Hivi ni lazima kila raia wa Tanzania awe na kovu la ile sindano ya ndui begani?

Asante sana kiongozi.
 
Shida yangu NI kwanini waliamua kuchanja wtz wote sehemu moja, mbona mataifa mengine hawana hii alama?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
Nadhani Ni mpangilio tu wa kutambulisha watu wa nchi fulani kupitia alama chanjo.


Ukitaka kujua huyu Ni mtanzania utaangalia begani, Wakenya wao wanachanjwa katikati ya mkono wa kulia kinabaki kialama, Hawa wakitaka kuthibitisha umezaliwa Kenya kienyeji utaona wanakwambia nyoosha mkono.

Waethiopia wanachanjwa begani Kama sisi.
Kuna siku rafiki yangu muethiopia aliona alama yangu begani alikuwa surprised akasema nyie mnachanjwa begani Kama sisi.
 
Kama ugonjwa ulitokomezwa kwanini mpaka sasa watu wanachanjwa?
 
Kwa maelezo ya wadau...hii alama si ya mtanzania pekee
Nchi zote barani Afrika, wanachanja chanjo ya ndui. Isipokuwa raia wao wanachanja mapajani au mkononi chini kidogo ya mabegani. Raia wa DRC wamechanjwa chini ya bega. Raia wa Burundi wamechanjwa mapajani. Ndui likuwa ugonjwa hatari sana, ambao kwasasa umeweza kuthibitiwa.
 
Kama ugonjwa ulitokomezwa kwanini mpaka sasa watu wanachanjwa?
Kwa uelewa wangu chanjo ndio inatokomeza ugonjwa. Mtu akichanjwa gonjwa likija halitamuathiri, usipochanja watu watakuwa hawana Kinga ya kupambana na ugonjwa so gonjwa likija litafagia tu. That's why chanjo zinakuwaga Ni za muendelezo, Mtoto akizaliwa lazima apewe ili imlinde.
 
Mimi nimezaliwa Msoga Chalinze na wala sina hiyo alama yenu ya kitaifa.
 
Huko nchi za wenzetu watoto wanadungwa? Au ni ka program ka muda mrefu kakuhafifisha kizazi.. Cha jamii fulani.

Twende tu hapo kwa wadzabe wawe kama mfano wetu.
 

Mzee umechemka sio smallpox bro ni BCG
 
Chanjo(vaccine) dhid ya ugonjwa wa kifua kikuu kawaida unaweza kuwekewa wadudu walio dhohofika ila wapo hai, live attusinate ama walio kufa, ama genes za wadudu sasa kwenye ndui unawekewa wadudu wa walio hai wa TB ila wamedhohofishwa ili kinga ya mwili iwatambue kwa ajili ya kutengeneza kinga dhidi yake
Sasa mara zote huchomwa chini ya ngozi epedermis na hutengeneza kovu kma ndui na tz walichagua bega la kushoto.
Pia katika madhara ya hii chanjo muda wowote immute yako ikishuka wale jamaa wanaamka na kukuletea tb inaweza ikwa ya mapafu(pulmonary tb) ama extrapulmonary tb kifupi ndo hivyo mkuu
 

Bacillus Calmette–Guérin inaitwa BCG Kwa kifupi na anachoma mtoto baada ya kuzaliwa on same day
 
"Mkononi sina tattoo bali na alama ya ndui,mtanzania namba moja majungu hayasumbui" - Prof Jay.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…