusoma vitabu.
Unakuta mtu anasoma kitabu cha How to influence people lakini hadi anakimaliza hana influence yoyote.
Mtu anaandika kitabu cha how to get rich fast afu pesa ya kuchapisha hicho kitabu amekopa.
Kiufupi nawaza hivi , huenda watu wengi wanaopenda kusoma vitabu huwa ni kwa lengo la kujifariji tu.
Ila mwalimu mzuri wa maisha yako ni uzoefu wako mwenyewe.
Kusoma vitabu ni sawa na kujaribu kujifunza kupitia maisha ya watu wengine huku ukijua maisha ya mwanadamu hayajirudii.
Kitabu kimewahi kubadilisha maisha yako kwa kiasi gani.