Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Naona kumekuwepo na hali ya upotoshaji nchini kuwa hatua za lockdown hazina manufaa! Hili naona kama ni upotoshaji ambao unasababishwa na ukweli kwamba viongozi wengi wameingiza siasa kwenye vita dhidi ya corona na matokeo yake ndo haya ya upotoshaji pamoja na mambo mengine.

Mifano iko mingi, lakini kuna mfano nilioamuwa kuutumia kujenga hoja yangu. Mfano huu ni wa gavana wa Ohio kule marekani anayeitwa Mike Dewine! Huyu alichukuwa hatua zote kabla ya Trump! Pamoja na kwamba Trump anaogopeka na viongozi wengi ndani ya republican mfano maseneta na magavana, huwa wana wasiwasi kupingana naye kwasababu ya umaarufu alio nao ndani ya chama cha Tembo ama Republicans!

Sasa huyu alichukuwa hatua za lockdown toka mwanzo kabisa wakati Trump akiwa analeta utani na gonjwa hilo! Matokeo yake, jimbo lake linafanya vizuri sana na yeye amekuwa maarufu siyo tu kule Ohio, bali marekani nzima! Alikuwa na guts za kufanya maamuzi sahihi ya kulinda raia wake kuliko rais wa nchi! Na wananchi wanasema hatua hizo alitakiwa azichukuwe Trump mwenyewe, na pengine mikusanyiko iliyokuwa ikiendelea kwenye majimbo mengine mfano New York, New Orleans na kwingineko ambako michezo iliendelea kama kawaida na mikusanyiko mingine kama makanisani nk, ambapo matokeo yake ndo haya tunayoyaona wanakufa kwa kasi na maambukizi ambayo yalikuwa tayari yametapakaa.

Jimbo lake lina maambukizi machache na vifo vichache sana, na wameshaanza kufungua taratibu taratibu. Pia jimboni kwake alifanya mkakati siyo wa total lockdown, hiyo ni baadhi tu ya sehemu. Wale wanaojitetea kuwa lockdown ni mbaya, wanawaongopea wananchi kwa manufaa yao binafsi, most likely uchaguzi. Ni bora waseme lockdown siyo njia muafaka kwasababu ya mfumo wetu wa uchumi ulivyo na maisha ya wananchi wake, lakini haina maana kuwa partial lockdowns hazifai. Na lockdowns kwenye maeneo korofi. Lakini pia tulipuuza tokea mwanzo na kuanza kusema wapinzani wanataka wananchi wafe na njaa! Hii ni propaganda ambayo matokeo yake si mazuri kwenye jamii inayokabiliana na janga hatari linalochukuwa maisha ya watu kila siku na pengine kila saa duniani.

Bila kupoteza muda, naweka hiki kipande hapo chini chenye kusapoti ninachokisema, pia link kama ukitaka kusoma habari yote na kujiridhisha wewe mwenyewe kuwa nisemayo ni kweli.

Mike Dewine gavana wa Ohio, alipata umaarufu hata kumzidi Trump ambaye naye akaanzisha utaratibu wa kuongea na waandishi kila siku, jambo ambalo Dewine alikuwa akilifanya jimboni kwake kila siku saa nane mchana, na wakati huo wana Ohio wanakuwa kwenye luninga zao wakimsikiliza. Ndiyo wakaanzisha usemi wa “it’s 2’oclock somewhere...wine with mr Dewine”, ambapo wanapata wine wakimsikiliza Dewine. Wala hawa kuwa na habari na Trump!

A Republican, he took early and bold actions to lock down his state, even as the head of his party, President Trump, dismissed the threat of the pandemic.

Ohio’s G.O.P. Governor Splits From Trump, and Rises in Popularity

Kwahiyo ndugu watanzania wenzangu, kabla ya kufanya upotoshaji, jiridhishe kwa kautafiti kidogo tu ili uweze kuwa huru kifikra! Ikifkia mahali unamkabidhi mtu mwingine afikirie kwa niaba yako, ujuwe kuna shida kubwa sana! Kusema lockdown haisaidii, ni sawa pia na kusema “to hell with social distancing”. Huwezi kuwaambia watu wafuate masharti kwa ugonjwa ambao siyo hatari kabisa kwa jinsi unavyochuliwa kutokana na hatua za viongozi wetu.

