Hivi ni sahihi mtoto kufukuzwa shule ya msingi kisa hajui kusoma na kuandika?

Hapana. Pamoja na kwamba ni maajabu na siyo sawa mtoto kufika darasa la 3 na hajui kusoma wala kuandika. Hao walimu wanatakiwa wampe special programme ya kumfundisha na siyo kumrudisha nyumbani.

Sasa kama ni hivyo shule ziko kwa ajili gani? Hao wazazi wangeweza kumfundisha nyumbani wangeshafanya hivyo lakini inavyoonekana hawana uwezo huo.

Hiyo special programme wampe kwa gharama za nani sasa??
 
Ila wazazi sisi mmmh🤣
Sasa mtoto anafika hadi darasa la tatu hafuatiliwi maendeleo yake shuleni???
HAjui kusoma wala kuandika mzazi alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kufahamu na kumtafutia msaada
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule ya Serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya Serikali.

Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.

Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani.

Je ni sahihi?
si sawa,
Alipaswa arudishwe aanze darasa la kwanza ili apate msingi mzuri wa kujua kusoma na kuandika.
 
Kkufupi amegoma kuwa na akili

Akili zinatolewa bure yeye kagomea
kuweni na akili basi na nyinyi hana akili? hawajui wazazi wake,hajui kwenda chooni ana jinyea? hajui mema na mabaya? sema tu anatatizo la ubongo kutotunza kumbukumbu sababu ya matatizo mbali mbali iwe ya lishe,afya na saikolojia we ndo huna akili mkuu kwa sababu hujui kutofautisha kati ya kuwa na akili(kujitambua,au kuwa na maarifa) na ubongonkutunza kumbukumbu(kukalili kitu na kukihifadhi kwenye ubongo)
 
English medium schools nyingi huanza kufundisha kusoma na kuandika kiswahili watoto wakiwa darasa la tatu. Je, huyo mtoto alikuwa anasoma somo la kiswahili darasa la kwanza la pili??
Ushauri: Mtafute mwalimu mzuri wa tuisheni wa nursery akusaidie.
 
Primary tulikua na mtu hadi anafika darasa la saba hajui kusoma wala kuandika, tulikua tunajiuliza sana mtihani wa darasa la nne alivukaje hadi leo hakuna jibu.
 
kuweni na akili basi na nyinyi hana akili? hawajui wazazi wake,hajui kwenda chooni ana jinyea? hajui mema na mabaya? sema tu anatatizo la ubongo kutotunza kumbukumbu sababu ya matatizo mbali mbali iwe ya lishe,afya na saikolojia we ndo huna akili mkuu kwa sababu hujui kutofautisha kati ya kuwa na akili(kujitambua,au kuwa na maarifa) na ubongonkutunza kumbukumbu(kukalili kitu na kukihifadhi kwenye ubongo)
Achana na hao mabwege, kama mtoto kafika std3 hajui kusoma na kuandika either kwa english au kiswahili kuna shida sehemu na hyo shida ndo inatakiwa itafutiwe ufumbuzi, ni ufumbuzi unatakiwa na siyo kufukuza. kuna watoto wanamaliza std 7 vijijini huko hawajui kusoma wala kuandika, hapo ni kwamba tatizo lilishinwa kutafutiwa ufumbuzi mapema ndo ikawa hvo.
 
Shule ya kulipia mtoto anafikaje la 3 bila kujua kusoma na kuandika?
 
Sio sahihi, na badala yake walimu walipaswa wamshauri mzazi amrudishe mwanae akaanze darasa la kwanza.
Lakini pia hapo naona kama ni uzembe wa mzazi kutokua mfuatiliaji wa maendeleo ya mwanae alipokua kwenye shule ya kulipia.
Sahihi kabisa alipaswa arudishwe mwaka na sio kufukuzwa shule.
 
Siyo sahihi... kuna watu wanamaliza mpaka la saba huku hawajui kusoma wala kuandika...
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule ya Serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya Serikali.

Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.

Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani.

Je ni sahihi?
Hiyo ni GBV, Gwajima d
 
Hiyo shule ys kulipia alifikaje darasa la 3 hajui kusoma?!
 
Inawezekana wala sababu sio kutokujua kusoma na kuandika, kuna uwezekano dogo anagonga ngeli waalimu wa kayumba hawamwelewi, hebu hili nalo lichunguzwe, huko kayumba watoto kibao wanamaliza la saba hawajui kusoma wala kuandika.
Points
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule ya Serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya Serikali.

Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.

Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani.

Je ni sahihi?
sio sahihi kabisa, arudishwe darasa na aanze kufundishwa
 
Mtoto ameondolewa/fukuzwa shule ya Serikali kisa hajui kusoma wala kuandika.

Mtoto huyo yupo darasa la tatu alikuwa anasoma shule ya kulipia sasa Baba yake kapunguzwa kazini na hivyo kumlazimu kumpeleka mtoto shule ya Serikali.

Lakini cha kushangaza baada ya miezi 3 mzazi anaitwa shuleni na kuambiwa kuwa mtoto hajui kusoma wala kuandika hivyo arudi akasomee nyumbani.

Mzazi akarudishiwa makaratasi yote ya uhamisho na sasa mtoto yupo nyumbani.

Je ni sahihi?
Huo ni mzigo wa serekali sio mzazi. Ni aibu sana kwa mtoto kushindwa kusoma na waalimu wapo
 
Walimu wanalipwa kwa kazi gani, kazi yao kubwa ni kufundisha wanafunzi. Kama mtoto hajui kusoma au kuandika ni jukumu lao kwa kushirikiana na mzazi kujua tatizo la mtoto na kumsaidia.
 
Darasa la tatu hajui kusoma na kuandika, sasa huko shule za kulipia alikuwa analipia nini!?
lazima huyo mtoto atakuwa na matatizo siyo bure, haiwezekani mtoto wa darasa la tatu tena wa private school ashindwe kusoma na kuandika.

Labda anatakiwa aandikishwe kwenye zile special schools huyo mzazi hasemi ukweli.
 
Back
Top Bottom