Maneno kuntu haya! Kudos!Hili swala nadhani tulifanye kuwa sisi Mkuu wetu ameamua tusitumie ile njia ya kujifungia, na ukiangalia nchi zetu hizi wananchi wake wana usugu fulani kwenye mafua.
Tatizo upande wa mkuu hakuna suluhu upande wa upinzani ni kubezwa na kuzarauliwa. Nao wanajitahidi kusisitiza kuna maana katika kujitenga.
Mashindano haya hayafai lolote, wapinzani kubezwa huku kunaweza kukitokea kweli hali ikabadilika na vifo vikajaa mitaani. Mkuu ataaibika sana,
Lakini pia kama hakutakuwa na vifo vingi na ugonjwa kupotea upinzani watabezwa na kuaibishwa sana.
Haya yote yanatija yeyote?
Ni upuuzi usio na maana yeyote kwa Mkuu na Upinzani pia, huu ni ugonjwa na janga linalo gharimu maisha ya watu. Basi upande mmoja unyamaze hasa upinzani wamesema sana basi wanyamaze.
Serikali nao wasilazimishe maana huu ugonjwa upo na unaendelea kuua watu. Wasilazimishe
mpka kuficha vifo na hali ya ugonjwa iliyopo kwa uhalisia wake. Siasa hizi zinapindukia kwenye chuki sasa na hasa vyombo vya usalama kuanza kuwakamata na kuwatesa wanao wakosoa, au kuwaambia mbadala wasioupenda wanasiasa wao, baada ya haya kuna maisha pia.
Mkuu asikimbie ofisi na majukumu yake na kwenda kujificha akiogopa ugonjwa na huku akiwahimiza wengine waendelee kufa na ugonjwa huku yeye akiwa mafichoni. Ni usaliti. Lakini wapinzani umefika wakati wa kunyamaza.
Kuna ofisi moja ingeweza kumaliza malumbano haya kama ingekuwa na watu makini na wenye ufahamu, bali hii ofisi imegeuka na kuwa haina manufaa kwa nchi na wananchi walio wachagua GENGE HILI ndiyo ofisi pekee yenye uamzi wa kumaliza shida hii. Lkn sasa ndiyo haina maana kabisa watu wake ni zero wamejazana humo kuwafirisi waTZ. Uongozi wake ni zero + zero ukiwasikiliza ni genge litakalo kumbukwa miaka mingi ijayo. Wana hira mashetani wasio na haya wamekalia kukomoana hasa kiongozi wao. Ni AJABU
SIJUI HUWA ANAVUTA BANGE KITUKO. NIWA KUOMBEA KWELI
Basi najua MUNGU ATATUOKOA na hawa watu bali walioandikiwa watakwenda wasioandikiwa watabaki.
Tuendelee kujikinga Corona ipo.
Sent using Jamii Forums mobile app
Two failled statesSiwezi kumbishia hata kidogo!
Ni ngumu sana kufanikiwa hiyo lockdown..maisha ya wengi ni ya vibarua watu wengi wanajikimu tofauti na nchi za ulaya na mabara mengine.Siyo lazima watu wote wawekwe lockdown. Kama kungekuwa na kujali, kunakuwepo na lockdown za kimkakati. Essential business kwetu zinaweza kuwa za tofauti ili kuweza kupunguza misongamano nk.
Na huko kwenye nyumba moja zaidi ya sita, ni suala la kuwa makini. Na kuhakikisha gonjwa haliingii? Ukiwa umeshafunga mipaka kwa muda na kuzuia hao watalii hata kwa siku 14, maambukizi yanakuwa siyo ya kasi, na wakati huo wale waliokutana na waathirika wanatafutwa kwa kasi.
Kajifungieni nyie na huyo Mbowe wenu.
Tumewachoka.the poorest comment since 2020 started
Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa anajitahidi kuficha uzembe wake kwa gharama kubwa sana.Huyu mtu ikitokea corona ikamfyeka,naamini naamini hata sheteni atamkataaNaona kumekuwepo na hali ya upotoshaji nchini kuwa hatua za lockdown hazina manufaa! Hili naona kama ni upotoshaji ambao unasababishwa na ukweli kwamba viongozi wengi wameingiza siasa kwenye vita dhidi ya corona na matokeo yake ndo haya ya upotoshaji pamoja na mambo mengine.
Mifano iko mingi, lakini kuna mfano nilioamuwa kuutumia kujenga hoja yangu. Mfano huu ni wa gavana wa Ohio kule marekani, anayeitwa Mike Dewine! Huyu alichukuwa hatua zote kabla ya Trump! Pamoja na kwamba Trump anaogopeka na viongozi wengi ndani ya chama chake cha republican, mfano maseneta na magavana, huwa wana wasiwasi wa kupingana naye kwasababu ya umaarufu alio nao ndani ya chama cha Tembo ama Republicans!