Siyo sahihi kusema lockdown haisaidii kwasababu zenu za kisiasa! Kwanza ingekuwa ni kwetu, huyo Dewine angekiona cha mtemakuni! Lakini kwasababu ya kiasi cha demokrasia na mfumo wao wa uongozi, Dewine aliweza kuchukuwa maamuzi muhimu kwenye jimbo lake kinyume na rais wa nchi! Na ameonekana kwamba alikuwa sahihi na kiongozi shupavu! Nyota yake inang’ara! Trump hawezi tena kusema kuwa lockdown haisaidii! Na Tanzania siyo sahihi kusema hivyo, semeni tu hamkuchagua lockdowns kwasababu mtakufa njaa.

Mag3 Nguruvi3 JokaKuu Kalamu1 imhotep Detective J
The topic is long overdue! No lockdown.
 
Mkuu sijui umetumia creteria gani kuifananisha Rwanda yenye 12.3m populationa na eneo la 26,338 km2 wakati population na TZ ina yenye 56+m na eneo la 947,303 km2 zaidi ya mara 35 kuilinganisha na Rwanda.... Kiuchumi kwa maana ya mtu mmoja mmoja wanakipato kizuri kuliko Tanzania ambao mlo wao mpaka mtu atoke aonane na mtu ili ale. Serikali imechukuq hatua na inaendelea kuhamasisha sana kupitia media... Mwitikio upo na tutafanikiwa
Rwanda ni kama mkoa tu. Kwani wagonjwa si walianzia Dar baada ya kuacha kuzuia wanaoingia? Lockdown haikutakiwa iwe ya nchi nzima! Rwanda yote tunaweza kuilisha sisi, ndo iwe Dar?

Kuhamasisha nina sapoti kabisa! Ila na hatua zichukuliwe!
 
The topic is long overdue! No lockdown.
Sawa, take responsibility and do what is needed! Kwani bado hakuna hatua za kuchukua kuzuia usambaaji wa kasi? Kwanza takwimu zenyewe ni siri! Mnasema mnafungua vitu wakati hamkuvifunga.

Unakumbuka Mzee Mwanakijiji aliuliza kama “Bahati nasibu ya Maghufuli italipa”?
 
Chanjo ya corona inaweza kupatikana mwaka mmoja ujao.

Mtihani ni namna ya watu kuishi ndani ya muda wote huo wakati chanjo au dawa ikisubiriwa.

Familia zetu za kiafrika ni zile za nyumba moja kuwa na watu zaidi ya sita wakitumia kwa pamoja vitu kama vyoo na majiko, hiyo lockdown inaweza kuongeza maambukizi badala ya kuyapunguza.
 
Rwanda ni kama mkoa tu. Kwani wagonjwa si walianzia Dar baada ya kuacha kuzuia wanaoingia? Lockdown haikutakiwa iwe ya nchi nzima! Rwanda yote tunaweza kuilisha sisi, ndo iwe Dar?

Kuhamasisha nina sapoti kabisa! Ila na hatua zichukuliwe!
Anyway kuweka record sawa mgonjwa wa kwanza alipatikania Arusha baada ya kutua pale na Rwandaair then wakaja wale waitaliano wa Zanzibar akaja meneja wa Mondi, Mwana FA... nakuendelea. Dar ina zaidi ya 6.5m population haina chakula cha kujilisha inapokea toka nchi nzima na inasambaza mahitaji mengine nchi nzima kama inavyopokea... Kubwa nakuelewa msisitizo wako hata Kama sikubaliani nao. Lockdown ni janga kuliko Covid19 kwa nchi yetu.
 
Kuna mifano pia ya nchi ambazo hazijafanya ,,lockdown” na ziko vizuri na kufanikiwa zaidi klk zile zilizofanya, mfano Taiwan ingawaje ipo karibu kabisa na China na ni moja kati ya nchi za kwanza kabisa kushambuliwa lkn haikufanya ,,lockdown” na sasa hivi Taiwan ni success story kwenye kupambana na virusi vya corona.

