Hivi ni kweli kusoma vitabu kunaweza kubadilisha maisha ya mtu? una ushahidi wowote?

Hivi ni kweli kusoma vitabu kunaweza kubadilisha maisha ya mtu? una ushahidi wowote?

Vitabu vinabadilisha jinsi unavyofikiri , ukishabadilisha jinsi unavyofikri lazima utende kwa utofauti kulingana na yale uliyoyasoma na matokea pia hutokea kulingana na fikra zetu , mfano mzuri hizi imani za kidini kila mtu anasoma kitabu cha dini yake na ana act tofauti na mwenzake kulingana na alichokisoma.
 
Unapokishika kitabu kimoja mkononi, haijalishi kina kurasa ngapi, tambua kwamba umeshika kazi iliyofanyiwa utafiti wa muda mrefu. Hakuna mtu anaandika kitabu bila utafiti, hivyo unaposoma kitabu kimoja ni sawa utasoma utafiti wa mtaalam fulani mwenye fani fulani. Ni sawa uko darasani unamsikiliza mhadhiri wa chuo kikuu akikupa madini kuhusu mada au somo fulani. Maana yake ni kwamba ukiweza kumudu kusoma angalau kitabu kimoja kila mwezi ni vitabu 12 kwa mwaka, ni sawasawa na kukaa darasani na kuwasikiliza wataalam 12 wakikupa nondo mmoja baada ya mwingine. Ukijenga hiyo tabia ya kusoma kila mwezi kwa miaka mitano, maana yake utakuwa umekutana na kuwasikiliza wataalamu sitini (60) ndani ya miaka mitano. Ukiamua kwamba hii ndio iwe tabia yako maisha yako yote, ina maana katika maisha yako umezungukwa na wataalam wa fani zote, utakuwa ni mtu mwenye maudhui na maarifa mengi. Mtu yeyote ambaye hana tabia ya kusoma vitabu ni sawa sawa na mtu 'aliyeacha kuishi', ni sawa na mtu aliyekufa - lakini anatembea.

Baadhi ya faida azipatazo mtu mwenye tabia ya usomaji wa vitabu;
  • Kujenga uwezo wa kufikiri kwa kina (Critical thinking), hivyo hufanya maamuzi bila kukurupuka, maamuzi yaliyofanyiwa tafakuri jadidi.
  • Kujenga maudhui (Content) ya kutosha, hata kwenye mazungumzo au mabishano, mtu mwenye tabia ya kusoma vitabu huzungumza kwa staha, kwa hoja, kwa sauti yenye utulivu, bila kupayuka. Kukwepa hoja ya msingi iliyopo mezani, kumshambulia mtoa hoja badala ya kutoa hoja, kupiga makelele ni dalili za watu wasio na tabia ya usomaji vitabu. Ukikaa kwenye mazungumzo au mabishano unaweza kuona kwa uwazi kabisa nani ni msomaji wa vitabu na nani si msomaji.
  • Huboresha afya ya akili, kuimarisha kumbukumbu, ubunifu na ufanisi katika shughuli za kila siku. Hata viongozi wengi wazuri ni wasomaji wazuri wa vitabu.
  • Ni namna nzuri ya kutumia muda wako vizuri, kujiliwaza, kujifariji, kujitia moyo, kuepuka msongo wa mawazo, na kukuepusha kutumia muda vibaya na kujihusisha na tabia mbaya kama vile ulevi, uvivu, uzinzi, sigara ina maana utaweza kutumia muda wako vizuri na hivyo kuboresha maisha yako.
Watanzania walio wengi, hata baadhi ya viongozi hawana tabia ya usomaji wa vitabu na matokeo yake wengi wanatia huruma, hawana maudhui, hawana hoja, hawana uwezo wa kuunga ama kupinga hoja fulani, wanatumia nguvu nyingi, makelele, mashambulizi binafsi, ubabe badala ya kujenga hoja. Yote haya ni matokeo ya ukosefu wa tabia ya kusoma vitabu.

