Hivi ni sahihi kwa binamu aliyeolewa kunikopa hela kila mara?

Grau

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Posts
4,828
Reaction score
4,740
Habari zenu wapendwa? Niende moja kwa moja kwenye mada.

Nina dada yangu ambaye mimi nilikuwa namuheshimu sana kutokana na kwamba nilizaliwa peke yangu sina Dada, kaka wala wazazi hivyo nikaona niwe karibu na huyu dada yangu ambaye ni mtoto wa Shangazi,
Mimi nimeajiriwa na serikali kama muuguzi hivyo wakati nasoma chuo huyu dada yangu hakuwahi kuwa karibu kiviile namimi ila mimi niliona ndio mtu wa karibu.

Nilipo maliza chuo nilipata kibarua cha kunishikiza mgodi × baadae mkataba uliisha bahati nzuri nikapata kazi 2018 nikaajiriwa na serikali na ndipo dada yangu alivyo anza kuleta ukaribu namimi, kiukweli alianza kunikopa maana nilikuwa kwenye zahanati na kama ujuavyo, kwenye Zahanati huwa kuna tumarupurupu kwa wale wenzangu wa afya wanajua. Niliona mimi akifanikiwa yeye nisawa kuwa nimefanikiwa mimi.

Kiukweli huyu dada yangu nilikuwa nikimkopa na siku moja ilitokea nikamkopesha 400,000/= alivyo kwama akaongea na Shangazi ambaye ni mama yake eti aongee namimi aniambie mtoto wake kakwama na hiyo pesa sidhani kama ataipata kwa sasa, ilibidi tu nimwambie shangazi waachane na hiyo pesa.

Kuna kipindi huyu dada yangu aliwahi niambia nimkopee milioni 5 Bank ili afanye mambo yake nikagona, aya kuna siku nimempa mtaji mke wangu ili awe anafanya biashara ya viatu ambapo nilikuwa namuagiza huyo dada yangu anatutumia mzigo mke wangu akiuza ukiisha tunamtumia huyo dada yangu hela anatuagizia tena, japo alikuwa akilia shida nampa hela ila ikafikia hatua akanikopa huo mtaji wa mke wangu na sasa namzungusha tu siwezi chukua mtaji kwa mke wangu nimpe yeye, je? Kwa wewe unalichukuliaje hilo swala? Ndugu bhana

N.B nimewapa tu story kwa kifupi nikisema yote nitakuwa naharibu niishie hapo.
 
Mpaka sasa nina kiwanja sijajenga kwasababu ya kusaidia ndugu wasio na shukrani, ndio maana nimesema menine sijaeleza hapo.
Hela hazina undugu mkuu. Subiria hapo upate jeraha la kudumu then usimame kufanya kazi, uone kama kuna ndugu yeyote atakuja kukupa support yeyote hapo.

Badilika kijana.. 🙂
 
Tenda wema nenda zako, kama huwezi kutenda wema acha usinung'unike bure bora lawama kuliko fedheha.
Chakufanya usimkopeshe kuepusha manung'uniko mkuu.

OVA.
 
Kuna binadamu wana asili ya kupe, wao ni kunyonya tu.

Sidhani kama yeye anakuona kama kaka, anakuona ni kibubu chake, akikwama aje kuchota.

Kuna pale mkono unapofika, ukiendekeza uonekane kaka bora utaishia kuwa kapuku.

Kuna wakati katika maisha ni sawa kabisa kusema HAPANA bila ya maelezo mengi.
 
Anakupenda na wewe unalaza damu.Akikulipa siku hiyo mpige kipara hadi tusikie huku akilia
 
Habari zenu wapendwa? Niende moja kwa moja kwenye mada.

Nina dada yangu ambaye mimi nilikuwa namuheshimu sana kutokana na kwamba nilizaliwa peke yangu sina Dada, kaka wala wazazi hivyo nikaona niwe karibu na huyu dada yangu ambaye ni mtoto wa Shangazi,
Mimi nimeajiriwa na serikali kama muuguzi hivyo wakati nasoma chuo huyu dada yangu hakuwahi kuwa karibu kiviile namimi ila mimi niliona ndio mtu wa karibu.

Nilipo maliza chuo nilipata kibarua cha kunishikiza mgodi × baadae mkataba uliisha bahati nzuri nikapata kazi 2018 nikaajiriwa na serikali na ndipo dada yangu alivyo anza kuleta ukaribu namimi, kiukweli alianza kunikopa maana nilikuwa kwenye zahanati na kama ujuavyo, kwenye Zahanati huwa kuna tumarupurupu kwa wale wenzangu wa afya wanajua. Niliona mimi akifanikiwa yeye nisawa kuwa nimefanikiwa mimi.

Kiukweli huyu dada yangu nilikuwa nikimkopa na siku moja ilitokea nikamkopesha 400,000/= alivyo kwama akaongea na Shangazi ambaye ni mama yake eti aongee namimi aniambie mtoto wake kakwama na hiyo pesa sidhani kama ataipata kwa sasa, ilibidi tu nimwambie shangazi waachane na hiyo pesa.

Kuna kipindi huyu dada yangu aliwahi niambia nimkopee milioni 5 Bank ili afanye mambo yake nikagona, aya kuna siku nimempa mtaji mke wangu ili awe anafanya biashara ya viatu ambapo nilikuwa namuagiza huyo dada yangu anatutumia mzigo mke wangu akiuza ukiisha tunamtumia huyo dada yangu hela anatuagizia tena, japo alikuwa akilia shida nampa hela ila ikafikia hatua akanikopa huo mtaji wa mke wangu na sasa namzungusha tu siwezi chukua mtaji kwa mke wangu nimpe yeye, je? Kwa wewe unalichukuliaje hilo swala? Ndugu bhana

N.B nimewapa tu story kwa kifupi nikisema yote nitakuwa naharibu niishie hapo.
"Mtaka nyingi nasaba hupata mwingi msiba"
 
Back
Top Bottom