Hata Sweden haikufanya lockdown na bado wametoka vizuri klk nchi zilizofanya lockdown kama Italia au Uingereza, isitoshe swala hapa siyo kwamba lockdown inasaidia au la, bali swala ni kwamba nchi nyingi hata zilizoendelea haziwezi kumudu lockdown.

Na watu wengi zaidi watakufa kutokana na madhara ya lockdown kuliko corona, wengi wamepoteza kazi, wamepoteza Health insurance, hata Afrika kwetu wanaokufa na njaa ni wengi kuliko wa corona, hiyo ndiyo argument, kwamba lockdown inaumiza zaidi kuliko kuponya, ...
Hebu acheni ushirikina wenu, nchi gani ambayo watu wake wengi wamekufa sana kwa lockdown kuliko corona.
 
Chanjo ya corona inaweza kupatikana mwaka mmoja ujao.

Mtihani ni namna ya watu kuishi ndani ya muda wote huo wakati chanjo au dawa ikisubiriwa.

Familia zetu za kiafrika ni zile za nyumba moja kuwa na watu zaidi ya sita wakitumia kwa pamoja vitu kama vyoo na majiko, hiyo lockdown inaweza kuongeza maambukizi badala ya kuyapunguza.
Lockdown kwa Tanzania ingeleta madhara makubwa
Kwa hyo naipa big up serikali kuto weka lockdown

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Anyway kuweka record sawa mgonjwa wa kwanza alipatikania Arusha baada ya kutua pale na Rwandaair then wakaja wale waitaliano wa Zanzibar akaja meneja wa Mondi, Mwana FA... nakuendelea. Dar ina zaidi ya 6.5m population haina chakula cha kujilisha inapokea toka nchi nzima na inasambaza mahitaji mengine nchi nzima kama inavyopokea... Kubwa nakuelewa msisitizo wako hata Kama sikubaliani nao. Lockdown ni janga kuliko Covid19 kwa nchi yetu.
Dar siyo wote wangehitaji msaada wa chakula mkuu. Na kama ni hivyo, hapo ndo lockdown ingewekwa kwa siku 14 huku contacts zikiwa traced! At the same time, zuia watu kuingia kama hakuna hatua madhubuti za kuwapima nk.
 
Lockdown kwa Tanzania ingeleta madhara makubwa
Kwa hyo naipa big up serikali kuto weka lockdown

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Lockdown kwa Tanzania ama kwa Dar? Pia kumbe unasapoti suala la wachina kuachiwa kuingia na wageni kwa kisingizio cha uchumi ama njaa?
 
#KIMATAIFA:Idadi ya maambukizi ya Corona nchini Kenya imeongezeka na kufikia 912 , huku nchi hiyo ikithibitisha kuwanyima kibali cha kuingia nchini Kenya madereva 51 raia wa Tanzania waliopatikana na Virusi vya Corona. ITV on Twitter
 
Hivi Kenya wametupita?
 
Chanjo ya corona inaweza kupatikana mwaka mmoja ujao.

Mtihani ni namna ya watu kuishi ndani ya muda wote huo wakati chanjo au dawa ikisubiriwa.

Familia zetu za kiafrika ni zile za nyumba moja kuwa na watu zaidi ya sita wakitumia kwa pamoja vitu kama vyoo na majiko, hiyo lockdown inaweza kuongeza maambukizi badala ya kuyapunguza.
Siyo lazima watu wote wawekwe lockdown. Kama kungekuwa na kujali, kunakuwepo na lockdown za kimkakati. Essential business kwetu zinaweza kuwa za tofauti ili kuweza kupunguza misongamano nk.

Na huko kwenye nyumba moja zaidi ya sita, ni suala la kuwa makini. Na kuhakikisha gonjwa haliingii? Ukiwa umeshafunga mipaka kwa muda na kuzuia hao watalii hata kwa siku 14, maambukizi yanakuwa siyo ya kasi, na wakati huo wale waliokutana na waathirika wanatafutwa kwa kasi.
 
Back
Top Bottom