Hivi ni mimi tu haya maisha yanataka kunikataa?

Jipige kifuani tena huku ukijisemea "mimi ni mwanaume" 💪💪💪..... halafu amka ukapambane.....

Onyo.

Usiongeze mtoto ata iweje...
 
Kwa mshahara huu unaanza vipi kusaidia wengine kaka??

Unaonekanaje kwenye jamii yako au hao ndgu zako wanakuonaje?? Isijekua unajionesha una pesa/ unalipwa vizuri ndio maana wanakuona wewe ni tegemezi.

Kazi yangu ya kwanza takehome ilikua 250k, na hapo nilikua najiweka nyuma kwenye kila kitu.
Sitoi pesa kwenye familia kindezi, "sina" ndo ulikua msemo wangu pendwa.

Mtu ukimpa pesa leo, tegemea na kesho lazima aje tena kuomba umkope.
 
Hili swali ni la msingi, na kama akilijua jawabu lake, huenda akajinasua kwenye huo mtego uliomnasa.
Kakuambi ni wadogo bado wanasoma na kaelezea yeye ndo first born!!
Mtu kukosa kipato suo lazima awe na ulemavu.
Jaribuni kuvaa viati vyake.
Kuna maisha watu wanapitia na sisi tuliofanikiwa unaona ni sababu za azembe ila omba yasikukute.
 
Kakuambi ni wadogo bado wanasoma na kaelezea yeye ndo first born!!
Mtu kukosa kipato suo lazima awe na ulemavu.
Jaribuni kuvaa viati vyake.
Kuna maisha watu wanapitia na sisi tuliofanikiwa unaona ni sababu za azembe ila omba yasikukute.
Wakati unaangalia maisha ya wengine, usisahau kuangalia na yako.
Ukiiendekeza 'black tax' lazima yakufike shingoni kama jamaa yako.
 
Tatizo kichwa chako, mbona wapo walimu wanaishi vizuri sana na wengine wametoboa. Yaani umejiingiza kwenye madeni na hamna ulichofanya yaani umekula bata tu, mnavyoanza kazi huwa mnapenda maisha ya show off. Ninachokushauri omba uhamisho kaishi kwa utulivu kijijini huko hakuna matumizi makubwa
 
Kweli nyuma ya deni Kuna maisha mengine lazima yaendelee
 
Wakati unaangalia maisha ya wengine, usisahau kuangalia na yako.
Ukiiendekeza 'black tax' lazima yakufike shingoni kama jamaa yako.
Kwa vyovyote huna uzoefu na changamoto wanazopitia vijana ambao ndo wanaanza maisha na wanatokea familia maskini!!
Usihukumu wengine kwa vijisenti ulivyo navyo aidha kwa kupitia familia inayojiweza.

Nawasikitikia ila huwezi kuwahukumu ni mfumo umewakuta.
Mind you niko above 50 usidhani unachat na undergraduate humu!!!
 
Inawezekana mkuu ukiwa na nidhamu ya fedha na ukiwa na bajeti unaona haiwezekani kwa sababu unakosa hivyo vitu viwili
kama ww pesa yako ni yako tu husaidii ndugu jamaa na marafiki na huna majukumu mengine mfano ya kifamilia na vile vile huna mahitaji mengine binafsi kama vile kuvaa, kula n.k hapo nakubaliana na ww.

Kusave pesa kwa kipato cha mshahara tu( yani uwe na pesa umeitunza tu bank) ni kitu ambacho kiuhalisia wa utekelezaji hakiwezekani tuache kudanganyana.
 
Maisha magumu wakati unakazi?Wenzio tuko tu maghto mwaka wa tatu huu kazi hamna,tulishaachishwa:,mke na mademu walishatukimbia,watoto Karibu wanasahau kama Wana baba maana kuwaona mpaka uwe na pochi,halafu anakuja mtu kama ww na sharubu zako unalalamika kweli?dunia Haina usawa.
 
Wewe hujui tu mkuu
 
mkumbushe
 
Relax and take it easy, stress pia huchangia mambo yasiende
 
Huyu ni mm kabisa[emoji17][emoji17][emoji17]
 
Pole mkuu kwa changamoto unayopitia.
Kama mdau alivyosema huenda mikopo ndio inakutesa zaidi kwa maana umekopea mshahara na hela ya mkopo imeisha lakini majukumu yako pale pale na imefikia wakati mshahara hauwezi kukidhi mahitaji.

Usikate tamaa, punguza matumizi yasiyo lazima, punguza kusaidia ndugu pasipo ulazima (kuwa bahiri na ukubali kusemwa na hao utakaowanyima hela). Shida za familia zetu huwa haziishi hasa kwenye extended families, shida zingine ignore sema huna hela hata kama ipo. Kubali nao wapitie kipindi kigumu cha mpito hawatakufa, hii itakupa ahueni ya mzigo kwenye matumizi kwa kiasi kidogo cha pesa unachopata.

Kubali kuwa umekosea mahali fulani jipe mda urekebishe kosa hilo (mpaka utakapomaliza kulipa mkopo).
Jitahidi kulipa madeni uliyokopa, usijaribu kudhulumu uliowakopa bora ulipe kidogo kidogo kuliko kudhulumu.

Punguza matumizi then ufocus kwenye kulipa madeni hasa hasa ya watu binafsi maana kama ni ya benki unakatwa automatically.
Kingine jitahidi kufanya saving hata kama ni ndogo kiasi gani iweke tu at least 10% ya unachopata kama utaweza.

Kwa sasa usifikirie kuacha kazi endelea na kazi ila acha kuwaza kwamba watu wengine watakuonaje kwa hali yako ya sasa. Hayawahusu, ishi maisha yako usiishi watu wanavyotaka uishi, ishi utakavyo kulingana na hali yako.

Nakutia moyo kuwa hayo unayopitia, kwenye maisha hutokea kwa wengine pia. Mwiko kukata tamaa maadamu una afya njema mengine unaweza kuyafix na ukabadilisha kabisa hali uliyo nayo kwa sasa na ikawa historia. Jipe mda!
 
Usiache kazi watu wengi tu wenye changamoto kama yako lkn kazi hakuna kuacha ,niishie hapa.
 
Mbongo ukimwambia hiv basi huwa anafurahi sana bt ukimwambia kama una maisha safi huwa wanaumia sana wanatamani wote tuwe na maisha magumu yaani sheeda tupate wote
 
Acha kabisa kubet
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…