Sasa huyu alichukuwa hatua za lockdown toka mwanzo kabisa wakati Trump akiwa analeta utani na gonjwa hilo! Matokeo yake, jimbo lake linafanya vizuri sana na yeye amekuwa maarufu siyo tu kule Ohio, bali marekani nzima! Alikuwa na guts za kufanya maamuzi sahihi ya kulinda raia wake kuliko rais wa nchi! Na wananchi wanasema hatua hizo alitakiwa azichukuwe Trump mwenyewe, na pengine mikusanyiko iliyokuwa ikiendelea kwenye majimbo mengine mfano New York, New Orleans na kwingineko ambako michezo iliendelea kama kawaida na mikusanyiko mingine kama makanisani nk, ambapo matokeo yake ndo haya tunayoyaona wanakufa kwa kasi na maambukizi ambayo yalikuwa tayari yametapakaa.
Jimbo lake lina maambukizi machache na vifo vichache sana, na wameshaanza kufungua taratibu taratibu. Pia jimboni kwake alifanya mkakati siyo wa total lockdown, hiyo ni baadhi tu ya sehemu. Wale wanaojitetea kuwa lockdown ni mbaya, wanawaongopea wananchi kwa manufaa yao binafsi, most likely uchaguzi. Ni bora waseme lockdown siyo njia muafaka kwasababu ya mfumo wetu wa uchumi ulivyo na maisha ya wananchi wake, au pia kwamba wamechelewa kwasababu tuliendelea kupokea wageni wote hata kutoka China! Lakini haina maana kuwa partial lockdowns hazifai na wala hazikufaa! Na lockdowns kwenye maeneo korofi ni za muhimu!
Lakini pia tulipuuza tokea mwanzo na kuanza kusema wapinzani wanataka wananchi wafe na njaa! Hii ni propaganda ambayo matokeo yake si mazuri kwenye jamii inayokabiliana na janga hatari linalochukuwa maisha ya watu kila siku na pengine kila saa duniani.
Bila kupoteza muda, naweka hiki kipande hapo chini chenye kusapoti ninachokisema, pia link kama ukitaka kusoma habari yote na kujiridhisha wewe mwenyewe kuwa niyasemayo ni kweli.
Mike Dewine gavana wa Ohio, alipata umaarufu hata kumzidi Trump ambaye naye akaanzisha utaratibu wa kuongea na waandishi wa habari kila siku. Jambo ambalo Dewine alikuwa akilifanya jimboni kwake kila siku saa nane mchana, na wakati huo wana Ohio wanakuwa kwenye luninga zao wakimsikiliza. Ndiyo wakaanzisha usemi wa “it’s 2’oclock somewhere...wine with mr Dewine”, ambapo wakati wa lunch wanapata wine wakimsikiliza Dewine. Wala hawa kuwa na habari na Trump!
A Republican, he took early and bold actions to lock down his state, even as the head of his party, President Trump, dismissed the threat of the pandemic.
Ohio’s G.O.P. Governor Splits From Trump, and Rises in Popularity
Kwahiyo ndugu watanzania wenzangu, kabla ya kufanya upotoshaji, jiridhishe kwa kautafiti kadogo tu ili uweze kuwa huru kifikra! kama ikifikia mahali unamkabidhi mtu mwingine jukumu la kufikiria kwa niaba yako, ujuwe kuna shida kubwa sana kwa upande wako! Kusema lockdown haisaidii, ni sawa pia na kusema “to hell with social distancing”. Kwasababu huwezi kuwaambia watu wafuate masharti kwa ugonjwa ambao siyo hatari kabisa kwa jinsi unavyochukuliwa, kutokana na hatua za viongozi wetu, pamoja na matam
Siyo sahihi kusema lockdown haisaidii kwasababu zenu za kisiasa! Kwanza ingekuwa ni kwetu, huyo Dewine angekiona cha mtemakuni!
Lakini kwasababu ya kiasi cha demokrasia na mfumo wao wa uongozi, Dewine aliweza kuchukuwa maamuzi muhimu kwenye jimbo lake kinyume na rais wa nchi! Na ameonekana kwamba alikuwa sahihi na kiongozi shupavu!
Nyota yake inang’ara! Trump hawezi tena kusema kuwa lockdown haisaidii! Na kwetu Tanzania siyo sahihi kusema hivyo, semeni tu hamkuchagua lockdowns kwasababu mtakufa njaa, ama pia mlichelewa kuchukuwa hatua za kufunga mipaka!
