Hivi ni sahihi mtoto kufukuzwa shule ya msingi kisa hajui kusoma na kuandika?


Hiyo special programme wampe kwa gharama za nani sasa??
 
Ila wazazi sisi mmmh🤣
Sasa mtoto anafika hadi darasa la tatu hafuatiliwi maendeleo yake shuleni???
HAjui kusoma wala kuandika mzazi alitakiwa kuwa mtu wa kwanza kufahamu na kumtafutia msaada
 
si sawa,
Alipaswa arudishwe aanze darasa la kwanza ili apate msingi mzuri wa kujua kusoma na kuandika.
 
Kkufupi amegoma kuwa na akili

Akili zinatolewa bure yeye kagomea
kuweni na akili basi na nyinyi hana akili? hawajui wazazi wake,hajui kwenda chooni ana jinyea? hajui mema na mabaya? sema tu anatatizo la ubongo kutotunza kumbukumbu sababu ya matatizo mbali mbali iwe ya lishe,afya na saikolojia we ndo huna akili mkuu kwa sababu hujui kutofautisha kati ya kuwa na akili(kujitambua,au kuwa na maarifa) na ubongonkutunza kumbukumbu(kukalili kitu na kukihifadhi kwenye ubongo)
 
English medium schools nyingi huanza kufundisha kusoma na kuandika kiswahili watoto wakiwa darasa la tatu. Je, huyo mtoto alikuwa anasoma somo la kiswahili darasa la kwanza la pili??
Ushauri: Mtafute mwalimu mzuri wa tuisheni wa nursery akusaidie.
 
Primary tulikua na mtu hadi anafika darasa la saba hajui kusoma wala kuandika, tulikua tunajiuliza sana mtihani wa darasa la nne alivukaje hadi leo hakuna jibu.
 
Achana na hao mabwege, kama mtoto kafika std3 hajui kusoma na kuandika either kwa english au kiswahili kuna shida sehemu na hyo shida ndo inatakiwa itafutiwe ufumbuzi, ni ufumbuzi unatakiwa na siyo kufukuza. kuna watoto wanamaliza std 7 vijijini huko hawajui kusoma wala kuandika, hapo ni kwamba tatizo lilishinwa kutafutiwa ufumbuzi mapema ndo ikawa hvo.
 
Shule ya kulipia mtoto anafikaje la 3 bila kujua kusoma na kuandika?
 
Sio sahihi, na badala yake walimu walipaswa wamshauri mzazi amrudishe mwanae akaanze darasa la kwanza.
Lakini pia hapo naona kama ni uzembe wa mzazi kutokua mfuatiliaji wa maendeleo ya mwanae alipokua kwenye shule ya kulipia.
Sahihi kabisa alipaswa arudishwe mwaka na sio kufukuzwa shule.
 
Siyo sahihi... kuna watu wanamaliza mpaka la saba huku hawajui kusoma wala kuandika...
 
Hiyo ni GBV, Gwajima d
 
Hiyo shule ys kulipia alifikaje darasa la 3 hajui kusoma?!
 
Inawezekana wala sababu sio kutokujua kusoma na kuandika, kuna uwezekano dogo anagonga ngeli waalimu wa kayumba hawamwelewi, hebu hili nalo lichunguzwe, huko kayumba watoto kibao wanamaliza la saba hawajui kusoma wala kuandika.
Points
 
sio sahihi kabisa, arudishwe darasa na aanze kufundishwa
 
Huo ni mzigo wa serekali sio mzazi. Ni aibu sana kwa mtoto kushindwa kusoma na waalimu wapo
 
Walimu wanalipwa kwa kazi gani, kazi yao kubwa ni kufundisha wanafunzi. Kama mtoto hajui kusoma au kuandika ni jukumu lao kwa kushirikiana na mzazi kujua tatizo la mtoto na kumsaidia.
 
Darasa la tatu hajui kusoma na kuandika, sasa huko shule za kulipia alikuwa analipia nini!?
lazima huyo mtoto atakuwa na matatizo siyo bure, haiwezekani mtoto wa darasa la tatu tena wa private school ashindwe kusoma na kuandika.

Labda anatakiwa aandikishwe kwenye zile special schools huyo mzazi hasemi ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…