Hivi ni sawa hili la kuhubiri ndani ya mabasi ya umma?

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Wadau naomba kuzungumzia kuna hili jambo kwa sasa limezidi kushika kasi kuhubiri ndani ya daladala imekuwa sehemu nyingi hasa mabasi ya Tegeta toka mjini yaaani mnakosa utulivu kwenye mabasi na mwisho wa siku wanachangisha sadaka sasa najiuliza hii hali vipi wadau
 
Ukifika salama ni maombi ya huyo muhubiri pengine unaenda/umetoka kuchepuka
 
Weka ka picha mkuu, na sisi wa Sungangwanda huku tumuone huyo mtumishi wa Mungu.

Kwa maoni yangu ni sawa. Kila mtu ana uhuru wa kufanya atakalo ili mradi hakulazimishi kusikiliza.

Kama hupendi wewe fungulia muziki kwenye simu yako anza kusikiliza.
 
Ni jambo jema!
 
Wewe waangalie wanaotoa sadaka halafu chukua darubini angalia ndani ya ubongo wao Kama utakuta kitu.
Ukikuta mwenye chembe ya akili nidai vocha ya wiki nzima
 
Maisha..
Wasaidie kwa kutoa sadaka.

Mungu atakulipa.
 
Kuna maeneo maalumu yametengwa kwa ajili ya hzo mambo.sio kwenye gar kila m2 na imani yake ni kubuguziana tu.kama ni popote waende hata pale magogoni wakahubiri bhas.watajua awajui
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…