Mag3 Nguruvi3 JokaKuu Kalamu1 imhotep Detective J
STOCKHOLM (Reuters) - More Swedes died in April than in any one month since 1993, figures from the Statistics Office showed on Monday, as the outbreak of the novel coronavirus pushed the death toll higher.Kuna mifano pia ya nchi ambazo hazijafanya ,,lockdown” na ziko vizuri na kufanikiwa zaidi klk zile zilizofanya, mfano Taiwan ingawaje ipo karibu kabisa na China na ni moja kati ya nchi za kwanza kabisa kushambuliwa lkn haikufanya ,,lockdown” na sasa hivi Taiwan ni success story kwenye kupambana na virusi vya corona.
Hata Sweden haikufanya lockdown na bado wametoka vizuri klk nchi zilizofanya lockdown kama Italia au Uingereza, isitoshe swala hapa siyo kwamba lockdown inasaidia au la, bali swala ni kwamba nchi nyingi hata zilizoendelea haziwezi kumudu lockdown.
Na watu wengi zaidi watakufa kutokana na madhara ya lockdown kuliko corona, wengi wamepoteza kazi, wamepoteza Health insurance, hata Afrika kwetu wanaokufa na njaa ni wengi kuliko wa corona, hiyo ndiyo argument, kwamba lockdown inaumiza zaidi kuliko kuponya, ...
Hivi Uganda wanaweza vipi?Ni ngumu sana kufanikiwa hiyo lockdown..maisha ya wengi ni ya vibarua watu wengi wanajikimu tofauti na nchi za ulaya na mabara mengine.
Hiki kirusi kipo na mbaya zaidi hakuna ajuaye lini dawa itapatikana. Kuishi kwa sasa ni mwendo wa kuchukua tahadhari.
Lugha hii siyo sahihi hata kidogo kwenye taifa la watu wenye kujielewa.
Leo nimemsikiliza rais wa Uganda nikashangazwa sana na utofauti uliopo kati yao na sisi. Daah! Hivi Mbona hao wameweza lockdown? Wale wamefunga hadi makanisa na misikiti!
#KIMATAIFA:Idadi ya maambukizi ya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 912 , huku nchi hiyo ikithibitisha kuwanyima kibali cha kuingia nchini Kenya madereva 51 raia wa Tanzania waliopatikana na Virusi vya Corona. ITV on Twitter
Hivi zile fujo za Kenya watu wa Nairobi kugombana na polisi sababu yake ni nini?.Hivi Uganda wanaweza vipi?
Mkuu, nimeishia hapo kuisoma mada yako.
Kiufupi, "Lockdown" ukisikiliza anavyoielezea Magufuli utajua kwamba, huenda hajui maana yake ni nini, au anatoa maelezo tofauti kabisa na maana halisi ya 'lockdown' na kwa nini inatumika sehemu nyingi duniani.
Lakini moja kwa moja, ukiunganisha mambo mengi anayoyaweka Rais kwenye hotuba zake kuhusu COVID-19, moja kwa moja utajua wazi kwamba yote yanafanywa kipotoshaji maksudi kabisa kwa sababu zake mwenyewe.
Kwa mfano: 'Lockdown' haina maana kwamba watu huko vijijini wasiende mashambani kulima. Hata huko kwingine kuliko na 'lockdown' sehemu ambazo hakuna misongamano ya watu shughuli zinaendelea kama kawaida.
Hakuelewa, au anapotosha maksudi maana na manufaa ya 'lockdown'. Kupotosha maksudi kunaungwa mkono na mambo mengine anayoingiza kwenye hotuba zake.
Halafu anajichanganya sana, tena nadhani maksudi akidhani watu anaohutubia hawaelewi.
Hao watalii waliojaza ndege hadi August wanatoka wapi, na hizo ndege zitakazokuja Tanzania ni za wapi? China labda?
Na bado anaendelea na vita:Anadhani kuna watu mahali fulani wapo wanategeshea kutuambukiza waTanzania kwa maksudi mazima na COVID-19!
Hawa watu tuliwakosea kitu gani?
Hivi zile fujo za Kenya watu wa Nairobi kugombana na polisi sababu yake ni nini?.
Marekani vifo vinakaribia laki moja na bado watu wanataka kutoka nje wakafanye shughuli zao za kila siku.
Kanisa kuu la Roma linafunguliwa licha ya Italia kuwa na vifo vingi.
Na wewe tumia akili ya kawaida tu, hapa kwetu shughuli zinaendea lakini ni kwa tahadhari.Tumia akili yako basi japo kidogo. Italia na nchi nyingine wanarudi kwenye maisha ya kawaida (lakini kukiwa na masharti makali) baada ya hali kuwa nzuri. Kwa uelewa wako maambukizi mapya Italia ni kiasi gani leo?
Na wewe tumia akili ya kawaida tu, hapa kwetu shughuli zinaendea lakini ni kwa tahadhari.
Anga limefunguliwa lakini masharti ya afya yamepewa msisitizo.
Ni akili za kitumwa kujaribu kufanya kila kitu anachokifanya mzungu pasipo wewe mwenyewe kujiongeza.