EWE NDUGU ANZA TABIA YA USOMAJI WA VITABU SASA
Hakika umeniongezea maarifa pia.

(Kila siku najitahidi kusoma kitabu). Nilianza na how not to die cha Fredrick grager,nikafata mashimo ya mfalme suleiman, nikasoma think again cha adam grant, nikafata cha Eat that Frog cha brian Tracy, secret living of Baba Sega's wives cha Rola, nasasa nasoma Think and grow wealthy,

Kiufupi hivi vitabu vimenibadirisha sna katika mitizamo awali nasasa baada ya. Nimejifunza mengi katik saikolojia, chakula , ushauri wa kuongeza kipato na athari za mitizamo hasi na chanya katika mambo mbalimbali.

Vimeniongeza katika kujiamini, kutazama mbele na major focus, vimenisaidia kujitenga na makundi yasio mazuri kwangu, matumizi mazuri ya muda, na namna ya kuishi na aina za watu maishani.

Niseme wazi kua: vitabu ni mwalimu mzuri zaidi na zaidi baaday ya mwalimu uliekutana nae darasani. Mengi na ziada unayapata kwa kusoma kuliko ulio fundishwa. Ni wewe sasa kuishi katika kujifunza " elimu haina mwisho" darasani hakutoshi wewe kupata maarifa pekee.
 
Kitabu kinaitwaje
Soma huu uzi
 
Wakuu habari,

Kwanini watu waliowahi kufanya makubwa hawakufanikisha hayo kupitia kusoma vitabu.

Unakuta mtu anasoma kitabu cha How to influence people lakini hadi anakimaliza hana influence yoyote.

Mtu anaandika kitabu cha how to get rich fast afu pesa ya kuchapisha hicho kitabu amekopa.

Kiufupi nawaza hivi , huenda watu wengi wanaopenda kusoma vitabu huwa ni kwa lengo la kujifariji tu.

Ila mwalimu mzuri wa maisha yako ni uzoefu wako mwenyewe.

Kusoma vitabu ni sawa na kujaribu kujifunza kupitia maisha ya watu wengine huku ukijua maisha ya mwanadamu hayajirudii.

Kitabu kimewahi kubadilisha maisha yako kwa kiasi gani.
Mambo ya wazungu hayo achana nayo
 
Kiukweel mim naamini kusoma vitabu vinakupa uwezo mpana wa kuliona tatizo au changamoto flani kwa ukubwa zaidi, mfano niliposoma" rich dad poor dad " nilipata mwanga mkubwa juu ya elimu ya fedha namna nzur ya kujenga akili za watoto wetu. Kitu kikubwa ni kujua unahitaji nin, kwa wakati gani na wapi utakipataa.
 
Kiukweel mim naamini kusoma vitabu vinakupa uwezo mpana wa kuliona tatizo au changamoto flani kwa ukubwa zaidi, mfano niliposoma" rich dad poor dad " nilipata mwanga mkubwa juu ya elimu ya fedha namna nzur ya kujenga akili za watoto wetu. Pia ni njia
 
Wakuu habari,

Kwanini watu waliowahi kufanya makubwa hawakufanikisha hayo kupitia kusoma vitabu.

Unakuta mtu anasoma kitabu cha How to influence people lakini hadi anakimaliza hana influence yoyote.

Mtu anaandika kitabu cha how to get rich fast afu pesa ya kuchapisha hicho kitabu amekopa.

Kiufupi nawaza hivi , huenda watu wengi wanaopenda kusoma vitabu huwa ni kwa lengo la kujifariji tu.

Ila mwalimu mzuri wa maisha yako ni uzoefu wako mwenyewe.

Kusoma vitabu ni sawa na kujaribu kujifunza kupitia maisha ya watu wengine huku ukijua maisha ya mwanadamu hayajirudii.

Kitabu kimewahi kubadilisha maisha yako kwa kiasi gani.
Kusoma na kuelimika ni vitu viwili tofauti.
 
Back
Top Bottom