Uchaguzi 2020 Hivi ni kweli kuwa CCM inakubalika kama ambavyo watawala wetu wanavyotuaminisha?

Uchaguzi 2020 Hivi ni kweli kuwa CCM inakubalika kama ambavyo watawala wetu wanavyotuaminisha?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Tunapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020, tunasikia tambo tupu toka kwa viongozi wakuu wa CCM kuwa uchaguzi wa mwaka huu ndiyo "kiama" cha Upinzani na hatutausikia tena Upinzani ndani ya nchi hii baada ya uchaguzi huo utakaofanyika mwezi wa Oktoba mwaka huu!

Swali ninalojiuliza: Hivi ni kweli kuwa upinzani upo mahututi kiasi hicho na kwenye uchaguzi wa mwaka huu tutauzika rasmi?

Hata hivyo ninavyoamini Mimi ni kuwa upinzani ndani ya nchi hii upo imara kuliko kipindi chochote, tokea tuanze mfumo huu wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992, isipokuwa uwanja wa kufanyia siasa nchini ndiyo hauko sawa ndiyo sababu inayowafanya viongozi wakuu wa CCM wajiaminishe hivyo kwa kuwa wanajua kuwa vyombo vyote vya dola ambavyo vinatakiwa kwa mujibu wa sheria viwe "neutral" badala yake vipo upande wa chama tawala cha CCM kwa uwazi kabisa.

Hata hivyo mambo yanakuwa "vice versa" unapoingia kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo Jamii Forum, unaposoma maoni ya wananchi, unajionea wazi kuwa upinzani nchini upo imara zaidi ya tunavyoaminishwa na watawala wetu.

Sasa ni kitu gani kinachowapa kiburi kiasi hicho viongozi wakuu wa CCM hadi watambe kiasi hicho kuwa kwenye uchaguzi wa mwaka huu watauzika rasmi upinzani wa nchi hii?

Jibu ninalopata hapa ni kuwa kiburi chote walichonacho viongozi wakuu wa CCM ni kutokana na Katiba ya nchi yetu namna ambavyo imempa madaraka makubwa mno Rais wa nchi, ambaye pia ndiyo Mwenyekiti wa CCM kitaifa na kumfanya mungu-mtu kwa kila alisemalo na kulifanya kuonekana kuwa kama ndiyo sheria na vyombo vyote vya dola kutekeleza kauli zake kwa vitendo bila kuangalia kuwa yupo sahihi au amepotoka.

Kwa mfano, Rais amepiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani, wakati huo huo akiruhusu mikutano ya chama chake cha CCM iweze kuendelea bila kubughuziwa na Jeshi la Polisi, na hilo linafanyika.

Tujiulize hivi: Rais anapata wapi madaraka ya kuzuia mikutano ya vyama vya siasa vya upinzani, ambavyo vipo kihalali kisheria?

Kama kweli CCM inajiamini kiasi hicho kuwa imewafanyia mambo mengi sana ya kimaendeleo wananchi na kuwa inakubalika sana na wananchi, basi ikubali kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi na hivi vyombo vya dola, kama Jeshi la Polisi na Usalama wa Taifa, vifanye majukumu yao kwa weledi na kwa mujibu wa katiba na visiegemee chama cha CCM na viwe "neutral" badala ya sasa hivi kuwa kama vitengo vya CCM.
 
Swali ninalojiuliza, hivi ni kweli kuwa upinzani upo mahututi kiasi hicho na kwenye uchaguzi wa mwaka huu, tutauzika rasmi?
Ni kweli, CCM inakubalika sana na uthibitisho wa kwanza ni ushindi wa kishindo cha asilimia 99.9% kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ulioendeshwa kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi huru na wa haki kwa kutumia kanuni ya " the end justifies the means" mshindi ni CCM.

Uthibitisho wa pili utapatikana November mwaka huu ambapo sasa kwa huku bara CCM inakwenda kuzoa viti vyote vya ubunge na udiwani, wembe ule ule uliotumika kwenye Serikali za Mitaa, ndio utatumika uchaguzi Mkuu wa October hii.

Hii yote ni kufuatia Rais Magufuli kukubalika sana hadi viongozi wa upinzani waliojitambua, wanaacha vyama vyao na kujiunga CCM.

Kwa mujibu wa sheria iliyounda Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni Tume huru japo sio shirikishi, na uchaguzi unaendeshwa kwa kanuni za uchaguzi huru na wa haki ila uwanja wa ushindani sawa wa kisiasa ndio uko tenge, yaani the playing field is not level.

Kwa ushindi wa kishindo wa CCM kwenye uchaguzi Mkuu ujao, naomba kuanza kutoa pongezi in advance.

CCM Oye!
Oyeee!
Viva Magufuli
Viva CCM
Mungu Ibariki Tanzania

P
 
Nakumbuka kwenye Uchaguzi wa Uingereza mwaka jana ilikuwa ukiingia kwenye mitandao ya kijamii bila kujua hali halisi kwenye uwanja wa mapambano ilikuwa inatoa picha kuwa chama cha Conservative kilikuwa kinaelekea kufutika bungeni.

Kelele za kwenye mitandao ya kijamii ziliwafanya wajinga wakadhani Labour inakwenda kukifanya chama cha conservative kuwa na wabunge wachache kama chama cha Liberal.

Baada ya matokeo ya kura kuanza kutangazwa, wale manazi wa Labour kwenye mitandao ya kijamii walianza kupotea mmoja mmoja.

Hii inaonyesha kuwa mshindi katika chaguzi kuu sio yule anayepiga kelele nyingi kwenye mitandao ya kijamii bali ni yule anayejua uwanja wa vita na wapiga kura wake.

Siasa ni kuwapa matumaini wapiga kura hata kama wanachokitumaini hawakipati kwa muda huo.

Wapinzani waliwapa matumaini wapiga kura mwaka 2015 kuwa tatizo la Tanzania ni ufisadi. Matumaini hayo yaliifanya CCM itafute mgombea ambaye wapiga kura hasa wa kipato cha chini watamuamini kuwa anaweza kutimiza matumaini yao.

Leo hii wapiga kura hasa wa kipato cha chini ambao ni wengi wameweka matumaini ya kisiasa na kiuchumi kwa CCM na Serikali yake.

Wapinzani kwa sasa wanajaribu kubadili ajenda iwe tatizo la Tanzania ni "Tume huru" ya Uchaguzi. Sioni kama wapiga kura hasa wa kipato cha chini ambao ni wengi watawaunga mkono.

Never underestimate the social awareness and sense of reality in a quiet person; they are some of the most observant, absorbent persons of all and don't underestimate the power of being underestimated.




Sent from my iPhone
 
MsemajiUkweli, Kulinganisha siasa za Ulaya na Afrika ni wendawazimu wa hali ya juu sana. Eneo la kwanza kura ya mwananchi ina umuhimu, eneo la pili kura ya mwananchi na mwananchi wote hawana umuhimu.

Halafu mbona ilifahamika mapema kabisa kwamba Labour Party hawawezi kushinda kwasababu walikuwa wamegawanyika kwenye mambo ya msingi kuliko ilivyo kawaida.
 
MsemajiUkweli, Ukimya wa mtu una majibu mengi never underestimate, but not in Tanzania, hata hao wakimya wakiamua kufanya wanayotaka bado kuna ushahidi wa kila namna kwamba kura zao haziheshimiwi, utasikia watu fulani wameiba masanduku ya kura wamekimbia nayo, mara mgombea wa chama fulani cha upinzani katekwa siku ya kupiga kura, au mawakala wa upinzani wameondolewa wote kwenye vituo kwasababu wameshindwa kujaza form!

So, usijaribu kulinganisha ukimya wa ulaya na wa hapa Tanzania, ukimya wa Ulaya una direct impact kwenye uchaguzi, but ukimya wa mtanzania haumsaidii chochote mpiga kura, mara nyingi maamuzi/ haki yao ya kumchagua wanayemtaka siku zote huporwa na chama tawala kutokana na sababu nilizoainisha hapo juu.

Nchi yetu kwenye uchaguzi bado haijawa na ustaarabu huo wa ulaya, bado tupo nyuma sana, siku zote mgombea wa chama tawala anajiona mwenye nguvu zaidi ya mpinzani, sababu anajua dola itakuwa upande wake, hawaheshimu tena nguvu ya kwenye ballot box, ndio maana wengi sasa wanakimbilia CCM kwa kuamini ubabe wa Magufuli utawabeba kwenye uchaguzi mkuu ujao, habari ya kuunga mkono juhudi ni utapeli mtupu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla, Kweli ni Tume Huru japo sio shirikishi, hivyo ina uhuru wa kumpendelea inayemtaka, hasa wa kutoka upande yule bosi wao aliewateua anayewalipa mishahara.

