Hivi ni kweli mshahara wa Rais ni Milioni 9 kama alivyowahi kutuambia Hayati Magufuli?

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Enzi ya uhai wake, hayati Magufuli aliwahi kutuambia kuwa analipwa shilingi milioni 9 kwa mwezi na akirudi toka mapumzikoni Chato atatuonyesha hati yake ya mshahara (salary slip).

Bahati mbaya mpaka anaingia kaburini hakuwahi kutuonyesha hiyo salary slip yake.

Je, ni kweli mshahara wa Rais ni milioni 9?
 
Sasa kama hatumii hata mia kuanzia msosi,safari na kusomesha mm naona hata angepewa laki ingetosha
 
Na wewe ulivyo na akili ndogo ukaamini?
 
Nikweli kwanu msharahara wa katibunkiongoiz ni 6 million .Hata wabunge mshahara ni 2.4 million lakink ukiweka marupurupu yasiyokatwa Kodi, Rai's anapata kama 60 take-home kila mwezi wakati wabunge wanakula 12 million take home
 
Tungekuwa na madaraja matatu ya mishahara Tanzania. Maafisa na watumishi daraja la chini wangelipwa laki tano. Maafisa wajuu wangelipwa milioni 1. Maafisa wajuu waandamizi wangelipwa M3. Raisi tungetafuta pa kumuweka katika makundi hayo. Kama record inaonhesha alikuwa karani mzuri basi hata kazi yake ya awali itazingatiwa
 
🀣🀣 Na wewe ulikuwa unamwamini yule tapeli? 😁😁
 
Ila yule babaπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™ŒπŸ™Œ
 
Si kweli nakataa rais pia anaweza kujichotea hata bilioni 5 akazichimbia hizo zikawa zake tu
 
Kwenye makaratasi inaonyesha hivyo (milioni 9), kipindi cha JK ilikuwa milioni 7

Zingatia neno makaratasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…