Hivi ni sahihi kiongozi kwenye hotuba yake kutumia dakika 10 kutambua itifaki ya waliopo?

Hivi ni sahihi kiongozi kwenye hotuba yake kutumia dakika 10 kutambua itifaki ya waliopo?

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Posts
60,050
Reaction score
104,466
Sijui Mimi ndio sielewi au ndio utaratibu au ni ujinga wetu wa kiitifaki Africa?

Unakuta kiongozi anapanda kwenye podium wanatumia dakika mpaka 10 kutambuwa itifaki wakati hotuba yake yenyewe ni kama ya dakika saba tu.

Na point yangu hapa kama itifaki ingekuwa ni ya kumtaja Rais tu na kusema itifaki imezingatiwa Nina uhakika hizi events zetu zinazokusanya viongozi wengi wakubwa kwa pamoja tungekuwa tunaweza kuokowa takribani dakika 60 ambazo kimahesabu ni SAA nzima hiyo.

Sasa nauliza na wenzetu ulaya na Marekani mambo ni haya haya ya kupoteza muda au ujinga huu upo Tanzania tu au Africa Mashariki?

Sasa hebu nitoeni ushamba wa itifaki huenda Mimi ndio sijui ni lazima kutaja majina ya viongozi wote kabla ya kuanza hotuba? binafsi nakereka sana kupotezeana muda.
 
Ni upuuzi sana, hili nalo litazameni

USSR
 
Wacha wajinga wapigwe jua Hadi akili ziwarudi siwezi kwenda kukaangwa na jua kisa mwana siasa, mm nitawatazam huku huku ila siyo kwenda kukaangwa na jua la Dodoma.
 
Taahira kaanzisha thread ya kulalamikia mataahira wenzie
 
Sijui Mimi ndio sielewi au ndio utaratibu au ni ujinga wetu wa kiitifaki Africa...
Hapa TZ na katika ma nchi mengine ya kipuuzi ya kiafrika ni kawaida kiongozi sio kutaja itifaki tu bali hata kumsifia mke/mchepuko wake bungeni kwa dakika 20 halafu anachangia kwa dakika 10 tu anaambiwa muda wake umeisha anaketi chini. Hizi nchi za kiafrika ni za kipumbavu sana.
 
Sasa chukua wazo lako nenda Bungeni hesabu dakika wanazopoteza wabunge kwenye kumshukuru Rais na familia zao jumlisha utakuta wanapoteza muda mwingi kuliko kusemea kero za wananchi majimboni mwao.
Bungeni wanaweza kuahirisha shughuli za kujadili kero za wananchi na kuanza kumshukuru raisi. Taifa la hovyo sana hili.
 
Back
Top Bottom