Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Hakuna nchi ambayo haitaabiki na corona Ulaya, lkn waliofanya lockdown hawako vizuri zaidi kuliko waliofanya ndicho nilichomaanisha, na kama una ushahidi kwamba Sweden imeathirika zaidi na corona kuliko nchi nyingine za Ulaya, karibu uweke hapa, ...
Hata akili ya kujiongeza huna si Google tu andika Nchi inayotaabika kwa virus vya Corona Scandinavia halafu rudi humu unipe mrejesho.. Mpaka leo wana visa 29 elfu plus na mavifo kibao na bado hawajafika kwenye peak, mind you Nchi ina watu million 10 tu.. Akili za kuambiwa amesema mwenyewe leo huko Chato kwa hiyo na wewe changanya na za kwako pia
 
.........Ni bora waseme lockdown siyo njia muafaka kwasababu ya mfumo wetu wa uchumi ulivyo na maisha ya wananchi wake, lakini haina maana kuwa partial lockdowns hazifai.


............Na Tanzania siyo sahihi kusema hivyo, semeni tu hamkuchagua lockdowns kwasababu mtakufa njaa.

Mag3 Nguruvi3 JokaKuu Kalamu1 imhotep Detective J

Dah....hivi huwa mnasoma nyuzi zenu wenyewe au mnatiririka tu? [emoji44]

Sent using Beretta ARX 160
 
Mkuu nashukuru kwa nondo za ukweli. Wape makavu! Saafi sanaa!
Issue hii ya coronavirus, Rais Magufuli ameonyesha udhaifu mkubwa sana katika uongozi, lakini bado kuna watu wanashangilia.

Kiongozi anasimama na kueleza raia zake waziwazi kwamba kwake kipaumbele chake ni "uchumi" na sio kulinda maisha ya wananchi hao, halafu bado watu hao hao wakabaki wanashangilia?

Hii inashangaza na kusikitisha sana.

Ndio, wakati wa njaa, kiongozi anaweza akahimiza watu wajitahidi walime ili wasife njaa, na hata kuwatishia kuwa hawapi msaada wa chakula, hata kama hilo linaweza kuwa tishio tu..., lakini wakati wa janga la ugonjwa usiojulikana kabisa, bado unaamini tu kuwa wewe ni tofauti na watu wengine wote duniani?

Uongoziwa aina hii unayo kasoro kubwa zaidi.

Bado hatujui sababu hasa zinazosababisha mlipuko wa ugonjwa huu katika nchi zetu hizi za Kiafrika ni tofauti na huko kwingineko; lakini tayari tunaanza kujisifu kwa sala..., kwa Mungu kutupenda sana sisi kuliko hao wengine?
 
Lockdown sio lazima ufunge kila kitu.
Mikusanyiko ya Baa,mikusanyiko ya makanisa na misikiti,sherehe,mikusanyiko ya siasa hii yote ingeweza kuzuiliwa bila kuathiri maisha.
Hivi mnavyofananisha Ohio na Mikoa Masikini ya Tanzania huwa mnafikilia kwa kutumia Nini?
Tanzania hii kwa Mfano Dar es salaam, zaidi ya 50% Wakazi wake ni wale wanaotoka asubuhi kubaingiza jioni arudi na chochote kwa Familia, ukimfungia kwa week 3 asitoke nje atakula nini na Watoto?

Tuache Ubinafsi, mimi siipendi CCM, kuna baadhi ya mambo sikubaliani na Mh. Rais ila katika hili nam support 1,000%

Hatutaki Lockdown, but stay safe, Vaa PPE na Mwisho wa siku lazima maisha yaende!
 
Watanzania tuna shida kubwa sana yaani Kiongozi anasema yeye Uchumi kwake ndiyo priority namba moja swala maisha ya watu baadaye halafu kuna mazwazwa yanapiga makofi 🤣🤣🤣🤣
 
Hata kama hawajatangaziwa lockdown, wanamudu social distancing na mikusanyiko hakuna! Msiwapotoshe watanzania kwa tamaa za madaraka!

Lockdown ni ngumu zaidi na inahitaji nidhamu zaidi ili ilete matokeo chanya, pichani ni India kwenye lockdown maambukizi yamezidi hata baada ya lockdown na Serikali imeongeza muda wa lockdown kama Kenya
1589745130817.jpeg
 
Hata akili ya kujiongeza huna si Google tu andika Nchi inayotaabika kwa virus vya Corona Scandinavia halafu rudi humu unipe mrejesho.. Mpaka leo wana visa 29 elfu plus na mavifo kibao na bado hawajafika kwenye peak, mind you Nchi ina watu million 10 tu.. Akili za kuambiwa amesema mwenyewe leo huko Chato kwa hiyo na wewe changanya na za kwako pia


Nimeomba chanzo, hizo namba umezipata wapi?
 
Wakati wa hotuba yake kanisani leo Raisi aliuliza jina la Askofu akaambiwa jina lake ni "Mshahara" akacheka sana na akastuka kuuliza ubini wake mimi nikahisi alifikiri wamemseti ili alifikiri watamwambia ubini wa askofu ni "Nyongeza" Hahahaa
 
Lkn mbona tofauti siyo kubwa sana, ukichukulia kwa mfano population ya Sweden ni mara mbili ya Denmark, na Denmark ulikuwa na lockdown?
😂😂😂😂 Umetaka data nimekupa sasa unaniuliza tena mimi maswali, Dada chukua tahadhari Corona inaua
 
Lockdown sio lazima ufunge kila kitu.
Mikusanyiko ya Baa,mikusanyiko ya makanisa na misikiti,sherehe,mikusanyiko ya siasa hii yote ingeweza kuzuiliwa bila kuathiri maisha.
Well said!👍🏽👏🏽
 
Nchi hii haina Uwezo huo wa kuwagawia Raia chakula..... Hilo moja.

Pili.
Huwa kuna baadhi ya Maeneo huwa na njaa na Serikali hupeleka chakula cha msaada, I hope unajua Kile kinachotokea!
Awamu iliyopita kwenye njaa wananchi walikua wanauziwa msosi na ghala la taifa la chakula Kg.1 ya mahindi kwa Tsh 50 (Tsh. Hamsin tu) ila kwenye awamu hii hao jamaa wa ghala la taifa wameambiwa wajiendeshe kibiashara.

Sijui jamaa wa ghala la taifa wakiambiwa wagawe chakula bure kwenye lockdown kama wana uwezo huo.
 
Eritrea hawajapiga lockdown na wamemaliza ugonjwa .. lockdown sio tiba ya corona ni njia ya kupunguza maambukizi kama ilivyo kuosha mikono kwa sabuni na maji


It is never too late to begin. Start now
Nitakusahihisha hapa. Waliimplement lockdown for 21 days. Na hili hata rais wa nchi yao alilitolea ufafanuzi.
Tofauti ni kuwa wao waliingia lockdown mapema kabla hali haijawa mbaya.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom