Naona kumekuwepo na hali ya upotoshaji nchini kuwa hatua za lockdown hazina manufaa! Hili naona kama ni upotoshaji ambao unasababishwa na ukweli kwamba viongozi wengi wameingiza siasa kwenye vita dhidi ya corona na matokeo yake ndo haya ya upotoshaji pamoja na mambo mengine.
Mifano iko mingi, lakini kuna mfano nilioamuwa kuutumia kujenga hoja yangu. Mfano huu ni wa gavana wa Ohio kule marekani anayeitwa Mike Dewine! Huyu alichukuwa hatua zote kabla ya Trump! Pamoja na kwamba Trump anaogopeka na viongozi wengi ndani ya republican mfano maseneta na magavana, huwa wana wasiwasi kupingana naye kwasababu ya umaarufu alio nao ndani ya chama cha Tembo ama Republicans!
Sasa huyu alichukuwa hatua za lockdown toka mwanzo kabisa wakati Trump akiwa analeta utani na gonjwa hilo! Matokeo yake, jimbo lake linafanya vizuri sana na yeye amekuwa maarufu siyo tu kule Ohio, bali marekani nzima! Alikuwa na guts za kufanya maamuzi sahihi ya kulinda raia wake kuliko rais wa nchi!
Jimbo lake lina maambukizi machache na vifo vichache sana, na wameshaanza kufungua taratibu taratibu. Pia jimboni kwake alifanya mkakati siyo wa total lockdown, hiyo ni baadhi tu ya sehemu. Wale wanaojitetea kuwa lockdown ni mbaya, wanawaongopea wananchi kwa manufaa yao binafsi, most likely uchaguzi. Ni bora waseme lockdown siyo njia muafaka kwasababu ya mfumo wetu wa uchumi ulivyo na maisha ya wananchi wake, lakini haina maana kuwa partial lockdowns hazifai. Na lockdowns kwenye maeneo korofi.
Bila kupoteza muda, naweka hiki kipande hapo chini chenye kusapoti ninachokisema, pia link kama ukitaka kusoma habari yote na kujiridhisha wewe mwenyewe kuwa nisemayo ni kweli.
Mike Dewine gavana wa Ohio, alipata umaarufu hata kumzidi Trump ambaye naye akaanzisha utaratibu wa kuongea na waandishi kila siku, jambo ambalo Dewine alikuwa akilifanya jimboni kwake kila siku saa sita mchana, na wakati huo wana Ohio wanakuwa kwenye luninga zao wakimsikiliza. Ndiyo wakaanzisha usemi wa it’s “12’oclock somewhere...wine with mr Dewine”, ambapo wanapata wine wakimsikiliza Dewine. Wala hawa kuwa na habari na Trump!
A Republican, he took early and bold actions to lock down his state, even as the head of his party,
President Trump,
dismissed the threat of the pandemic.
Ohio’s G.O.P. Governor Splits From Trump, and Rises in Popularity
Kwahiyo ndugu watanzania wenzangu, kabla ya kufanya upotoshaji, jiridhishe kwa kautafiti kidogo tu ili uweze kuwa huru kifikra! Ikifkia mahali unamkabidhi mtu mwingine afikirie kwa niaba yako, ujuwe kuna shida kubwa sana! Kusema lockdown haisaidii, ni sawa pia na kusema “to hell with social distancing”. Huwezi kuwaambia watu wafuate masharti kwa ugonjwa ambao siyo hatari kabisa kwa jinsi unavyochuliwa kutokana na hatua za viongozi wetu.
Siyo sahihi kusema lockdown haisaidii kwasababu zenu za kisiasa! Kwanza ingekuwa ni kwetu, huyo Dewine angekiona cha mtemakuni! Lakini kwasababu ya kiasi cha demokrasia na mfumo wao wa uongozi, Dewine aliweza kuchukuwa maamuzi muhimu kwenye jimbo lake kinyume na rais wa nchi! Na ameonekana kwamba alikuwa sahihi na kiongozi shupavu! Nyota yake inang’ara! Trump hawezi tena kusema kuwa lockdown haisaidii! Na Tanzania siyo sahihi kusema hivyo, semeni tu hamkuchagua lockdowns kwasababu mtakufa njaa.
Mag3 Nguruvi3 JokaKuu Kalamu1 imhotep Detective J