Hivi ni nani anawadanganya watanzania kuwa lockdown haifanyi kazi? Hata kama tumeigomea, tuache kupotoshana!

Kiujumla, unapokubali ku"-stay safe", tayari umekwishajiwekea 'lockdown' kiaina. 'Measures' zoote za ku'stay'safe' zinahimizwa kufuatwa katika lockdown' ya aina zote.
 
Unadhani kwa nini Rwanda inagawa Chakula kwa Raia wake kipindi hiki cha Lockdown?
Haya unasema kugawa chakula Rwanda, na hapo hapo unaona Dar hawawezi kugawa chakula huku sisi wenyewe tukijigamba kulisha mataifa mengine.
Kwa hiyo ni bora zaidi ku'risk' maisha ya watu wetu kuliko kuyaokoa kwa kuwagawia chakula ambacho tunao uwezo nacho?
 
Hivi mbona watu waongo sana 😂😂😂 Sweden wanafanya vizuri wakati wenzako wanataabika huko na ndiyo wanaongoza kwa vifo kwa Nchi za Scandinavia, Italy walifanya baada ya mambo kuchacha same as UK alitaka kujaribu mbinu ya ndugu yako ikalipuka walivyokuja kupata akili ikawa too late. Vipi Brazil mbona hamuitaji na walijigamba kuwa Corona mafua tu sasa hivi chamoto wanakipata. Tuombe Mungu atuepushie hichi kikombe ila tusitake kujaribu kupotosha watu kwa mfano ya uongo na kijinga
 
Kiujumla, unapokubali ku"-stay safe", tayari umekwishajiwekea 'lockdown' kiaina. 'Measures' zoote za ku'stay'safe' zinahimizwa kufuatwa katika lockdown' ya aina zote.
Unaweza kwenda kwenye shughuri zako za kila siku bila kuwa Under Lockdown na Uka stay safe.....
 
Wewe si ndiye umetolea mifano ya Sweden na Taiwan? Kwa taarifa yako, hata kule wanakoanza kufungua sasahivi, bado wanajali kuhusu social distancing! Hata wakifungua, wanahakikisha kuwa namba ya watu wanaoingia ni idadi ambayo inaruhusu social distancing, yani kunakuwa hakuna msongamano. Hayo ni mambo yanayohitaji uongozi na mikakati.
 
Unaweza kwenda kwenye shughuri zako za kila siku bila kuwa Under Lockdown na Uka stay safe.....
Ndipo hapa naona wengi wanataka kupotosha wananchi kwasababu za kisiasa! Kwasababu sasahivi naona ni kama “hakuna corona”, na watu hawachukui hatua. Kumuiga Trump kwa kuacha kuvaa barakoa nayo ni makosa makubwa kabisa.
 
Mkuu nashukuru kwa nondo za ukweli. Wape makavu! Saafi sanaa!
 
Nchi hii haina Uwezo huo wa kuwagawia Raia chakula..... Hilo moja.

Pili.
Huwa kuna baadhi ya Maeneo huwa na njaa na Serikali hupeleka chakula cha msaada, I hope unajua Kile kinachotokea!
 
Tanzania raha ,tunaongozwa na kiongozi mwenye akili na uwezo mkubwa sanaa..... thanks God

CCM DAMUDAMU!!!,CHAMA CHA MAMA &BABA
 

Hakuna nchi ambayo haitaabiki na corona Ulaya, lkn waliofanya lockdown hawako vizuri zaidi kuliko waliofanya ndicho nilichomaanisha, na kama una ushahidi kwamba Sweden imeathirika zaidi na corona kuliko nchi nyingine za Ulaya, karibu uweke hapa, ...
 
Eritrea hawajapiga lockdown na wamemaliza ugonjwa .. lockdown sio tiba ya corona ni njia ya kupunguza maambukizi kama ilivyo kuosha mikono kwa sabuni na maji


It is never too late to begin. Start now
 


Nimetoa hiyo mifano baada ya kusoma ulichoandika na wewe kutumia mifano ya Ohio, USA kutaka kuhalalisha lockdown TZ, ...
 
Lockdown, begins with you

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kwenda kwenye shughuri zako za kila siku bila kuwa Under Lockdown na Uka stay safe.....
Ndiyo, inawezekana..., hakuna anayelikataa hilo.
Upotoshaji ni hapo mnaposisitiza kuwa maana ya lockdown ni kusitisha shughuli zote. Hii siyo kweli

Na ni mhimu kujua maana ya kuweka 'lockdown' ni nini. Sisi tunakataa tu bila hata ya kuelewa 'lockdown' inakusudia kufanya nini.

Sio swala la kuzuia tu watu wasitoke nje, au wasifanye shughuli zozote wakiwa wanafuata maelekezo yote ya kuzuia maambukizi.

Sisi tunahimiza watu waende makanisani, huku tukifunga shule zote. Hapo huone 'contradiction' yoyote na kuonyesha kwamba tunaamua tu kufanya yanayotupendeza bila hata ya kuweka fikra nyuma yake?
 
Nimetoa hiyo mifano baada ya kusoma ulichoandika na wewe kutumia mifano ya Ohio, USA kutaka kuhalalisha lockdown TZ, ...
Hata kama hawajatangaziwa lockdown, wanamudu social distancing na mikusanyiko hakuna! Msiwapotoshe watanzania kwa tamaa za madaraka!
 
Nchi hii haina Uwezo huo wa kuwagawia Raia chakula..... Hilo moja.

Pili.
Huwa kuna baadhi ya Maeneo huwa na njaa na Serikali hupeleka chakula cha msaada, I hope unajua Kile kinachotokea!
Hapana.
Hilo moja, sikubaliani nalo, na wala hata huelezi inakuwaje Rwanda wagawe lakini sisi tushindwe na Dar peke yake. Tena sio kila raia aliyeko Dar atahitaji kugawiwa chakula.

Hilo la pili; sijui "kile kinatokea" baadhi ya maeneo wanapogawiwa chakula wakati yanapokumbwa na njaa. Ukieleza naweza nikaelewa, na kukubali/kukataa ikibidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…