But all in all, regardless of the circumstance, bado upinzani upo Tanzania, na hakuna uthibitisho wa kweli nguvu ya upinzani Tanzania inapungua, nionavyo una nguvu zaidi, if they want to prove it, WALETE LEVEL PLAYING FIELD, watapotezwa vibaya, and they know it very well, vinginevyo ni kujidanganya tu kusema upinzani unapotea nchini.

Wengi wanajidanganya upinzani unapotea sababu hawajaona mikutano ya hadhara ya wapinzani, wamezoea kumuona Dr. Bashiru kila siku akizunguka Tanzania nzima peke yake, ndio maana wamekuwa vipofu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MsemajiUkweli,
Ni hivi, ushindi wa ccm unapatikana kutokana na Magufuli kutumia madaraka yake vibaya kupitia katiba mbovu. Hata muandike biblia ukweli uko wazi. Na ukweli ni kuwa Magufuli hawezi siasa za ushindani, na hata alipokuwa mbunge hakuwahi kushinda kwa kura bali figisu.

Tabia yake hiyo binafsi ndio kahamishia nchi nzima kutokana na mapungufu ya katiba. Hakuna nje ya hilo fullstop.
 
jd41,
Kwa kuzingatia vigezo na masharti ya kiutaalama na kiufundi siyo huru!

Vipo vigezo vilivyoainishwa kitaalam na kiufundi kwa tume ya uchaguzi kuwa huru au la!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Napenda kutofautiana nawe Mkuu Pascal Mayalla kwa kuchukulia uchaguzi wa serikali za mitaa, kuwa ndiyo kigezo chenu cha CCM kuwa itazoa ushindi wa tsunami kwenye Mkuu wa mwaka huu.

Hivi utawezaje kuuita uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa huru, wakati ukweli unajulikana, hata ukimuuliza mtoto mdogo anayesoma chekechea atakueleza namna uchaguzi huo ulivyovurugwa kiasi cha kutisha, kwa baraka zote toka viongozi wa ngazi za juu wa CCM?

Hivi uchaguzi uliojaa mizengwe kiasi kile kwa watendaji wa kata "kuwakacha" wagombea wa upinzani kuwapokelea fomu zao za kugombea, ndiyo Mkuu unaweza kuthubutu kudiriki kuwa uchaguzi ule ulikuwa huru na haki?
 
Kwa kuzingatia vigezo na masharti ya kiutaalama na kiufundi siyo huru !

Vipo vigezo vilivyoainishwa kitaalam na kiufundi kwa tume ya uchaguzi kuwa huru au la !


Sent using Jamii Forums mobile app
Kitaaluma ndio kisheria; ipo huru, kwamba imeanzishwa kwa mujibu wa sheria namba...ya mwaka... na kwamba Rais atateua mwenyekiti wake, in that case existance yake inatambulika kisheria ipo huru, so that is on paper; but tukija kwenye uhalisia ndio neno shirikishi lina apply.

Je, hawa wengine ambao hawajahusika kwenye kuteua mwenyekiti wanapewa nafasi sawa kwenye majukumu ya kila siku ya hiyo tume (chaguzi mbalimbali ambazo tume inazisimamia) ndio maana ikaitwa iko tenge/upande, inapendelea/kuegemea upande mmoja wa aliewateua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu,majibu yake ni mepesi sana,wewe hauishi mbinguni upo na jamii inayokuzunguka,jalibu kupitapita maeneo tofauti tofauti kwa muda wa siku kumi,chunguza jibu utalipata kama hawa watu wa rangi ya SENENE wanakubalika?

Pia umwambi bwana Mayalla,P,baada ya mwezi wa 12 aje na takwimu ya watakaopiga kura watakuwa wangapi?uone kama watafika hata wapigakura milionin 6 nchi nzima.
 
KANYAMA,
Unanikumbusha hadithi ya kale ya mtu aliezusha tukio la uongo na baadae yeye mwenyewe akaamini uongo wake mwenyewe.
 
Back
Top Bottom