Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Point yako ni nini sasa? Ulichoandika hapa kina uhusiano gani na nilichoandika?
Kwa nini mnatumia nguvu nyingi kutetea tafsiri yenu ya lockdown (ambayo HAKUNA hata nchi moja duniani ilifanya)?
Lockdown haiwezi kufanyika nchi nzima ikasimama. Uchumi wa nchi nzima utayumba na ule wa mtu mmoja mmoja ndio utateketea kabisa.

Marekani watu milioni 30 wamepoteza ajira sasa jiulize kwetu hapa hali itakuwa vipi.
 

Tuna Rais muongo mno. Halafu kuhalalisha uongo wake, anatangaza kuwa hawezi kusema uongo akiwa madhabahuni lakini immediately anaanza kuongopa mchana kweupe pee! Eti "kuna mashirika ya ndege siwezi kuyataja yamejaza bookings za kuja Tanzania..."!!!
 
Lockdown haiwezi kufanyika nchi nzima ikasimama. Uchumi wa nchi nzima utayumba na ule wa mtu mmoja mmoja ndio utateketea kabisa.

Marekani watu milioni 30 wamepoteza ajira sasa jiulize kwetu hapa hali itakuwa vipi.

Hivi wewe mtu unaelewa hoja ya muanzisha thread na kinachopaswa kujadiliwa kwenye thread hii?
Well ni hivi: lockdown haina maana ya kufungia kila mtu nchi nzima na kuzuia watu kufanya kazi. HAKUNA nchi hata moja iliyofungia watu ndani kwenye full au partial lockdown. Kazi zote muhimu zimekuwa zinafanyika, umeelewa sasa?
 
Hivi tunavyoongea shule za msingi zimefungwa huu ni mwezi wa pili, hiyo ni lockdown maalum.

Michezo pia imesimamishwa hiyo ni lockdown lakini shughuli nyingine za kiuchumi zinaendelea kama kawaida.

Nchi ya dunia ya tatu huwezi kuwa na lockdown kama zile za mataifa makubwa.
 
Lockdown kwajamii yetu haisaidii. Hapa madereva bodaboda, mama ntilie, wakulima na wafugaji watakula wap?
Maana wao wanataka nikutafuta na kula bac.
Hizo habali zenu wapelekee Kenya

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Umeamua kujibishia mwenyewe? Kila la heri.
 
Magufuli na ccm wanajua kuwa Watanzania wengi ni wajinga kwa hiyo wanaweza kuwaambia kitu chochote however ridiculous na wakakiamini. Ila nina mashaka kama Jiwe kweli anajua maana halisi ya lockdown.
Umetuweza kweli. Yaani sisi ni wajinga. SIku za nyumba nilisikia kwamba eti Raisi Kenyata alisema Raisi Nyerere anatawala (malizia) na yeye anatawala (malizia) ndiyo maana Kenyata alikuwa na kazi ngumu kuwatawala Wakenya lakni yeye Rais Nyerere alikuwa hapati ugumu kutawala watanzania. Kwa hiyo bwana mkubwa kwa vile sisi n wajinga ndiyo maana tunatawaliwa. Tusaidie angalau mikakati ya kujiondoa na huu ujinga maana kama ni shule wapo wanye PHD lakini wanajiita wameokotwa jalalani. Wapo wenye PHD wanajikomba wapate vyeo. Sasa kama hata shule haisaidii kufuta ujinga tufanyeje angalau watoto wetu waondokane na huo ujinga.
 
Hata kama wanafungua huku kuna vifo vingi, haina maana kwamba kufunga hakujawasaidia kuokoa maisha ya wananchi.

Hao wa marekani wanaotaka kutoka nje ni wachache sana!group dogo sana la mashabiki wa Trump.

Wenzenu wakifungua hata kama vifo vingi, ni kwasababu ya kosa la kuchelewa kufunga, lakini siyo kwasababu ya kufunga. Common sense yenyewe ingetosha.
 
Fujo za watu wa Kenya kule East leagh? Wanakoishi wasomali?Uganda na Rwanda umezisahau. Kama Rwanda wamelisha nchi sisi tumeshindwa vipi kuilisha Dar? Tena siyo wote Dar ambao wangehitaji msaada.
 
Ni sahihi kabisa mkuu, kila mtu apambane na hali yake. Anayetaka kujifungia ajifungie anayetaka kutoka atoke.
Hapo ni sawa kabisa na serikali kukabiliana na corona? Kwahiyo hapo wewe unajiskia huru kweli kweli 🤦🏾‍♂️. Kumbe ni uhuru wa either kutafuta kifo au kuugua na kusambaza virusi.

Uhuru wa kukosoa wenyewe hamna, lakini uhuru wa kupata corona mnao. Ama kweli kuishi kwingi ni kuona mengi!
Nguruvi3
 

Kwa kuanzia, tuanze kuhoji tunachoambiwa badala ya kukubaliana na kila kitu. Ila tuwe tayari kulipa gharama ya kusimamia ukweli.
 
Magufuli anasema Hofu ndio inauwa sana kuliko corona kwa hiyo Lockdown haitasaidia

Swali langu kwenye cheti cha kifo je sababu inaandikwa "Hofu" ?
Hata mwenye HIV akifa huwezi kuta sababu ya kifo kuwa HIV, HIV inapelekea mwenye virusi kufa kwa matatizo ya mapafu n.k. Hivyo mshtuka (hofu) hupelekea mtu kufa kwa shinikizo la damu au kushindwa kwa moyo. Tafakari
 
Hata mwenye HIV akifa huwezi kuta sababu ya kifo kuwa HIV, HIV inapelekea mwenye virusi kufa kwa matatizo ya mapafu n.k. Hivyo mshtuka (hofu) hupelekea mtu kufa kwa shinikizo la damu au kushindwa kwa moyo. Tafakari
Kwa hiyo dawa ya hofu nayo ni kujifukiza?
 
Critics zitatoka nyingi lakini Kwa hili Raisi JPM ni mfano wa dunia, shida tu ni Raisi toka Africa tena Tanzania. Ingekua ni mweupe basi angekua kwenye headlines na promo kibao.

Karata alizo changa Raisi wetu kuchangua clinical approach badala ya epidemiological approach ndo tofauti kuu.
After all Raisi wetu ni mwanasayansi, jiulize ni Maraisi wangapi duniani ni wanasayansi na wanaelimu ya maabara.

JPM is the right president for our nation
especially at this era. Period. Kila Jambo na nyakati zake.
 

Rais wa Brazil nae ni mweusi au anatoka Africa? Mbona nae anakosolewa kwa kufanya ujinga kama anaoufanya Jiwe tu?
But you are right; Magufuli ni mfano duniani. Mtu akitaka kujua ni kipi kisichotakiwa kufanywa au kusemwa basi standard unit ni kuangalia kinachosemwa au kufanywa na Magufuli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…