Hivi ni kweli mtu akila chakula kizuri tofauti na mlo aliouzoea atapata shida ya tumbo?

Hivi ni kweli mtu akila chakula kizuri tofauti na mlo aliouzoea atapata shida ya tumbo?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
11,208
Reaction score
20,517
Kuna mama jirani hapa kaja kunitembelea Leo,huyu Mama kazi zake ni za saidia fundi, kufua pamoja kufanya usafi Kwa watu.

Sasa Leo alichonishangaza ni alichoniambia, kuwa Jana alipikia watoto Wake ( wako below 11 yrs)chakula ambacho ni muda mrefu hawajala.

Anaendelea kusema kuwa siku ya Jana baada ya kupata malipo mazuri kidogo aliamua apikie watoto wake chakula kizuri aina ya wali,anasema alinunua nyama robo akapikia watoto wake Wali na Nyama ila Cha kushangaza Baada ya muda wa masaa kadhaa kupita watoto wakaanza kuharisha.

Sasa anasema chanzo Cha watoto wake kuhara ni kutokana na kula chakula kizuri (wali nyama)

Maana hawajozea aina mpya ya chakula kizuri kama hicho Bali wamezoea kula ugali na mboga za majani Kila siku kuanzia mwanzo wa mwaka Hadi mwisho wa mwaka Sasa kitendo Cha kula chakula kizuri ndo maana watoto wake wakadhurika.

Je Kuna ukweli kuhusiana na Hilo?
 
Kuna ukweli kuwa unaweza kuvimbiwa na kuharisha kwa kula chakula kizuri kwa kuwa tumbo halijazoea kuchakata chakula hicho japo kuna sababu zingine huwa zipo kwa mtu kuharisha kama kula chakula kichafu chenye vimelea vya magonjwa na sumu
 
Kushindilia chakula tumboni nako kuna madhara. Unaweza kutapika na kuharisha, unakuta mtu anakula kilafi chakula kingi cha kigeni kwa kuwa hana uhakika wa kukila tena basi anabugia chakula kingi tumboni na hatimaye kinamchachia huko tumboni anaanza kuharisha
 
Nyama robo mzoga...
 
Kuna ukweli kuwa unaweza kuvimbiwa na kuharisha kwa kula chakula kizuri kwa kuwa tumbo halijazoea kuchakata chakula hicho japo kuna sababu zingine huwa zipo kwa mtu kuharisha kama kula chakula kichafu chenye vimelea vya magonjwa na sumu
Nyama robo kawalisha watoto mzoga lazima wakashikilie ukuta chooni..
 
HII HAPA SABABU WATU WANAOOSHI MAISHA MAGUMU WAKIINGIA KWENYE SHEREHE BURE HUWA WANAPENDA KULA SANA UTAKUTA MTU ANAKULA SAHANI MBILI JALALA HATA VITOTO, LAZIMA UVIMBIWE NA KUHARA.

KWAHIYO WATOTO WALIVIMBIWA KWA UROHO NA KUHARA NA SI CHAKULA KIPYA HUU NI UONGO KABISA OTHERWISE LABDA NYAMA ILIYONUNULIWA ILIKUWA IMEOZA HAKUNA SABABU ZAIDI YA HIZI.
 
Mkuu, nyama robo familia inavimbiwa vipi??? Tatizo mpishi tu, hata huo uozo wa nyama hauusiki. muulize alipikaje hyo nyama. Utakuta aliikatia nyanya kama anaunga dagaa.. inatakiwa asirudie tena huo mchezo.. bora akanunue mishkaki next time. ataua watoto.
 
Tahadhari!
Kutokana na uhaba wa nyasi na jua kuwa kali sana, kumepelekea ng'ombe kukosa malisho na hatimae mlipuko wa magonjwa.

Ng'ombe wengi wanaochinjwa mabuchani ni wale waliodungwa madawa mengi sana. Hivyo nyama zao zina chembechembe ya sumu za madawa ya mifugo.
Na wengi wa wauza nyama mabucha ya uswahilini, huchanganya nyama ya ng'ombe aliyejifia na yule aliyegongwa muhuri na maafsa ukaguzi.
Mifugo inayotokea mikoa ya nyanda za kati, morogoro na ukanda wa pwani kwa kipindi hiki cha jua kali, inaishi kwa kudungwa sindano.
Hivyo matumizi ya nyama zake ni hatari kwa afya ya mtumiaji.
 
kuna yule mzee aliyegundua nembo ya taifa.yule mzee alizoea kula jalalani.siku serikali ilivyogundua,wakampeleka IKULU wakampa pilao kuku yule mzee alivyokula minyoo ikayoboa utumbo kwa mshtuko,yule mzee akafa
 
Back
Top Bottom