Hivi ni msomi mzuri wa 'sociology' au 'psychology' ndio mwenye utaalam wa kusoma tabia ya mtu na kubashiri matokeo? Je, jibu la Rais ni sahihi?

Hivi ni msomi mzuri wa 'sociology' au 'psychology' ndio mwenye utaalam wa kusoma tabia ya mtu na kubashiri matokeo? Je, jibu la Rais ni sahihi?

Mwanamayu

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2010
Posts
11,662
Reaction score
6,888
Wakati wakiaapishwa makatibu tawala wa mikoa, Mhe. Rais Samia alisikika katika hotuba yake kuwa aliwasimamisha wakuu wa mikoa na makatibu tawala hao wa mikoa ili kusoma sura zao na kubashiri yatakayotokeoa mikoani.

Alisema kwa msomi mzuri wa sociology atafahamu nini kitatokea kwa kuangalia sura zao ila nimekuwa nikijiuliza, hivi ni msomi mzuri wa sociology au psychology ndio mwenye uwezo wa kusoma tabia za watu kwa kuwasoma sura zao?

Mwenye jibu sahihi atueleze hapa? (sikiliza kwenye muda around 1:06:04).

 
Sociology inahusisha pia kusoma psychology mkuu
 
Hata kwa sociology hakuwa mbali sana maana atakuwa aliangalia personal social interaction, social development n.k
 
Tofauti kubwa kati ya sosholojia na saikolojia ni kwamba sosholojia inahusisha utafiti na uelewa wa jamii (au makundi ya watu kwa pamoja) na hasa mahusiano, hali saikolojia inalenga zaidi juu ya tabia ya mtu binafsi. Tabia ya mtu binafsi kisaikolojia hujionesha katika mwonekano wake (mavazi, umbile, kauli, nk).

Kwa kuwa sosholojia ni taaluma kuhusu mahusiano katika jamii na jamii ni watu wenye tabia tofauti, Rais SSH alikuwa sahihi.
 
Ukiunganisha sociology an saikoloji kama wananvyoziita social psychology unajihusisha na kujifunza tabia ya mtu katika kundi la watu.
 
Ni lugha tu hapo imekuchanganya ila kwa kibantu fasaha hamna tofauti na wapiga ramli
 
Back
Top Bottom