Hivi ni sahihi kwa binamu aliyeolewa kunikopa hela kila mara?

Hivi ni sahihi kwa binamu aliyeolewa kunikopa hela kila mara?

Tumesha saidiana sana unaju
Ndugu yako ni sahihi kukukopa,ndugu husaidiana sana unajua kuna shida huibuka ambapo unakopa mara moja moja sio mbaya sasa yeye kila wiki nimkope hela. Tena anadharau anaomba hadi nimkopeshe mtaji wangu!
 
Ni pesa ndogo. Lakini mwendelezo wake si mzuri kwa sababu huyo binamu hana mpango kazi. Pia anataka kuvuruga hadi biashara ya viatu. Cha kufanya, huyo binamu anatakiwa asimamiwe, ukiishaona ndugu unamsaidia halafu anafeli mtaji, usiendelee kutoa hela bila kumfanyia tathmini ya kina na mikwara kibao.

Usipende kumpa ndugu samaki bali mpe nyavu avue samaki. Kumkalia kimya siyo kumsaidia bali kumuharibu mana inawezekana anaomba pesa halafu anatumia hovyo hovyo huku jamaa akipambana na anafamilia pia.
Sio kukopa laki 4 tu alisha wahi niambia nimkopee milioni 5 , yaan katika utumishi wangu wa UMMA sijawahi kopa hiyo hela alafu yeye nimkopee yeye afanye mambo yake mimi nikatwe mshahara ihali nina familia.
 
Hela hazina undugu mkuu. Subiria hapo upate jeraha la kudumu then usimame kufanya kazi, uone kama kuna ndugu yeyote atakuja kukupa support yeyote hapo.

Badilika kijana.. 🙂
Nakazia na ndugu hawanaga shukrani ndio hao hao ikitokea hali kama hiyo huwa ndio wakwanza kusema alizembea.
 
Nikimwambia leo sina anapiga tena simu baada ya siku 4 kunikopa tena na anakwambia kwenye mahesabu yako huna hata 300,000/= uniazime
Huyo ni wa kumwambia tu kuwa mwaka huu umebanwa sana, pesa zote unapeleka kwenye projects zako, yaani Kila akikuomba unamtajia projects zako za uongo na kweli, tatizo unaona tabu basi mdanganye kama hivyo.
 
Back
Top Bottom