Hivi ni nani anawatetea wafanyakazi sekta binafsi ukizingatia Rais wa nchi hii ni moja?

Hivi ni nani anawatetea wafanyakazi sekta binafsi ukizingatia Rais wa nchi hii ni moja?

saigilomagema

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2015
Posts
4,683
Reaction score
7,222
Km mtakavyokumbuka tarehe moja mwezi huu wa 5 ilikuwa sikukuu ya wafanyakazi duniani yaani mei mosi. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ndiye aliyekuwa mgeni rasmi.

Wakati wa hutba zake aliwaahidi wafanyakazi wa sekta ya umma mambo mengi mazuri ikiwamo annual increment yaani nyongeza za mishahara ya kila mwaka ambazo zilikuwa zimesimamishwa.

Mambo mengine aliyowaahidi ni nyongeza kubwa sana za posho, upandishwaji wa madaraja kila mwaka zoezi iliyosimamia miaka kadhaa kule nyuma.

Upande wa sekta binafsi hakuna hata neno moja lililosemwa si na kiongozi yeyote wa TUCTA, Waziri wa kazi wala Raisi mwenyewe. Sasa nauliza nani msemaji wa hawa watanzania wenzetu?

Mbona wako km watoto yatima? Mwaka jana serikali ilitangaza nyongeza ya mishahara ktk hii sekta ambayo ingeanza kulipwa mwezi wa Januari, tena ni agizo alilolitoa makamu wa Rais. Nendeni mkafuatilie km kuna mfanyakazi wa sekta binafsi ameongezewa mshahara.

Wafanyakazi wa sekta binafsi annual increment kwao ni hadithi, mfanyakazi kuanzia siku anaajiriwa mpaka anastaafu hakuna kitu km hicho. Hizo zinazoitwa madaraja au posho ni msamiati kwao, yaani ni neno geni wasilofahamu maana yake.

Kuna taasisi zingine binafsi wamekataza wafanyakazi wao kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi ingawa ni hitaji la kisheria. TUCTA nao wapo wapo tu, hawana hata muda wa kufuatilia.

Kwa mfano kuna hivi vyuo vikuu binafsi wafanyakazi wao wanatakiwa wajiunge ama THTU au RAAWU lakini uhalisia hauko hivyo wamekatazwa na kutishwa kuwa hakuna kujiunga na chama chochote cha wafanyakazi.

Fikiria wasomi wazima wako km mandondocha hawawezi kukutana kujadili maslahi na changamoto zao. THTU hawana muda kufuatilia hivi vyuo wao wanahangaika na posho, ni kwamba hawaelewi kuwa hawa walitakiwa kuwa wanachama wao? Na lazima wangelipa ada?

Tunaiuliza serikali ina mpango gani na hawa watanzania wanaonyanyaswa, kuonewa, kudharauliwa na kutishwa ndani ya nchi yao? Nani wa kuwatetea?

Wabunge wetu hata hawajui km kuna sekta binafsi wao wapo kwa maslahi yao.
 
Sekta Binafsi Wengi wana Maisha Mazuri kuliko hao wa Umma.

Ukifanya kazi kwa bidii lazima ufanikiwe.

Sasa hao wa umma wamekalia kuwaza maslai zaidi ya kazi.

Ndio maana hawana maisha mazuri wala furaha.
 
Kifupi hakuna chama cha kuwa tetea na kwa huu uchumi huria na ufinyu wa ajira, waajiri wameshika mpini na serikali haiwezi kuwapangia cha kulipa.
 
Back
Top Bottom