Hivi ni kweli Wizara ya Ardhi imeshindwa kutatua kero za wapangaji nchini?

Wizara zinazo onekana kumsaidia mh Rais na watanzania ni..
1.wizara ya ulinzi
2.Mambo ya nje baada ya kuja kabudi
3.Tamisemi
4.Nishati
5.Madini
6.Maji .....Hii ni Baada ya mbarawa kuvuta bangi chooni nakweli amevuta maana kwa kasi hii arudishwe tena na naibu wake mzee wa kuzinguana tunaona mwezi sasa.
7. Viwanda
8.Elim
9.Utawala bora

Wizara zinazofanya vizuri ila hazina ufatiriaji mzuri na wakina na wakimbinu zaidi ni wizara ya
1. AFYA Bado kunashida kubwa mahospitalini waziri fatiria kwa mbinu nishida sana , nitaasisi za jakaya na Moi na saratani ndo hazina kashfa
Huko vijijini ndo baraa zaidi na mshauri waziri pamoja na juhudi kubwa za kodi zetu kuwekeza huko na upatkanaji wa dawa kuwa mkubwa ila huduma , na ukipata malalamiko mtafute alielalamika akueleze badara ya kujibu kwa ujumla.
Wizara ya mambo ya ndani inaenda vizuri kuna tatizo lawatu wachache wanaokwamisha
Wizara ya .. mazingira na muugano tumpe mda zungu na uzuri ameliona tatizo mwenyewe nacyo mifuko tu ya plastic
Wizara ya sheria na katiba... Pako vizuri ni mambo ya mda kuondoa kasoro na kujipanga kurekebisha sheria zisizo na masrahi badara ya kumsubiri rais kutoa maelekezo
Wizara ya Kazi ajira na.... Hii bado sana mhagama na mavunde hawana lolote wanafanya vitu kama moto wa mabua. Nazani hawa wote hawafai kabisa, mfano mavunde kunakodi nyingi sana mnapoteza kwa wafanyakazi ambao hawapewi mikataba, mhagama nae mashirika yamemzidi nguvu yanajipigia tu mpaka mkuru atumie vyombo vyake yy kakaa tu.

Ngoja nikale kwanza
 
Hukuna sababu ya kupiga marufuku watu kujenga. Hio serikali ijenge hizo nyumba Bora na nafuu kuliko ambazo watu wanajenga,waziuze kwa mikopo nafuu uone kama watu watahangaika kujenga makazi holela.
 
Location,location,location.
 
Hukuna sababu ya kupiga marufuku watu kujenga. Hio serikali ijenge hizo nyumba Bora na nafuu kuliko ambazo watu wanajenga,waziuze kwa mikopo nafuu uone kama watu watahangaika kujenga makazi holela.

Hilo nalo ni wazo zuri, itasaidia sana kuweka mpangilio bora wa makazi na mazingira ya kuishi yanayovutia.
 
Halafu msisahau. Kodi kwenye pango zipo.
1.withholding tax ambayo ni 10%
2.stamp duty 1%

Mwenye nyumba atakuongezea wewe tu, yeye hataumia. Mfano Kodi yako 300,000/- ukiongeza tax inabidi iwe 330,000/- ili kulipa 10% na yeye abaki na 300,000/- yake. Je mpangaji utachagua ulipe 300,000 au 330,000/- ?
 
Huwezi kuregulate makazi yasiyo rasmi. Huyajui, Sasa utaregulste vipi?
 
Acha tulipe tuu ili tuwasaidie wenye nyumba, maana wamegharamika kujenga hizi nyumba tunazopanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wala hatukatai kuwa waligharamika, tunataka tu kuwe na utaratibu kisheria. Kama ilivyo mtu akitaka kufanya biashara ya Bus amegharamika kulinnua, lakini lazima afuate bei elekezi zilizowekwa pamoja na kuhudumia watu kwa utaratibu.
 
Huwezi kuregulate makazi yasiyo rasmi. Huyajui, Sasa utaregulste vipi?
Nilidhani serikali sasa iko kwenye kazi ya urasimishaji makazi? Tuseme Waziri Lukuvi hakusema ukweli?
 
Hivyo sivyo inavyopaswa kuwa ndugu. Kwenye hiyo 300 yake inakatwa 30, na anapaswa kuwa na mashine ya efd....Hizi mambo naziona Masaki, Obey, Mikocheni. Mzungu huwezi kumpangisha nyumba kizembe bila receipt.
 
Hivyo sivyo inavyopaswa kuwa ndugu. Kwenye hiyo 300 yake inakatwa 30, na anapaswa kuwa na mashine ya efd....Hizi mambo naziona Masaki, Obey, Mikocheni. Mzungu huwezi kumpangisha nyumba kizembe bila receipt.
Wewe wasema. Mwenye nyumba kashaamua apate 300,000/- hio 10% utalipa wewe anaongeza kwenye Kodi. Mwisho wa siku mpangaji ndio anabeba mzigo. Wewe unaona Masaki Sisi tunalipa hivyo humu uswahilini kwasababu tra ukienda kwenye makadirio ya Kodi lazima ulete mkataba wa pango na ulipiwe 10+1%
 
Nilidhani serikali sasa iko kwenye kazi ya urasimishaji makazi? Tuseme Waziri Lukuvi hakusema ukweli?
Kwa kuongea, sawa.
Ila lile zoezi sidhani Kama kumekuwa na mafanikio yeyote. Sanasana limechangia wizi wa Mali za watu.
Yaani watu wanatembea na kisimu halafu wanarekodi coordinates na kuandika mmiliki bila ushahidi wowote.
Na hizo hati zenyewe sijui ngapi zimeshatoka.
 
Nawakumbusha tu ikiwekwa hiyo kodi kwa wenye nyumba tunaoumia n sisi wapangaji mwenye nyumba ataijumuisha kwenye kodi zake hivyo hapo wananchi wenzangu wa kawaida n bora tukakaa kimya tu tusipoteze muda kulilia maumivu tukizani tunawakomoa wenye nyumba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama wapangaji wenyewe mmeshindwa kujiunga na kutetea maslahi yenu mnatarajia wenye nyumba ndo wawa tetee?au mnatarajia serikali ndo iwatetea.Kama mnataka kuondokana na kero basi hakikisheni kwanza mnaungana na kuunda Chama cha Wapangaji.Kisha muwe na Viongozi wenu muwe na ofisi zenu,Mlipe ada za uanachama kisha mtatewa na maslahi yenu mtapata.

Kama hamuwezi kujiunga basi hamuwezi kudai haki.Nimemaliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…