Hivi ni sawa hili la kuhubiri ndani ya mabasi ya umma?

Hivi ni sawa hili la kuhubiri ndani ya mabasi ya umma?

Wadau naomba kuzungumzia kuna hili jambo kwa sasa limezidi kushika kasi kuhubiri ndani ya daladala imekuwa sehemu nyingi hasa mabasi ya Tegeta toka mjini yaaani mnakosa utulivu kwenye mabasi na mwisho wa siku wanachangisha sadaka sasa najiuliza hii hali vipi wadau
Wachawi mnaangaika sana.ukiwekewa singeli ,poa tu kusikia habari njema unapiga kelele
 
Wewe hovyo Sana Yaani habari za Mungu zinakuumiza Ila singeli ndiyo iwe habari njema.Wachawi kazi mnayo.
Wewe una matatizo. Unalazimisha kwamba habari za Mungu ndio njema, Nani kakwambia? Halafu kwani ni lazima kuamini? Tutazifata huko kwenye makanisa tuondoleeni usumbufu kwenye mabasi. Msilazimishe unaloamini wewe kila mtu aamini. Hata mchawi ana haki zake..
Mbona wachawi hawaji kanisani kuhubiri sera zao?
 
Penye wengi pana mengi...tujitahidi kuvumiliana ili tujenge jamii ya watu waliostaarabika.........huwezi kufurahishwa na kila wanalofanya watu kama ambavyo wengine hawafurahishwi na unayoyafanya........msawazo kwenye jamii hauletwi kwa kushindana bali kwa kuvumiliana........
 
Kuna mwaka fulani nilisafiri kipindi cha Pasaka, basi nililopanda wakaweka mawaidha ya dini ya kiislamu, ikawa muda wote ni kuponda ukristo na hiyo sikukuu ya Pasaka.

Ile safari ilikuwa ndefu balaa, na hakuna hata mmoja aliyeweza kumwomba dreva abadili, dreva na kondakta wote wamefuga ndevu.
 
[emoji3][emoji3] ungeshuka
 
[emoji3][emoji3] ungeshuka

Nilikaza mpaka nikafika safari yangu vizuri, mimi hizi bifu za imani huwa najitahidi sana kuzipuuza.

Ila naamini kuna watu walikwazika sana, na walikuwa wanalalamika kivyao bila hata kumwambia dreva wala konda.

Ni sawa na huyu aliyeleta hii taarifa, watu sahihi wa kuwaambia ni hao wahubiri na wahusika wa gari. Kama vipi unakuwa mpole safari inaendelea.
 
Wewe una matatizo. Unalazimisha kwamba habari za Mungu ndio njema, Nani kakwambia? Halafu kwani ni lazima kuamini? Tutazifata huko kwenye makanisa tuondoleeni usumbufu kwenye mabasi. Msilazimishe unaloamini wewe kila mtu aamini. Hata mchawi ana haki zake..
Mbona wachawi hawaji kanisani kuhubiri sera zao?
kiukweli hapo hata akiwa wa dini yoyote yule sio ustaarabu.

binafsi huwa nna waza sana......
kabla ya hawa wenzetu kutuletea hizi dini ,tulikua na dini (Imani) zetu za kimila na mambo yalikua yanaenda.......

wakaja hawa wenzetu kutuletea za kwao ,tukaacha za mababu zetu huko japo hawa wenzetu ni wajanja wajanja sana....waarabu Kwa wamisionari
walikua na mambo yao waloyaficha nyuma ya pazia sio hivi hivi ...

Tukaacha dini za mababu zetu na saivi tumekua "wakereketwa" kuliko hata walotuletea hiyo dini yenyewe.....tupo radhi kuuwana kisa dini za mapokezi ..

Ukereketwa huu umefikia hatua ya kupelekeshana , kutishiana ooh usipofanya hiki cjui mara kile utafikwa cjui na nn , mara toa hiki upate kile .......kufokeana, kuogopeshana nikae natetemeka, sadaka mda mwingine Ka lazima, unaenda nyumba ya ibada ukitaka kutoka linapigwa biti Ka cjui nn .....aisee sipendi
 
Hii ni Kero wanatakiwa wadhibitiwe!

Huwezi kufika tu mahali popote unaanza kubwatuka injili zako!

Makanisa yapo, waende huko wakabwatuke!
 
Wewe una matatizo. Unalazimisha kwamba habari za Mungu ndio njema, Nani kakwambia? Halafu kwani ni lazima kuamini? Tutazifata huko kwenye makanisa tuondoleeni usumbufu kwenye mabasi. Msilazimishe unaloamini wewe kila mtu aamini. Hata mchawi ana haki zake..
Mbona wachawi hawaji kanisani kuhubiri sera zao?
Duuh mkuu umefika mbali..[emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom