Dialogist
JF-Expert Member
- Apr 14, 2014
- 1,512
- 2,508
Hii barabara ya mwendokasi ya kupita Mbagala Kila uchwao inaleta ajali, watu wanakufa kila mara bila sababu za msingi na serikali ya mtaa, kata, wilaya, kuu zote zipo na zinajua kinachoendelea. Maana ni wao ndio wameifungulia hii barabara ili gari zipite.
Hii barabara haina alama yoyote ya usalama, madereva hawafati sheria. Ni vifo mara kwa mara.
Leo hii asubuhi imetokea ajali mbaya sana eneo la msikitini (picha) na inasemekana ni watu wengi wamefariki ikiwemo madereva wote wawili. Kana kwamba haitoshi eneo hilo hilo jana ilitokea ajali. Haitoshi tena leo mchana wa saa 6 ajali nyingine barabara hiyo
Hilo eneo la kipati, na watu wawili kuhofiwa wamefariki papo hapo waliokuwa wamepakizana mishkaki kwenye pikipiki iliyoanguka nao kukanyagwa na fuso. Jioni hii tena maeneo ya Kipati, ajali ya bus na bajaji. Asante Mungu hakuna vifo.
SERIKALI YETU SIKIVU, HILI NI MPAKA LINI???