Hivi ni kweli watu wanarogwa wasipige hatua za kimaendeleo?

Unakuta mtu kila unachoshika hakishikiki

Na unakuta umewekeza akili, jasho na damu lakini wewe unakuwa tu wa mkia.

Wajuvi wa mambo karibuni
Kwa nchi kama hizi zetu na za ubepari uliopitiliza sehemu kubwa ya mafanikio ya watu inategemea zaidi familia uliyotoka, connections, kipaji na bahati, jitihada ni jambo la mwisho kabisa kwa wengi unaowaona wamefanikiwa sana.
 
Kwenye imani unaweza kuamini ni kweli watu hulogwa , ila kwenye uhakika yakini na kweli sio kweli kuwa watu hulogwa, zipo sababu zake za uwazi kabisa za mtu kushindwa kuendelea.

Hapo uchague wewe pa kusimamia sasa.
 
Bahati ni nini haswa
Ni jambo linalokujia bila jitihada au kujipanga sana.
Mfano mama au baba yako awe kiongozi mkubwa kwa hiyo akupachike sehemu au akupe dili la biashara au connections.

Mfano muende kufanya usahili watu 2000 kwa kazi ya kawaida tu lakini watu 10 ndio wanaohitajika, hapo unaweza kukuta hata 1000 wana vigezo vya kufanya hiyo kazi lakini watakaochaguliwa ni 10 tu kwa sababu haiwezekani wote wenye vigezo mkapewa kazi na vitatumika hata vigezo visivyo na mashiko kuwapunguza tu mpake wafike watu 10.
 
Bahati ni nini haswa
Ukienda kwenye uchimbaji madini wa hawa wachimbaji wadogo wanaobahatisha au kutumia vifaa hafifu vya kutambua madini kama utachimba kwenye mwamba usio na madini hata utumie jitihada gani kuchimba utatoka Kapa tu, mwingine akienda kubahatisha sehemu yenye mwamba wenye madini akayapata kwa haraka na mengi kwa ujinga tu unaweza kuhisi uganga au uchawi ndivyo vimemfanya mwenzako kupata hayo madini na kwamba wewe uliyekosa umelogwa kumbe hapa suala ni bahati tu.
 
Kama kupambana wengi wanapambana kwa nguvu, lakini ni akili ya kuona fursa na kuvuka changamoto unazokutana nazo ndio itaamua nani afanikiwe. Mambo yakifeli angalia chanzo badala ya kuhusisha uchawi.

Akili + jitihada + consistency = mafanikio, kikikosekana kimoja hapo utaishia kutimiza ndoto za wengine.
 
Kwenye imani unaweza kuamini ni kweli watu hulogwa , ila kwenye uhakika yakini na kweli sio kweli kuwa watu hulogwa, zipo sababu zake za uwazi kabisa za mtu kushindwa kuendelea.

Hapo uchague wewe pa kusimamia sasa.
Uchawi upo wazee na unafanya kaz sambamba na husuda ( kijicho). Sehem yoyote ikizungumzwa kuw n uchawi uliopitiliza bas hata mendeleo huwa chini sana. Mana husuda ina mchango mkubwa san kwenye kupata n kukosa

Angalia kiwango cha maendeleo mikoa y kusini angalia pia hali ya mstumiz y uchawi
 
Unaniambia upo bila kuleta uthibitisho ? Mimi sitaki kuamni tu , kwa umri wangu na uzoefu wa maisha naona ni imani tu basii na ndivyo ilivyo .
 
Ni imani za watu tu mkuu. Mambo yasiyo bayana. Kama huamini sio tatizo.
Wachawi wapo uswahilini kutwa kushinda vibarazani tu, hususani wanawake wanaroga [*******] wateja wakubwa wa mambo hayo ya shirki na ulozi kwa waganga wa kienyeji ni wanawake.. kuanzia asubuhi mpaka jua linazama unakuta vibibi na wanawake wa makamo na vibinti vimeshinda tu vibarani km sio vibarazani chini mti kuangalia kila anaepita ukipita tu wanaanza kuwanga kukuongelea yule hivi yule vile na huko ndio kuroga kwenyewe sasa, wewe ulifikiri kuroga mtu hadi akaubebee matunguli wakati waganga siku hizi wananyuka suti na wana ofisi kali.. maongezi yao ni nazi nazi nazi unajua kazi ya nazi ?
 
Imani za Uchawi/ Ushirikana/ Uganga zimejaa Tanzania yote, labda watu wa Kusini wao hawajifichi tu au kuonea aibu hayo mambo kwa hiyo wanafanya kwa wazi tofauti na wengine wanaoifanya kwa kificho.
 
Kuna maeneo hapa Tanzania miaka 20 iliyopita yalikua hayana maendeleo na waliamini sababu ni uchawi na husda lakini baada ya ongezeko la watu wa kutoka nje ya maeneo hayo wameziona fursa ambazo wenyeji walikua hawazioni kwa kuamini uchawi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…